Nakulilia Ivon Njochanilo, Ulimwengu utasimama na Wewe

Mwandishi, umeandika uzi mrefu wa kuvuta hisia kweli kweli, nakupongeza kwa hilo. Ila tuijadili kesi hii kwa kifupi tuweke hisia pembeni;

1) Hata kama mtu ametokea kijijini, huwezi kudanganywa kirahisi kiasi hicho na ukakubali kosa. Labda awe sio mzima kiakili.

2) Hakimu ana kosa gani hapo??? Mtu kakiri kwamba ametenda kosa, kuna kipi cha ziada cha yeye hakimu kung'ang'ania ushahidi wa ziada??? Sheria inasema mtuhumiwa akikiri kosa mara tatu basi hakimu anatakiwa kutoa hukumu moja kwa moja.

3) Kuna ushahidi gani ukiachia maneno, kuthibitisha kwamba hilo kosa hajatenda mtuhumiwa???

4) Hukumu ya kulawiti mtoto wa chini ya miaka 8 ni maisha na sio miaka 30.

2) Hakimu na baraza la wazee katika kushauriana ilitakiwa washauriane huku mezani kuna vielelezo. Mleta uzi anasema vielelezo havikuwepo, kama ni kweli havikuwepo hii inamaanisha hakimu ametoa hukumu ila hajacover angle ya 'beyond reasonable doubts'
 
Mkuu, mshukuru Mungu kama hayajakukuta. Watu wengi hurubuniwa kukubali kosa ili yaishe na wamefungwa. Ama hawakutenda kosa au walitenda ila ushahidi haujitoshelezi, polisi/mpelelezi anamshawishi mtuhumiwa akubali kosa kwamba alishaongea na hakimu kamuahidi ataifuta kesi au atampa adhabu ndogo hata ya fine ya 50K.
Ni habari ya kusikitisha. Lakini habari hii ingeleta hisia kali zaidi kama ungegusia na maelezo japo kwa uchache toka upande wa pili, yaani dada na mama mkubwa. Yawezekana wangekupa maelezo yasiyo sahihi kwa asilimia mia ili kulinda upande wao, lakini kwa saikolojia yako ungebaini kama kijana alifanyiwa njama, alionewa, au la.

Dada mtu ndiye aliyempeleka kijana polisi, wakati mama aliyemleta kijana mjini akiwa safarini, kijana amekaa mahabusu mwezi mmoja, katika kipindi hiki cha mwezi mzima, huyu mama lazima alikuwa amerudi toka safarini. Je, huyu mama alipofika nyumbani na kukuta kijana yuko mahabusu hakuchukua hatua juu ya suala hili zito? Na ikumbukwe yeye ndiye aliyemleta kijana kwake na hivyo alikuwa chini ya himaya yake, hivyo usalama, afya, na malezi kwa ujumla, ni juu ya huyu mama. Haya ndio ulitakiwa uambatanishe na hayo uliyotuandakia ili na sisi tupate vionjo halisi vya jambo lenyewe.
 
dunia imekaa segemnege sana,kiasi kwamba inakuwa ngumu kukubali moja kwa moja kijana IVO kaonewa.

miaka 19 inatosha kabisa yeye kufanya akichoshitakiwa nacho.

walalamikaji hawaonyeshi kuwa na nia mbaya na mtuhumiwa tokea wameamua kuishi naye.

pia haiingii akilini kwamba pesa imetembea kupindisha kesi,maana kwa maelezo ya mleta mada familia yenye mhanga wana maisha ya chini tu.

kesi za ubakaji na mauaji,ni kesi mbaya tena za kutisha ambazo ni ngumu pia,kiasi cha polisi wanaopewa wazipeleleze kuwa makini sana,tamaa ya pesa mara nyingi hukaa kando hapo.
 
Mkuu kuna watu wa namna hiyo. Ni rahisi kabisa kudanganywa. Kwa maisha ya kifanya na tamaduni za kule, nashawishika kuwa ilikuwa rahisi sana kwa kijana yule kumuamini askari, maana atakuwa alivaa koti na kujitanabaisha kwamba yeye ni msaada kwake.
Dunia ina mengi mno
asante ndugu Mungu akubariki
 
pia haiingii akilini kwamba pesa imetembea kupindisha kesi,maana kwa maelezo ya mleta mada familia yenye mhanga wana maisha ya chini tu.
Sisi hatujasema kuwa kuna pesa yoyte imetembea, tumeomba tu msaada wa kusaidiwa rufaa ya kijana wetu. Na tumeweka na angalizo kuwa hii jambo lisihusishwe na familia, tumeeleza tu tukio
 
Mpelelezi wa kesi hii, wakati anampeleka Mahakamani alimrubuni kijana huyu kuwa, kesi hii ilikua ni nyepesi tu kwahio alichotakiwa kufanya ni KUKUBALI kosa na Mheshimiwa Hakimu angemuachia huru.👈🏼 sina cha kuchangia, alichokifanya huyo dogo ni upumbavu haswaa.
 
shukrani
 
Sisi hatujasema kuwa kuna pesa yoyte imetembea, tumeomba tu msaada wa kusaidiwa rufaa ya kijana wetu. Na tumeweka na angalizo kuwa hii jambo lisihusishwe na familia, tumeeleza tu tukio
Inavyoonekana ni kama unataka dogo ahurumiwe.
Lakini kwa maelezo yako inaonyesha dhahiri huyo kijana IVO alikuwa anamlawiti huyo mlawitiwa sema tu katika kuelezea umejaribu kunyoosha baadhi ya mambo ili simulizi yako ikae vizuri
ILA yote kwa yote RUFAA ipo mkuu
 
Ni habari ya kusikitisha. Lakini habari hii ingeleta hisia kali zaidi kama ungegusia na maelezo japo kwa uchache toka upande wa pili, yaani dada na mama mkubwa. Yawezekana wangekupa maelezo yasiyo sahihi kwa asilimia mia ili kulinda upande wao, lakini kwa saikolojia yako ungebaini kama kijana alifanyiwa njama, alionewa, au la.

Dada mtu ndiye aliyempeleka kijana polisi, wakati mama aliyemleta kijana mjini akiwa safarini, kijana amekaa mahabusu mwezi mmoja, katika kipindi hiki cha mwezi mzima, huyu mama lazima alikuwa amerudi toka safarini. Je, huyu mama alipofika nyumbani na kukuta kijana yuko mahabusu hakuchukua hatua juu ya suala hili zito? Na ikumbukwe yeye ndiye aliyemleta kijana kwake na hivyo alikuwa chini ya himaya yake, hivyo usalama, afya, na malezi kwa ujumla, ni juu ya huyu mama. Haya ndio ulitakiwa uambatanishe na hayo uliyotuandakia ili na sisi tupate vionjo halisi vya jambo lenyewe.
Mkuu umechanganya. Mtoa mada si mimi.
 
Back
Top Bottom