Nakosa mke kisa dini

Nakosa mke kisa dini

Cogito ergo_sum

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2016
Posts
1,648
Reaction score
2,930
Huyu mchumba wangu tumekuwa pamoja katika mahusiano takirbani miaka miwili ila tuna tofauti za kidini yeye Muslim mimi ni Catholics.

Tulikuwa tumepanga mwaka huu tufunge pingu za maisha (ndoa) ila tatizo amejaribu kugusia hilo swala kwa wazazi wake na kuwambia kuwa mimi ni dini tofauti wamekataa kabisa hawataki aolewe na mtu ambae sio dini yake.

Wamemwambia kuwa watamtenga.Wanasena mwanamke hana dini ila ikija wa kwao anataka kuolewa wanakataa.

Wakuu nifanyeje hawa wazazi wanipe mke?

Naomba ushauri wenu wakuu namna ya kulisolve hili swala.
 
duh je wakikataa pia itakuwaje mkuu ?
Mkuu unacho takiwa kufanya weka mipango ya kumpa mimba mwanamke akisha pata mimba usiende kujitambulisha ukiona bado wanazingua mtoto akifika miaka kadhaa weka nyingine mwisho wataruhusu wenyewe

Hii mbinu ilitumika na rafiki yangu mpaka leo hawasalimiani na mama mkwe

Ila maisha yanasonga kama kawaida

Ila ukiamua hivyo inabidi umpe semina ya kutosha huyo mpenzi wako nawe uwe mvumilivu
 
Watoto wa kondoa wana dini hatar, hapo hamna namna kama hutobadili dini huyo ndo bye bye
 
Huyu mchumba wangu tumekuwa pamoja katika mahusiano takirbani miaka miwili Ila tuna tofauti za kidini yeye Muslim Mimi ni CATHOLICs .Tulikuwa tumepanga mwaka huu tufunge pingu za maisha (ndoa) Ila tatizo amejarbu kughusia Hilo swala Kwa wazazi wake na kuwambia kuwa mimi ni dini tofauti wamekataa kabisa hawataki aolewe na mtu ambae sio dini Yake a
Wamemwambia kuwa watamtenga.
Wanasena mwanamke hana dini iila ikija wa kwao anataka kuolewa Wanakata duh!

Duh wakuu nifanyeje hawa WARANGI wanipe mke.
Naomba ushauri wenu wakuu namna ya kulisolve hili swala.
Hao ni wadini balaa.
Kijiji cha Haubi asilimia kubwa ni wakristu tena RC, kwa vile marehemu Askofu isuja alitoka kule.
 
Tafuta mrangi mwingine, usipoteze muda
 
hili swala huwa linatesa watu wengi sana hata mimi mwanzo lilinisumbua lakin mwisho wa siku yalieleweka
 
Mimi pia yalinikuta hayo ,alikuwa ni mtoto wa alhaji swala tano,nikafanya yafuatayo;
1.Nikampa Mimba
2.Ndugu zake karibu wote walinisusa
3.Tukafunga ndoa bomani akiwa na mimba ya miezi nane
4.Tukabariki ndoa kanisani katoliki
5.Maisha yakaendelea ,ndugu wote wakawa marafiki
6.Bahati mbaya ndoa ilikuja kuvunjika baada ya miaka mingi..
 
Kama umelishwa sumu ya upendo kwake unaona hata kwa maziwa hautapona basi usipoteze muda we badili dini tena kwa haraka usichelewe,
 
Back
Top Bottom