Nakumbuka Kenya

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
219
Nimefanikiwa tena kufika laiser hill academy shule ambayo niliwahi kusoma shule ya msingi kwa kipindi sha miaka 3 kuanzia mwaka 1996 , nilipofika hapa nimekumbuka mengi na kuwaza mengi sana kila ninapoangalia mambo na vijimambo vingine .

Kwanza nilisikia mwalimu mmoja niliyekuwa namchokoza sana bwana omondi ameshafariki dunia , na wengine wengi ambao wameshaacha kazi , wengine wamekimbilia katika fani zingine na kuacha kazi ya kujitolea ya ualimu .

Nikakumbuka mara ya kwanza nilipokanyaga hapa laiser hill academy , mimi na wadogo zangu 2 wote tulinunuliwa vitu kutoka Tanzania nakumbuka ilikuwa mkoani arusha , vitu ambayo tumezoea kuvitumia toka enzi hizo .

Baba yetu alipotuacha hapa na kutukabidhi kwa mkuu wa bweni letu mambo yalibadilika , yule mkuu kwa jina aliitwa Mr Otwanee , alitoa vitu vyote vilivyoandikwa made in Tanzania na kutupa vya kikenya .

Kisha tulienda kukaribishwa mlo wa jioni , humo ndani tulikutana na vitu kama sukuma wiki , na vyakula vingine ambavyo vilikuwa ni vigeni sana kwetu na hatukuwahi kufikiria kwamba tunaweza kubadilikiwa .

Siku moja tulitoka kwenda katika mbuza za wanyama karibu na Nairobi , kabla ya kwenda kule unatakiwa kununua vitu kama vyakula , vinywaji na kadhalika , tulipotoka shule tulipelekwa super market Fulani inayoitwa Nakumat .

Ukifika Nakumat kila unachoangalia ni made in Kenya kuanzia sausage , biskuti , juice na kadhalika , ni tofauti sana na mtoto anayesoma st maries akitoka weekend anapelekwa GAME mlimani city anaenda kununua apple za afrika kusini , mashati ya kikenya , mafuta ya kongo .

Tuliporudi nyumbani tulianzisha ugomvi na mama , kwa sababu tulishazoea vitu na mali za Kenya , ukiletewa nguo unaangalia imetoka wapi , viatu kama ni bora ya Kenya , colgate kama ni kutokea Kenya NIDO , OMO , Sausage na vitu vingine vidogo vidogo .

Ndio maana ukitembelea tovuti za wakenya kama www.mambogani.com unaona kila memba ana lebo ( AM PROUD TO BE KENYAN ) kweli lazima mtu awe proud si kila kitu anatumia chake ? wasi wasi na mashaka ya nini ?

Uwe na siku njema
 
kuna uwezekano kuwa wewe ndiye mwenye hii profile ya "shy"?....mmmmmh!...ila ahsante!
 
Back
Top Bottom