The Green Village
Senior Member
- Aug 30, 2013
- 170
- 73
wapi imeandikwa kuwa kila mwenye elimu ni lazima aajiriwe?Habari zenu ndugu,
Ni kipindi kirefu nimekua nikiangaika kutafuta ajira pasipo mafanikio.Nimefanya interview zakutosha lakini nimekua nikiambulia ahadi tu za kupigiwa simu toka kwa ma hr ambazo hazina ukweli wowote.Kitu kikubwa kinachotukosesha ajira sisi vijana ni kipengere cha experience ambapo waajiri wengi wanahitaji uzoefu usiopungua miaka mitatu na kuendelea.Swali ni je nawezaje kupata huo uzoefu wakati ofisi nyingi hazitaki kuniajiri na hata ninapoomba kujitolea naambiwa nafasi hakuna ?kwa kifupi ndugu zangu nimekata tamaa kabisa kama siku moja nitakuja ajiriwa na najutia miaka mitatu niliyoipoteza chuoni pamoja na ada niliyoitumia kwani laiti ningejua ni bora ile ada ningeitumia kwenye kujiajiri kuliko kupote pesa na muda wangu.
Yani hapa nasubiri miujiza ya mwenyezi Mungu tu kwakweli.
Eeeh Mungu tuangalie waja wako,tuko kwenye kipindi kigumu sana.
btw, lengo kuu la elimu ni kuondoa ujinga na kuongeza maarifa kichwani!
maarifa hayo ndio yatakufanya uweze kupambana na mazingira katika hali yoyote ile, ikiwemo hii ya ukosefu wa ajira..
mkuu, kama wewe wa higher learning unalia, je mwenzio uliyemwacha nyuma kwa kufeli kidato cha nne ama la 7, atakuwa na hali gani sasa?
tafadhali tumia elimu yako kuongeza tabasamu usoni mwako.. sio huzuni..