'Nakufahamu' au 'Nakujua' ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Nakufahamu' au 'Nakujua' ?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by SMU, Jan 9, 2009.

 1. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,932
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Kuna tofauti kati ya maneno kufahamu na kujua. Kwa mfano Mtu ukisema 'namfahamu vizuri sana Anna' kuna tofauti na kusema 'namjua vizuri sana Anna'?
   
 2. Bonnie1974

  Bonnie1974 JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 407
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mzee where are you heading?
  Wacha hizo mkulu......teh...teh....teh
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Adam AKAMJUA mkewe, akazaa mtoto wa kiume akamwita Kaini, ... akaMJUA tena akazaa wa pili akamwia Abel ........... akaMJUA tena, akamzaa Lameck........
  Haya maneno wala sijui yamekaaje. Ni sawa na Kukazana au MTU MZIMA.....
   
 4. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,932
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Duh! Kumbe inawezekana ni matusi eenh:)?
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,547
  Trophy Points: 280
  Kumfahamu ni kuwa na taarifa za huyo mtu/kusikia habari zake/kumuelewa. Kumjua mtu, ni kumwelewa kwa undani. Ukiulizwa unafahamu Kiingereza?. Jibu likiwa ndiyo, maana yake unafahamu kuwa Kiiingereza ni moja ya lugha na wenyewe ni Waingereza/Wangereza. Ukiulizwa kama unajua Kiingereza, maana yake ni kuijua-lugha ya Kiingereza kwa kuizungumza/
  Kuisoma na kuandika.
  Ile ya Adam kumjua Mkewe ni kukosekana kwa tafsiri ya neno "Carnal Knowledge" by then, tafsiri ya sasa ni 'kumuingilia'
   
 6. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #6
  Jan 10, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  unaposema una mfahamu mtu kwa ujumla inaishia kwenye tabia nk.Lakini unaposema unamjua mtu unakwenda mbali zaidi.Ina maana hata maumbile yake ya nje unayafahamu.Huu ndio ufahamu wangu.

   
Loading...