Mama watoto wangu, wazazi wake wamekataa mtoto wao asibadili dini ili tuweza kuwa mume na mke

mafoleni

JF-Expert Member
Nov 18, 2016
220
371
Mara kadhaa nimekuwa nikileta mada ya kuhusu mama watoto wangu ambae ni Islamic na wazazi wake wamekataa mtoto wao asibadili dini ili tuweza kuwa mume na mke mbele ya MUNGU kwa sababu Mimi ni Christian.
Ukweli ni kwamba tumetoka mbali sana kimaisha toka tulipokuwa tumepanga mpaka kujenga na Maendeleo mengine ya kibiashara.
Nimejaribu kuvumilia sana nikijua huenda atabadili mawazo na kuamua kwenda kinyume na wazazi ili kunifata Mimi ili tuweze kuoana lakini mwenzangu anasikiliza maamuzi ya wazazi.
Kiukweli sasa imefikia stage naona kama tunapotezeana muda tu. Nikajiuliza maswali mengi sana mpaka nikaamua sasa kutafuta mkristo mwenzangu ili niweze fanya mipango ya ndoa. Ila kwa kuwa tayari nimezaa nae nikaona sio mbaya nimuache kwenye nyumba tuliyojenga akae na watoto kisha mi nikapambana kujenga nyingine ambayo nitaishi na huyo nitakae muoa.
Kikubwa kilichofanya niombe mawazo ya ndugu Zangu humu tatizo ni hili hapa:
1..YUPO KWAO NA HATAKI KURUDI KWAKE
2..ANATAKA NIMUHUDUMIA AKIWA HUKO HUKO
3..HATAKI KUONA HUYU ANAEHITAJI NDOA NAMSHIRIKISHA KATIKA BIASHARA YOYOTE ILE AU KUKAA KATIKA OFIC ZANGU
Naombeni ushauri ndugu Zangu Nyumba nimemuachia akae na hataki, nalipa kodi niliko panga huku Nyumba YANGU ipo na haikaliwi na mtu. NIFANYEJE?
 
Hapo ni sawa na mmeachana,so anataka mgawane kila kitu we uanze upya na mkeo,nae aanze upya..m'baki mnalea watoto tu.Ila bado kuna option ya ndoa ya kiserikali..Angalieni hao watoto.Fanya hivyo
Mara kadhaa nimekuwa nikileta mada ya kuhusu mama watoto wangu ambae ni Islamic na wazazi wake wamekataa mtoto wao asibadili dini ili tuweza kuwa mume na mke mbele ya MUNGU kwa sababu Mimi ni Christian.
Ukweli ni kwamba tumetoka mbali sana kimaisha toka tulipokuwa tumepanga mpaka kujenga na Maendeleo mengine ya kibiashara.
Nimejaribu kuvumilia sana nikijua huenda atabadili mawazo na kuamua kwenda kinyume na wazazi ili kunifata Mimi ili tuweze kuoana lakini mwenzangu anasikiliza maamuzi ya wazazi.
Kiukweli sasa imefikia stage naona kama tunapotezeana muda tu. Nikajiuliza maswali mengi sana mpaka nikaamua sasa kutafuta mkristo mwenzangu ili niweze fanya mipango ya ndoa. Ila kwa kuwa tayari nimezaa nae nikaona sio mbaya nimuache kwenye nyumba tuliyojenga akae na watoto kisha mi nikapambana kujenga nyingine ambayo nitaishi na huyo nitakae muoa.
Kikubwa kilichofanya niombe mawazo ya ndugu Zangu humu tatizo ni hili hapa:
1..YUPO KWAO NA HATAKI KURUDI KWAKE
2..ANATAKA NIMUHUDUMIA AKIWA HUKO HUKO
3..HATAKI KUONA HUYU ANAEHITAJI NDOA NAMSHIRIKISHA KATIKA BIASHARA YOYOTE ILE AU KUKAA KATIKA OFIC ZANGU
Naombeni ushauri ndugu Zangu Nyumba nimemuachia akae na hataki, nalipa kodi niliko panga huku Nyumba YANGU ipo na haikaliwi na mtu. NIFANYEJE?
 
Pole sana! Ila ulishaharibu toka mwanzo....

Huwa nachukia mtu kuwa na uhusiano wa jumla mtu ambaye si dini yake....
Ona sasa sasa hivi unalia lia,ina maana hujui kama hayo mambo huwa yanatokea huko mbele?
 
Duh hapo ndio mlishaachana hivyo mkuu. Ila niunge hoja ya member mmoja hapo juu 'hiyo nyumba ipangishe nandio iwe pesa yake yamatumizi' au ndio iwe pesa yawewe kulipia pango huko ulipopanga huku ukiendelea kumuhudumia.

Yawezekana anaogopa kuishi kwenye hiyo nyumba yawezekana asiwe huru kuingiza mwanaume anahisi bado atakuwa katika himaya yako so hatokuwa huru
 
pole mkuu bt tatzo ulijua toka mwanzo hili jambo sa ungepaswa kufunga ndoa ya kiserikali kila mtu abaki na din yake coz din ni njia2 ya kumtumikia mungu hvo njia zote zpo sawa ukiachana na propaganda zinazopigwa na na viongoz wadin zetu kua dini fulan ndo sahh
 
unampenda? ndoa ni mapenzi na mahaba sio dini.....mmeshazaa, hiki unachofanya sio salama... huyu unaetaka kumuoa amekubali coz ana sbb zake....yule kaondoka kenda kwao sbb haamini unakifanya......tafaraki jinsi penzi lenu lilivyochipua likamea vyema, leo maacha shina linakauka sbb ya ubinafsi wenu....fungeni hata ya serikali......be man....real man.
 
Back
Top Bottom