nakupenda mume / mke wangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

nakupenda mume / mke wangu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by charminglady, Sep 12, 2012.

 1. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,860
  Likes Received: 1,135
  Trophy Points: 280
  Mu-hali gani wana MMU, mie hapa buheri wa afya,

  Juzi kati nilikuwa maeneo flani, meza iliyofuata waliketi watu wanne. Kati yao walikuwa wanawake wawili na wanaume wawili. Ni watu wa makamo hivi. Mara moja wale wababa akapigiwa simu na mkewe, akapokea. nahisi mke alimuuliza uko wapi? mume akajibu nipo mahali flani na rafik yangu Evance na shemeji yani mke wa Evance. sijui mke alimwambia nini but mume akajibu "nakupenda sana mke wangu na akakata simu"

  swali je hayo maneno yanatosha kukuridhisha kuwa mumen/mkeo yupo mahali salama???
   
 2. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Inategemeana
   
 3. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  inategemea limetumika wakati gani,unajua maana ya neno ipo kwenye muktadha!
   
 4. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Inategemea upande wa pili wa simu huyo baba mtu mzima aliambiwa nini na huyo anayehisiwa kuwa mkewe mpaka akamjibu hivyo kuwa nakupenda sana mke wangu!
  Binafsi sioni tatizo kama walikuwa wamekaa kwa maana ya kuenjoy kwa kupiga vinywaji tu kujiburudisha na kuondoa uchovu wa kazi za mchana.
  Ila kama huyo Evance aliyemtaja hakuwa naye hapo then twaweza kuhisi kuna kamchezo kasiko salama kanafanywa na huyo baba.
  So kwa kifupi maneno kama haya yanategemea na mazungumzo ya wahusika na namna wanavyoaminiana na pia wakati linapotumika.
   
 5. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,123
  Trophy Points: 280
  Hayatoshi chochote usidanganyikeee! Mimi niliwahi kudate na mtu anataka umwabie live kwenye simu nakupeda (umtaje jina) alafu umbusu hadharani, akanikuta master mwenyewe nimeshindikana, simu naweka silent! Nikiona simu yake naenda chooni, basi anaanza na demand zake ahh mi natekeleza, akiridhika nakata simu, huyo mdogomdogo narudi kuendeleza libeneke.
   
 6. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Kwa case ulozungumza wewe mi naona hayo maneno yana maana kubwa sana. Its good ukiwa na jamaa anayeweza ku declare publicly feelings zake kwako.

  Ningechukia angesema "me too"

  Mimi wa hivyo anakuwa keshaniloga walahi. Napenda kweli maneno matamu, hasa yakitamkwa adharani.
   
 7. nasnee

  nasnee Member

  #7
  Sep 12, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  inategemeana how do they treat each other and by ze wa ha2jui walikua wanajibizana nn,so itakua ngumu kutoa judgement..............
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Mtu akisema hadharani ina maana hata kama yupo na mwingine
  wewe ni first kwake
  hamuogopi huyo wa pembeni
  labda hiyo ndo point...

  kwamba yuko na mwizi na mwizi anajijua kuwa ni mwizi lol
   
 9. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  YES and NO.

  Anaweza akawa na kimada bado akatamka hayo maana kimada haogopeki na wengi wao hua wanajulishwa kabisa kuwa mwenye nyumba yupo.

  Au. . .anaweza akawa anamaanisha na wala haoni ugumu kutamka hivyo mbele ya watu kwasababu anajivunia wewe kuwa mume/mke wake. Hii ya pili ni raha sana. Hata pale anapokuwa haishi kukusifia/sema anavyokupenda kwa watu wake wa karibu wakati wewe haupo. Unaishia kuambiwa tu siku ukikutana nao.
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280

  mhhhh kuumbee?
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Sep 13, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Wewe mubaya wewe
   
 12. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,378
  Trophy Points: 280
  Ila sometime unakupa matumaini kuwa yuko safe, na unaona hawezi kuwa na mtu maana ametamka hadharani kuwa anakupenda, so kama kuna hawara hapo anajua kabisa kuwa hapendwi yeye.
   
 13. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,860
  Likes Received: 1,135
  Trophy Points: 280
  wadau, nimesema hivyo kwa sababu niliwahi kudate na mkaka flani. yan yeye alikuwa na wivu mpaka kero. kila anapopiga simu swali la kwanza upo wapi, unafanya nini. utamjibu kisha baada ya mazungumzo ananambia haya nambie hv "nakupenda sana mume wangu" while ni bf. mara nikiss,haijalishi upo sehemu gani,iwe kazini upo na wateja, iwe upo ofisi za watu ye atataka hayo yote. ukisita anasema namcheat. kiukweli tulishindwa kwa tabia hizo. . . ina maana hayo maneno yanamlinda mtu asi-cheat?????
   
 14. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0

  akushindi wewe NN
   
 15. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #15
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  yanamuhakikishia mtu kuwa kwa wakati wowote na muda wowote akikuambia uyaseme unayasema,uwezekano wa ku cheat ni mdogo na kama una cheat basi aliye pembeni yako kwa wakati huo yaani mwizi ajijue yeye ni mwizi tu,yupo mmiliki halali!na ni maneno ya kawaida kutumika ktk mahusiano ya ndoa,mimi huwa naamini hata kama mume anataka kuiba kwa wakati ule anapoyatamka,kwanza yanaweza kumkera hawara aliyenae,na pia yanamrejeshea fahamu mume /mke ya kukumbuka anachotaka kufanya ni dhambi!
   
 16. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,350
  Likes Received: 2,687
  Trophy Points: 280
  CL hiyo ni hulka tu ya baadhi ya wanaume ambao hawajiamini na ndio maana alikuwa anajump kwenye conclusion pindi matarajio yake yalipokuwa kinyume.
  Wapo wapenzi ambao kuambiana neno "nakupenda" ni nadra sana lakini matendo yao utagundua tu jinsi walivyoshibana. Binafsi huwa naamini maneno matupu hayavunji mfupa maana upendo wa kweli huonekana katika matendo maneno ni mbolea tu
   
 17. neggirl

  neggirl JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2012
  Joined: Jul 30, 2009
  Messages: 4,830
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Maneno pekee hayatoshi.. Lakini yakienda sambamba na imani uliyonayo kwa mhusika yanaweza yakatosha. Kuna uwezekano kuwa hakuwa na mahusiano yoyote tata na mmojawapo ya hao wanawake aliokaa nao... au hata yapo. But nampa CREDIT ya kuweza kusema na wakasikia kwamba NAKUPENDA MKE WANGU.. pia kusema hivyo bila kuuma uma kunaweza kumjengea mkewe imani zaidi.
   
 18. V

  Von Mo JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 1,830
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
   
 19. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #19
  Sep 13, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe ailimia 250%. Lol.

  Hata kama alikuwa amekaa na kimada ...suala hapo ame prove kuwa wewe ni number one.
  Otherwise asingetamka hayo.

  Ukimpenda mtu kweli kweli hayo maneno hayawezi kuwa mazito kutamka...tatizo wengi ni wizi mtupu!

   
 20. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #20
  Sep 13, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Na unaweza kumkamata cheater kwa maneno tu...ukianzisha dirty discussion kwenye simu afu yeye yuko na mtu pembeni lazima ajione mdogo na aume ume maneno.

  Mi napenda huo utamaduni aisee...it makes me feel confident.

   
Loading...