Nakerwa na tabia ya wakata tiketi wa Mabasi ya Mwendokasi kudai hawana chenji kila siku

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Nimeona Rais Samia kamtumbua kiongozi wa juu wa Mwendokasi labda kero zitapungua kwa kweli.

Ukiachana na kero ya msongamano wa abiria na utaratibu mbovu ambao kila siku hata Jamii Forums naona mnaupigia kelele, kingine ni kuhusu suala la chenji.

Hilij ambo ni dogo lakini linakera na linapaswa kupigiwa kelele, kila kituo ukienda unaambiwa hawana chenji, hata wakati mwingine ukitoa Shilingi 2,000 au hata buku utaambiwa hakuna chenji ili jambo linakera sana tena sana.

Najua Usafiri wa Mwendokasi unaendeshwa na Kampuni kubwa na yenye uzoefu, inakuwaje kila Kituo kuna changamoto ya chenji?

Mbona zamani hakukuwa na hizi mambo, nakumbuka kila kituo kilikuwa kinapewa coins nyingii kwa ajili ya kutoa chenji kwa wateja wao.

Abiria wengi wanaacha 50, 50 zao 100, 100 zao nyingi tu kwa kuwa wanakwambia hakuna chenji so kama vipi kaa hapo pembeni usubiri ipatikane, muda unaenda, mambo ya ajabu kabis hayo.
 
Uwa nasubiria, akija abiria mwingine namwambia lipia nusu chenji yangu imebaki.

1. Akiiba tsh 100 chenji kwa watu 100 iyo ni 10,000/=

2. Wana tiketi zao wameziprint ambazo ofisi haizijui. Kwa siku akiwa nazo 100 akiuza kwa naulinya 700 iyo ni 70,000/=

Kwahiyo mtu anapata 100k uku amekaa na bado posho na mshahara.

DART Mwendokasi
 
Leo nimeona mwakilishi kutoka BoT katika kipindi cha kumekucha ITV kuhusu kuhamasisha wananchi kupekeka fedha hizo za sarafu katka matawi ya bank inchi wapewe fedha za karatasi
Dhumuni bank wazirejeshe katika mzunguko ktk sehemu zenye uhitaji mkubwa pia wajue idadi yake ili kuepuka gharama za kuziagiza

Wamesema wananchi wamekuwa wakiweka ndani tu bila matumizi pia wanaocheza KOROKOKO wamekuwa wakitumia shilingi 200 kama kifaa Cha kuchezea HIVYO KUPEKEKA SARAFU HIZO KUWAADIMU

Inanikera pale napo nunua bia au soda naambiwa "chench" hakuna na baa hakuna Pipi hata umalize nao😂😂😂 fegi situmii
 
Mara kibao nakuta folen nikifikiria pale tapoteza muda kuhusu chenchi, huwa natoa buku nawaachia tu iyo 250 maana najua chenchi zipo ila ujanja ujanja n uhuni na sina namna.

Kinachokera sana ni msongmano na gari hamna
 
109,200 hela ndogo sana hii akipata
Nyie ndio watu wapumbavu ambao taifa linaingiza hasara kupitia watu mwenye akili kama zako.. hiyo 100k in per day je month ni kiasi gani.. unajua mtu akiomba rushwa ya 100k akashtakiwa Huwa adhabu yake ni ipi kwa mujibu wa sheria.. unazania mtu kama huyo anaechukua 150 kwa kichwa angepewa wizara kama ya nishati alafu akaongeza 150 kwenye mafuta hiyo iwe inaenda mfukoni kwake au wizara za habari Sanaa na mawasiliano kaongeza 150 kwenye mihamala ungejisikia vipi.. nyinyi mnaotetea huo upuuzi ndio mnazalisha kizazi cha zakayo.. vijana kama nyie taifa halipaswi kuwategemea sababu tofauti yenu na mbuzi ni position ya madako..
 
Back
Top Bottom