Nakaribia kudhulumiwa, naombeni ushauri

Nadhani j3 ingekuwa bora zaidi
Sawa mkuu.

Nitajaribu jmosi kwasababu nitakuwa mitaa ile kwa shughuli nyingine, ikishindikana basi nitarudi tena j3 kwasababu bado nitakuwepo Dsm.
 
Nenda kachukue dawa kwa mganga ukija iweka ukafagia na ufagio wakat anatoka hatarudi Tena atasahau Hadi vitu vyake humor ndani
 
Ahaaaa!! Mkuu hilo suala nalo ni la kulia lia?!! Achana na mambo ya jeshi kwenye jambo hili wala halihusiani kabisa!! Huyo ni raia kama raia mwingine,.
 
MREJESHO:

Kama wengi mlivyoshauri, jana nilifika Ngome-Upanga majira ya saa 9 alasiri. Nikapokelewa na na maafande pale getini nikaulizwa shida yangu, nikajieleza kwa ufupi, kabla ya kukaribishwa ndani nikapewa kiti kwanza nikae palepale getini na kupewa pole!

Afande mmoja muungwana sana ambaye alionekana ndio kiongozi wa walinzi wa siku ya jana pale getini, akaniomba nionyeshe nyaraka zozote (kama ninazo) kuthibitisha namdai. Nikatoa mkataba na commitment aliyoifanya Kwa maandishi nilipokutana nae mara ya mwisho Desemba mwaka Jana na kuahidi kunilipa ifikapo tar 29/01/2024.

Kwanza maafande wakanishangaa kwanini nimemruhusu akae muda wote huo bila kumbananisha alipe au nimfukuze.

Wakaniuliza kama nina picha yake nikawaonyesha picha yake aliyoweka Whatsapp. Baadhi ya maafande wakamtambua.

Wakaniomba sana kwamba nisipeleke hili swala ndani, watakachofanya ni kwamba watawasiliana nae ili j3 aje alipe au kama hana pesa achukue mkopo anilipe j3 hiyohiyo.

Kwahiyo wakaniomba nifike Ngome j3 kabla ya saa sita mchana. Nitamkuta mdeni wangu. Nikachukua namba ya yule afande in charge nikasepa zangu.

Wakuu, leo asubuhi wakati naamka nimekuta msg za mdeni wangu akinibembeleza kwamba j3 tukutane pale Ngome nje anilipe pesa yangu yote [emoji28][emoji28]. Nadhani wale maafande wenzake wameshampigia.

Ndugu zangu, nawashukuru sana kwa ushauri. JF forever! Nimepanga akishanilipa tu j3 namlamba na notice ya mwezi mmoja ahame.

ASANTENI SANA NA MUNGU AWABARIKI.
 
Halafu nafkiri kuna shida ya viongozi au sisi watu tunaofanya kazi huku chini chini. Hapo Ngome ukifika wanakupokea vizuri kuliko makambini. Sehemu ya majeshi wanayokupokea kwa changamoto zaidi ni pale Makumbusho
 
Nyie wanajeshi wa karne hii ni matapeli mbayaaa 😂😂🤣🤣 sijui wanakwama wapiii.
Halafu ni wababe vibaya mno heri huyo unamdai hela nyingi.... kuna huyu jamaa alikopa vitu dukani vya elfu 40,000 tu lakini ni miezi inakatika
 
Halafu nafkiri kuna shida ya viongozi au sisi watu tunaofanya kazi huku chini chini. Hapo Ngome ukifika wanakupokea vizuri kuliko makambini. Sehemu ya majeshi wanayokupokea kwa changamoto zaidi ni pale Makumbusho
Ni kweli mkuu. Sijui huku chini kuna shida gani yani [emoji28]. Watu wamejaa viburi sana.
 
Ajabu sana mkuu! Dawa yao ni kwenda kuwaripoti tu. Wakati mwingine shida inakuwa sio pesa ila kuwafundisha uungwana na kuepusha madhara kwa watu wengine.
 
We una moyo mlainiiii 👀
Mimi ningeenda kumreport ndani tu akapate na adhabu huko kambini😂
 
Kumbe inawezekana eeh? Nitaenda na mimi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…