Nakuita Hivi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nakuita Hivi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, May 3, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 3, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nakuita wewe chanda,
  Uliye wangu nyonda
  Pekee ninakupenda
  Mimi nakuita hivi; au vile!

  Ninakuita habiba
  Uloichomoa miiba
  Ukantuliza shurba
  Mimi nakuita hivi; au vile!

  Nakuita waridi
  Ewe ua la ahadi
  Pendo lako ni zawadi
  Mimi nakuita hivi; au vile!

  Nakuita Malkia
  Mtawala ulonijia
  Na moyo kuniachia!
  Mimi nakuita hivi; au vile!

  Ninakuita Faraja
  Ulochagua umoja
  Ya penzi letu la haja!
  Mimi nakuita hivi; au vile!

  Ninakuita wangu
  Wangu peke yangu
  Kwa ardhi na kwa mbingu
  Mimi nakuita hivi; au vile!

  Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  May 3, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Ebana naomba kulitumia hili.....kuna shori mmoja hivi ana play hard to get lakini nikimshushia hii mistari ataingia tu kwenye kumi na nane...
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  May 3, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  ruhusa granted!.. no attribution necessary..
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  May 3, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Thanks man....will let you know the outcome
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  pole mzee MMM huyu anayekuzengua kweli this time umepatikana kweli utamalisha mashairi yote duniani
   
 6. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Kwani Mzee MMM imekuwaje siku hizi? Naona punde utatoka kwenye Kilimo kwanza hadi kwenye uwanja wa Malenga...lol
   
 7. C

  CLAY KITUMBOY Senior Member

  #7
  May 4, 2010
  Joined: Sep 8, 2009
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wonderful stuff
   
 8. T

  Tall JF-Expert Member

  #8
  May 4, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  endelea kumwita wangu peke yangu na ubarikiwe sana.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  May 5, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  mmh.. si unajua tena.. kuishi kwingi kuona mengi!

  Nipo hapa nawasikiliza Vijana na wimbo wao "Maria wangu"..!

  those were the days
   
 10. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #10
  May 6, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Nyani Ngabu,umenichekesha.Umezoea copy and paste tunga ya kwako ndio umpelekee huyo shori wako..Akishakukubali nani atakuwa anakupa mistari ya hapa na pale?utarudi tena kwa Mwanakijiji?
   
Loading...