Nakala ya SMS.

Mkuu,
Mtu aliyefanyiwa hilo hana uwezo wa kumiliki simu ya zaidi ya 100K, sanasana ni Techno ya kawaida ambayo hata si smart-phone.
Lkn to her surprise alifowadiwa sms zote alizotumiwa na mtu mwingine, ambapo hao wawili hata hawajuani(actually ni competitors). Na hali hii imemfanya huyu dada aingie matatizoni kwa habari ya mahusiano.

Mkuu nadhani huyo aliyemfanyia aliinvolve mtu anayefanya kwenye kampuni ya simu. Mimi nakumbuka mwaka 2010 niliwahi fanyiwa huo mchezo na demu flani alikuwa anasoma st.john nilikuwa natoka naye. Mimi bila kuwa na taarifa kumbe alikuwa ana track calls, sms, na kila nachofanya ikiwemo emails na kusurf yani alikuwa na passwords zangu zote. Yani lolote nitakalofanya as long as natumia line yangu aliyo track lazima apate copy.
Mwisho wa siku nilikuja umbuka vibaya siku aliponionyesha sms, nilizokuwa natumiana na demu mwingine na hapo ndipo tulipopigana chini lakini baadae sana alikuja kuniambia alikuwa anatumia mtu wa ndani wa hiyo kampuni ya simu.
Nadhani ndicho huyo dada atakuwa kafanyiwa.
 
Wakuu,
Kuna dada ananiambia kuwa mchumba wake alimwomba simu, akaifanyia kitu/utundu fulani, matokeo yake huyo jamaa amekuwa anapata nakala ya msg zote zinazotumwa kwa huyu dada.

Ninachotaka kujua je hiyo kitu inawezekana kwel? Kama kweli inawezekana mbona ni hatari sana kwa mahusiano?

Naombeni usaidizi kwa hili.
The truth shall set you free. Can you handle the truth?
 
mkuu anatumia simu gan ungetoa details hizo tungeanzia hapo

Waz thinking the same....!!!!pia hata nokia yenye tochi unaweza fanya hayo kweli???plz...!!!!tuelezeni ni simu gani zenye uwezo huo....!!!!!!come to think of it hapa ni kuwa na uelewa wa hizo software maana unaweza ukategeka kwa zawadi ya simu kumbe ishafanyiwa mambo...lol!!!kazi kwelikweli!!!!
 
hebu niulize kwnz kbl sjaidownload, kwhy nivoidownload malipo nafanya vp? na hakuna hata trial nikatumia hata mwez mmoja, kwann msitupe za free na zinazochungulia hata sms na calz tu.
 
Kama unamtafutia kisa cha kumuacha mkeo muingizie hiyo program ila kama bado unamuhitaji achana nayo.

duuuuuh, inaonekana hali za kwenye ndoa sio nzuri kabisa, mana kila mtu ana wasiwasi na mwenzie, naona kila mtu naogopa kufanya hivyo kwa sababu anaogopa mapresha ya kujitakia, ina mana hakuna uaminifu? mnanitisha kweli kwa kweli
 
Mkuu naiomba hii? Inapatikana madukani mwetu hii? Nataka tu nifunge kwa simu ya mamsapu ili ajua mimi niko clean!!! Ha ha ha!!

Angalia tu isije kukulazimu kutafuta line ya pili iwekwe kwenye nokia ya tochi.
 
Back
Top Bottom