Nakubali serikali mbili, lakini ningependa ziwe Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar....

Chris Lukosi

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
4,581
2,937
Ndugu zanguni,

Mimi nimekubali kabisa tena kwa moyo mkunjufu serikali mbili.

Napendekeza hizo serikali mbili ziwe kama ifuatavyo

SERIKALI YA TANGANYIKA

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Nadhani kwa muundo huu kutakuwa hakuna kelele tena kwa sababu kila mtu atakuwa bize kivyake....

tz-tng.gif
 
Hapo muungano una nafasi gani ? Hivyo ndivyo ilivyokuwa January, 1964 kabla ya Muungano.

Kwa maneno mengine unapendekeza muungano uvunjike.

Ndugu zanguni,

Mimi nimekubali kabisa tena kwa moyo mkunjufu serikali mbili.

Napendekeza hizo serikali mbili ziwe kama ifuatavyo

SERIKALI YA TANGANYIKA

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Nadhani kwa muundo huu kutakuwa hakuna kelele tena kwa sababu kila mtu atakuwa bize kivyake....

tz-tng.gif
 
Kwa marekebisho yanayopendekezwa na CCM ndivyo itakavyokuwa. Kutakuwa na serikali mbili: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo kiukweli itakuwa ni serikali ya Tanganyika kwa kuwa haitakuwa na mamlaka Zanzibar (hii ni baada ya Zanzibar kujichukulia/kupewa mamlaka inayodai).
 
Kwa hiyo umehalalisha kuvunjika kwa Muungano,

Uongozi wa CCM naomba wamwombe Askofu Mtetemela awafundishe kuhusu Mfalme Belishaza wa kule Babeli, alipoona maandishi yameandikwa ukutani, alishindwa kuyasoma akalia kwa sauti, ''NENDENI MKAMUITE DANIEL"
Mengine atawafafanulia, Lakini kwa mwanajamvi kasome, Kitabu cha Nabii Daniel 5:1-31

CCM wamepigwa upofu na kiburi cha madaraka, hawawezi tena kuona kilichoko mbele yao, hawawezi kuona kilichoko nyuma yao, hawawezi kuona kilichoko kati mwao. Asomaye na afahamu.....
 
Nje ya Muungano hakuna Zanzibar.....Kuna Unguja na Pemba nataka ulijue hilo---Mwl JK.

Ila kuna nini? Unao ushahidi kwa hayo unayosema au ulimsikia mtu fulani na ukaanua kumeza huo mseno bila kutafakari.

Zanzibar ilikuwepo kabla ya Muungano, tena ilikuwepo kabla hata Tanganyika kuwepo. Iweje leo useme nje ya Muungano Zanzibar haipo?

Historia inathibitisha kuwa Seyid Said alihamia Zenjibar miaka ya 1840.
 
Ndugu zanguni,

Mimi nimekubali kabisa tena kwa moyo mkunjufu serikali mbili.

Napendekeza hizo serikali mbili ziwe kama ifuatavyo

SERIKALI YA TANGANYIKA

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Nadhani kwa muundo huu kutakuwa hakuna kelele tena kwa sababu kila mtu atakuwa bize kivyake....

tz-tng.gif

mkuu siku izi unatumia akili sana kufikiri, big up......
lakini mkuu huu si ndo msomamo wa ccm siku zote? kuwa serikali huru ya Zanzibar, na serikali ya jamhuri ya Watu wa Tanzania. Serikali ya Jamhuri ndo itatoa rais na ndo anaitawala tanganyika kwa ukamilifu na Zanzibar nusu
Tanganyika tunakupenda kwa moyo wote!
 
Ndugu zanguni,

Mimi nimekubali kabisa tena kwa moyo mkunjufu serikali mbili.

Napendekeza hizo serikali mbili ziwe kama ifuatavyo

SERIKALI YA TANGANYIKA

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Nadhani kwa muundo huu kutakuwa hakuna kelele tena kwa sababu kila mtu atakuwa bize kivyake....

tz-tng.gif

Unataka yakukute yaliyomkuta Mansour? Nachelea kusema kwa msimamo wako huo, huenda yale uliyokutana nayo Chadema yakawa madogo!
 
Kama kuna mtu hata mmoja alifia Tanganyika kwa nn tuliobaki tusiwe na haki ya kuuliza ilipo?

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Kwa hiyo umehalalisha kuvunjika kwa Muungano,

Uongozi wa CCM naomba wamwombe Askofu Mtetemela awafundishe kuhusu Mfalme Belishaza wa kule Babeli, alipoona maandishi yameandikwa ukutani, alishindwa kuyasoma akalia kwa sauti, ''NENDENI MKAMUITE DANIEL"
Mengine atawafafanulia, Lakini kwa mwanajamvi kasome, Kitabu cha Nabii Daniel 5:1-31

CCM wamepigwa upofu na kiburi cha madaraka, hawawezi tena kuona kilichoko mbele yao, hawawezi kuona kilichoko nyuma yao, hawawezi kuona kilichoko kati mwao. Asomaye na afahamu.....

du kiswahili kimepanuka , hata Babeli walikuwa wanaongea kiswahili? duh!!
 
mkuu unatakiwa kuwa na msimamo. MIE nataka taifa la TANGANYIKA lililopata UHURU 9/12/1961
Ndugu zanguni,

Mimi nimekubali kabisa tena kwa moyo mkunjufu serikali mbili.

Napendekeza hizo serikali mbili ziwe kama ifuatavyo

SERIKALI YA TANGANYIKA

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Nadhani kwa muundo huu kutakuwa hakuna kelele tena kwa sababu kila mtu atakuwa bize kivyake....

tz-tng.gif
 
Vyovyote itavyo kuwa sawa
Ila
1. Zanzibar kubaki nchi (taifa)
2. Na mipaka ya nchi ya Zanzibar
3. Uwepo wa serekali ya Zanzibar
A. Baraza la wawakilishi
B.mahakama
C.baraza mawaziri
4. Uwepo wa mzanzibar
5. Uwepo wa rais wa Zanzibar mkuu wa nchi na kamada mkuu wa vikosi vyote cya SMZ.

MAMBO HAYA HAYAJADILIWI WALA HAYANA MBADALA ILA WAZANZIBAR WAKUBALI KWA KURA YA MAONI.

kaxi kwenu ktk mengine tutaamua kwa kura ya wazi dodoma .
 
05/03/2014 ulipendekeza Muungano uvunjike kabisa:
Hivi watanganyika wenmzangu tatizo lenu nini?

Kwa nini tuendelee kubebeba hii misumari?

Tunafaidika nini na huu muungano ?

Ni wakati umefika tubwage manyanga

JITAMBUE!
22/03/2014 JK alipohutubia ukabadili msimamo na kumfuata, ukaunga mkono serikali mbili, ya Muungano na ya Zanzibar:
...Hotuba aliyoitoa Rais Kikwete jana imenibadili kabisa msimamo wangu kuhusu muungano na ninakubaliana nae kuwa dawa ya kutatua mgogoro wa ndoa sio kuvunja ndoa bali kuyaondoa yale yanayosababisha ndoa iwe chungu...

25/03/2014
zimepita siku tatu tu tangu ulipomuunga mkono JK, leo unataka serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar:
Ndugu zanguni,

Mimi nimekubali kabisa tena kwa moyo mkunjufu serikali mbili.

Napendekeza hizo serikali mbili ziwe kama ifuatavyo

SERIKALI YA TANGANYIKA

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Nadhani kwa muundo huu kutakuwa hakuna kelele tena kwa sababu kila mtu atakuwa bize kivyake....
Inaelekea unachanganywa sana na upepo kila unapopita. Jambo la msingi ni kusikiliza hoja za watu, kuzichanganya na zako, kuzichambua, ndipo kuja na msimamo wako. Vinginevyo utakuwa unabadilika kila inapotolewa hotuba!
 
05/03/2014 ulipendekeza Muungano uvunjike kabisa:

22/03/2014 JK alipohutubia ukabadili msimamo na kumfuata, ukaunga mkono serikali mbili, ya Muungano na ya Zanzibar:

25/03/2014
zimepita siku tatu tu tangu ulipomuunga mkono JK, leo unataka serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar:

Inaelekea unachanganywa sana na upepo kila unapopita. Jambo la msingi ni kusikiliza hoja za watu, kuzichanganya na zako, kuzichambua, ndipo kuja na msimamo wako. Vinginevyo utakuwa unabadilika kila inapotolewa hotuba!

Umemkamatia bafuni mkuu!! Tena akiwa uchi wa mnyama, nguo zake umezitia kwapani, Haya akimbie sasa kama ana roho ngumu!! Hahahahaaaaa
 
Vijana kama hawa ndio tunawaitaji nchi hii wazo zuri kijana nitakufikiria nafasi ya kukuweka!
 
Wanabodi!!!

  1. Unawachukua wabunge 80 toka Visiwani (kwa miaka50!) wanakaa Dodoma wanajadili Barabara za Geita na Katavi. Unawalipa msharahakila mwezi na posho kwa kodi toka Tanganyika!
  2. Unammchukua Makamu wa Raisi, Mawaziri, Mabalozi na 20% ya wafanyakzi wa Wizara za Muungano toka visiwani.. kisha unawalipa mishahara na posho (kwa miaka 50!) kwa kodi za Watanganyika!
  3. Tunajuinga na Afrika Mashariki. Bara wanalipia pesa ya kodi gharama za Afrika Mashariki.. Wabunge ni 9 kama walivyo wabunge toka Rwanda (9), Kenya (9). Then!!!!! Tanyanyika inatoa Wabunge (6) Na Visiwan iwabunge (3). Then Bara kwa kodi zao unawalipia wabunge wa Visiwani katika Bungela Afrika Mashariki!!!
  4. Unawateua wabunge toka Visiwani kamati za Bunge Muungano kukagua barabara kule Ngara na Tandahimba unawalipa pesa ya kodi ya Tanganyika kwa miaka 50!
  5. Halafu unakaa unajivuna Muungano huu ni waKuigwa Bara la Afrika na Dunia yote na unajipiga2 kifua kuwa na fikra sahii za waasisi wa Taifa hili!
  6. Miaka 50! Wewe unakuwa rafiki au mshirika wangu!Siku zote tukionana mimi nakununulia tu soda au bia wewe.. wewe hata siku mojahaununui… na unaona ni poa tu! Kwa mika 50!
  7. Halafu watoto wetu wa shule kule Handeni naKondoa wanakaa Chini hawana madawati na tunalalamika na kuona ni sawa!

SAA INGINE NAONA KAMA TANGANYIKA AU TANZANIA BARA TUMEROGWA AND WE ACTUALLY DO NOT KNOW OUR PRIORITIES!
WATOTO NA WAJUKUU ZETU WATAULIZA SIKU MOJA NA HATUTAKUWA NAMAJIBU!

WATANGAYIKA TUAMKE TUACHE UNAFIKI HUU!
 
Back
Top Bottom