Najuta kuoa mwanamke mlokole

Najuta kuoa mwanamke mlokole

NILISHA APA.... KAMWE SIWEZI KUOA MLOKOLE KWENYE MAISHA YANGU...

hata mamangu mzazi ameni kataza hilo...


Labda, narudia tena labda " Abadili dini aje Roman Catholic " Mbali na hapo tupa kule.

Sifa zao hawa:

1. Wana jeuri hawa.
2. Wana hofu ya mchungaji wa kanisa kuliko mume wake, yani ana muheshimu mchungaji kuliko mme wake... Na hapa ndio ntapiga mtu mpaka nitoe taya.
3. Hawa jui malezi ya mama kwa mtoto.
4. Hawana akili za maendeleo, wana waza kufunga naku sali mwanzo wa mwaka mpaka mwsho.


Nili wai kua na girlfriend mlokole... Bora tuli achana aisee... Headache tupu.
Vipi ulimgegeda?
 
Ndugu shukuru Mungu kwa kukupa mke anayetafuta yaliyo ya Mungu maana maandiko yanasema mke aweza kumwokoa mumewe na mume aweza kumwokoa mkewe maana kwa Mungu mnahesabika kuwa mwili mmoja uliounganishwa na kristo. Je angekuwa anaenda disco kulewe umalaya kipe kiko sahihi nawe unaonekana una shida badilisha njia zako kama sio sahihi.
 
Miezi miwili iliyopita nilipelekwa polisi na wazazi wa mke wangu, kwa kosa la kumpiga binti yao karibu nimuue, ndugu walikuja kunitoa

Iko hivi;
Huyu binti nilimuoa miaka miwili iliyopita na tuna mtoto mmoja, yeye na wazazi wake wote wameokoka, Hivi sasa naweza kusema kwamba mke wangu ameolewa na kanisa na si mimi.

Akitoka kazini saa kumi na moja jioni anakwenda kwenye maombi kanisani hadi saa tatu , na hii ratiba ni kila siku Monday to Friday, Jumamosi pia wanakwenda Jumapili ni kutwa nzima, wakati mwingine kuna mkesha katikati ya wiki, hali hii, imefanya ashindwe hata kupataa muda wa kumlea mtoto wetu wa mwaka alielazimika kumwachisha ziwa akiwa na miezi mitatu kutokana kubanwa na mambo ya kanisa.

Mtoto huyu ni kama amebadilishiwa mama, maana sasa analelewa na house girl wetu kwa hali na Mali
Ilifika pahala nikashindwa kuvumilia hali hii na nikamuita na kumueleza hali halisi na kumtaka abadilishe ratiba zake, akadai kwamba hana jinsi kwa kua ratiba ya kanisa kwake haina substitute , nikamwambia ni amri sio ombi

Akaendelea hivyo hivyo, kwa Mara ya kwanza nilimpa kipigo kwa kukaidi amri yangu, niliendelea kumpiga mara kwa Mara sababu ikiwa ni kanisa, kila tunapoitwa kusuluhishwa wazazi wake humtetea na kudai walikosea kunipa mm binti yao, ikawa tunagombana na wazazi wake vikaoni hadi nikaamua kuachana na vikao.

Mwanzoni mwa mwezi wa sita alidai kuna mkesha wa maombi siku hiyo na hivyo atalala huko, nikamwambia ukitoka huko utafute nyumba nyingine, baadae mama yake akanipigia kwamba kuna mkesha hivyo wote watalala church kwenye mkesha, nikamjibu haiwezekani wamruhusu wife arudi kwa kuwa ana mtoto mdogo, akakata simu

Kweli, wife hakurudi, ila kila saa alikua akinipigia simu karibu usiku kucha nami sikua napokea naiangalia tu hadi inakatika hadi saa kumi alfajiri, alikuja amesindikizwa na dada yake maana walijua nimekasirika sana

Walipofika tu niliwakamata wote wawili na kuwapa kipigo kizito sana hadi wife kuzirai, dada mtu aliniponyoka na kukimbilia main road huku nikiwa nimemtengua mbavu akapanda boda boda, saa moja wazazi wa wife wakaja nilikua nimemfungia stoo wakamchukua wakaenda nae.

Baadae wakanifuata kazini na polisi wakaniweka ndani kwa shambulio la kudhuru mwili, nilitoka kesho yake , kesi ikahamia Ustawi wa Jamii tuliitwa pale, mbele ya wazee wa pande zote, ikaamriwa kwamba binti arudi kwa wazazi wake hadi hapo baadae hali ikiwa nzuri, ila wazazi wake wakasema wanamchukua kimoja hawanihitaji tena, kwamba nisubiri taratibu za talaka, nikasema haina shida nipo tayari, tukaja nyumbani wakamchukua mtoto na hg na nguo zake wakarudi kwao

Nimeyasahau hayo naishi kwa auheni kiasi kwa sasa Ingawa bado nina msongo, surprisingly Friday wife akanifuata kazini hatukua tumeonana for two months, roho yangu iliingia kitu flani hata mtoto wangu sikutaka hata kuwa naenda kumuona ingawa pale ustawi wa jamii niliruhusiwa

Wife akaniomba tuongee, akasema anahitaji turudiane, akadai anaomba arudi home kwangu hata kesho yake ikiwezekana, kwamba ananipenda, kwamba tutarekebisha tu, nikamwambia haiwezekani simtaki tena

Wadau wana Jf, nimemwambia atafute Mme mwingine kanisani kwao ndo watawezana na sio Mimi, mke wa hivi hanifai, hata mshahara wote anapeleka huko, hilo kanisa Jumapili moja tu kuna sadaka kama 12 hivi tangu asubuhi hadi jioni, unaweza kwenda na laki mbili usirudi hata na shilingi jioni, bado katikati ya wiki, halafu wachungaji wanaishi kifajari.

Huyo mchungaji wa hilo kanisa ameshawateka akili, mimi binafsi nilikua huko nikahama kutokana na hiyo biashara ya kutakiwa kushinda huko 24/7 na pia kutumia sehemu kubwa ya mapato yangu kanisani badala ya kujenga familia, kanisa gani wanaomba hadi salary slip? Na usipowapa watakusema sana kwamba umepotea njia na kadhalika
Kanisa gani halijali ndoa za watu?

Sio kwamba sipendi mke wangu aende kanisani, aende kwa kiasi na ratiba akizingatia kuwa yeye ni mama wa familia, inapaswa kwenda kanisani unashiriki na wenzako mchana au jioni unarudi home, jumatano unakwenda kwa maombi masaa mawili, six jioni unarudi kwako, there will be nothing wrong, lakini huwezi kwenda kushinda huko 24/7. Seven days a week, inakuja kweli hiyo?

Hata dada wa mke wangu niliempiga, mumewe pia alikuja kwangu na malalamiko kama haya ya kwangu, nimeamua simtaki tena, kwanza akili yangu imeshachanganyikiwa,
Nonsense

Ni bora nirudi kwa Rachel, alinivumilia tangu chuo hadi mtaani nikamtendea vibaya nikaoa mlokole nisiemjua, kwa kweli najuta sikujua nachofanya.
Vumilia tu ndg ndoa hizi za sasa ni pasua kichwa, kwa upande wa wenzetu walokole sijui mafundisho yao yakoje kwani hata mimi yalinikuta hayo ya mwanamke mchana kutwa na usiku kucha hapungui kanisani huku pato la familia likiteketea. Kingine hawa wanawake waliokoka walio wengi si watii kwa ndoa zao isipokuwa mchungaji wao na kanisa lao.
 
Stori ya kutunga. Ninachojua mimi makanisa ya kilokole yanakua na mkesha mara moja kwa wiki, au mara moja kwa mwezi. Hakuna mkesha kila siku. Hiyo ni chuki yako binafsi dhidi ya walokole.
Story ina viashiria vya kuwa ya kutungwa kutokana na conclusion yake. Ila kati ya haya 100% aliyoyasimulia about 65 % ni yakweli kabisa.

Nayashuhudia baada ya kuyaona kwa macho yangu. yaani kuna mama yangu mlezi wa mke wangu kaolewa na kibosile mkubwa kabisa na mama ana kazi yake nzuri sana serikalini. ila huwezi amini huyu mama katekwa na mchungaji mmoja hapa dar. mama muda wake wote ni 50% Kazini 45% kanisani 5% kwa majukumu ya familia. huwezi amini weekend zote yupo church mpaka anarudi saa 7 usiku kwa mmewe ambaye alijitoa huko kanisani kisa upuuzi huo. akiulizwa ulikuwa wapi na mmewe anajibu tulikua tunahesabu sadaka. yaani ni watu wameoana wana elimu nzuri umri mkubwa mpaka wanawajukuu lakini huwezi amini namna wanavyoishi.

Mchungaji anatoa vyeo kwa watu wenye vipato vizuri na kazi nzuri kama vile wafanyakazi wa Tra na taasisi zingine. anawaagiza wamletee mpaka hati za nyumba zao sijui anataka kuzifanyia nini?

Mimi mke wangu mlokole ila mziki wangu anaujua hawezi kuthubutu na mwisho kuingia kwenye kibanda changu nilichokijenga kwa jasho langu ni saa 12 ikizidi na nusu jioni. alijaribu kuja saa moja na nusu akakuta milango imefungwa serious kosa nililofanya sikuwajulisha watoto kama mama kapigwa ban. nilipoingia bafuni kuoga nikakuta wamemfungulia geti. ila toka siku hiyo sijaona tena hizo sanaa.

Ukiamua chagua kuolewa na mume au kanisa huwezi kutaka vyote viwili at a go.
 
Moja ya watu ambao nilishasema sitaoa ni walokole.Infact wengi wao wana back history chafu sana yenye kinyaa ambayo inakifu wanakimbilia kanisani kuficha maovu yao.Yuko mmoja namjua alitoa mimba sana ujana wake kuja kuolewa hapati mtoto hadi leo
 
Kuoa au kuolewa na walokole ni kero.
1.Vikao vingi vya kanisa
2.Mara nyingi wapo kanisani.
3.Muda wa familia hakuna
4.Ukimgusia kuhusu hili anadai ni unataka yeye akiuke maamuz ya kanisa lao.
Maana wanaprograms kibao kila saa .
Halafu mpenzi au mume mke wao nibahati kujulikana kwa huyo muhusika.
So kama si mlokole usioe mlokole .
Walokole lazima waolewe na walokole wenzao watawezana.
Mtu wakawaida oa mtu wakawaida.
So jipange tena upya.
 
achene kulaumu watumishi wa Mungu wakati hata hamjui ukweli wa makanisa na kazi inayofanyika huko. wengi makanisa yenu ni JF, facebook nk. jamaa kasema yeye tu lakini hatujamsia mke wake na mnaanza kuhukumu makanisa kuwa yanaharibu watu. pia kanisani kuna sera ambayo sio rasmi. oeni wa kwenu maana mnajuana vizuri. wewe ukiwa mlokole ukaoa mkarismatic lazima kuna mambo mpishane hasa hisia zinapoanza kukata na kuanza kujitambua kama umeharisha njea ya shimo la choona maji yamekatika. ndoa sio dharura na wala sio kitu cha kukimbilia kama hujakuwa na uhakika
Mama zetu, na bibi zetu wote walishika dini.. Ila hawakushinda kanisani. Dini in vile unavyoishi na watu wanaokuzunguka.. Mshika dini hapimwi kwa kushinda kanisani.. Huo ni unafiki.

Familia ilalamike ..na wewe mchungaji unafurahia watu wanalala kanisani?! Kweli.?! Hiyo sio sawa hata kidogo. Mwanamke anapaswa kumheshimu mumewe na hiyo ni amri..
 
Story inaviashiria vya kuwa ya kutungwa kutokana na conclusion yake. ila kati ya haya 100% aliyoyasimulia about 65 % ni yakweli kabisa.

nayashuhudia baada ya kuyaona kwa macho yangu. yaani kuna mama yangu mlezi wa mke wangu kaolewa na kibosile mkubwa kabisa na mama ana kazi yake nzuri sana serikalini. ila huwezi amini huyu mama katekwa na mchungaji mmoja hapa dar. mama muda wake wote ni 50% Kazini 45% kanisani 5% kwa majukumu ya familia. huwezi amini weekend zote yupo church mpaka anarudi saa 7 usiku kwa mmewe ambaye alijitoa huko kanisani kisa upuuzi huo. akiulizwa ulikuwa wapi na mmewe anajibu tulikua tunahesabu sadaka. yaani ni watu wameoana wana elimu nzuri umri mkubwa mpaka wanawajukuu lakini huwezi amini namna wanavyoishi.

Mchungaji anatoa vyeo kwa watu wenye vipato vizuri na kazi nzuri kama vile wafanyakazi wa Tra na taasisi zingine. anawaagiza wamletee mpaka hati za nyumba zao sijui anataka kuzifanyia nini?

Mimi mke wangu mlokole ila mziki wangu anaujua hawezi kuthubutu na mwisho kuingia kwenye kibanda changu nilichokijenga kwa jasho langu ni saa 12 ikizidi na nusu jioni. alijaribu kuja saa moja na nusu akakuta milango imefungwa serious kosa nililofanya sikuwajulisha watoto kama mama kapigwa ban. nilipoingia bafuni kuoga nikakuta wamemfungulia geti. ila toka siku hiyo sijaona tena hizo sanaa.

Ukiamua chagua kuolewa na mume au kanisa huwezi kutaka vyote viwili at a go.

Na wewe umeweka chumvi. Kuhesabu sadaka hadi saa 7n usiku? Sadaka inakua milioni ngapi? Hata kama kumekua na kikao, pengine cha Baraza la Kanisa ambavyo vinaweza kuchukua hadi masaa 4, tena mwa mwezi mara moja, haiwezekanai mama arudi saa 7. HUU NI UONGO ULIOPITILIZA.

Lakini haiyumkini huyo mama unayemsema akawa na wajibu Kanisani, ambao pengine unamfanya achelewe kurudi nyumbani. SWALI NI KUWA KILA SIKU KUNA IBADA? Sio kweli. Makanisa mengi yana ibada Jumatano saa 10 au 10.30 - 12.00, ijumaa muda huo huo, na Jumapili saa 3 au 4 mpaka saa 7 mchana. Sasa huko kurudi nyumbani saa 7 usiku kumetoka wapi?

JAMANI ONDOENI PICHA MBAYA KUHUSU WALOKOLE KUWA WANAKESHA KANISANI. Jaribu kwenda siku moja moja uone hali halisi.
 
Na wewe umeweka chumvi. Kuhesabu sadaka hadi saa 7n usiku? Sadaka inakua milioni ngapi? Hata kama kumekua na kikao, pengine cha Baraza la Kanisa ambavyo vinaweza kuchukua hadi masaa 4, tena mwa mwezi mara moja, haiwezekanai mama arudi saa 7. HUU NI UONGO ULIOPITILIZA.

Lakini haiyumkini huyo mama unayemsema akawa na wajibu Kanisani, ambao pengine unamfanya achelewe kurudi nyumbani. SWALI NI KUWA KILA SIKU KUNA IBADA? Sio kweli. Makanisa mengi yana ibada Jumatano saa 10 au 10.30 - 12.00, ijumaa muda huo huo, na Jumapili saa 3 au 4 mpaka saa 7 mchana. Sasa huko kurudi nyumbani saa 7 usiku kumetoka wapi?

JAMANI ONDOENI PICHA MBAYA KUHUSU WALOKOLE KUWA WANAKESHA KANISANI. Jaribu kwenda siku moja moja uone hali halisi.
Nguruwe na kondoo hawawezi kukaa zizi moja.
 
Mkuu pole kwa masahibu.
Ningependa nishauri ila kabla sijafanya hivyo, nataka kujaua anaabudu Kanisa gani na wapi? Ni TAG, EAGT, KKKT,..n.k na kanisa lake ni wapi e.g Kariakoo, Mbagala,...?
Ndugu yangu, toa ushauri wako kumsaidia kuweka sawa familia yake, hayo mambo uko kanisa gani, sehemu gani haina maana. Kikubwa ni USHAURI wako hidden ID's
 
achene kulaumu watumishi wa Mungu wakati hata hamjui ukweli wa makanisa na kazi inayofanyika huko. wengi makanisa yenu ni JF, facebook nk. jamaa kasema yeye tu lakini hatujamsia mke wake na mnaanza kuhukumu makanisa kuwa yanaharibu watu. pia kanisani kuna sera ambayo sio rasmi. oeni wa kwenu maana mnajuana vizuri. wewe ukiwa mlokole ukaoa mkarismatic lazima kuna mambo mpishane hasa hisia zinapoanza kukata na kuanza kujitambua kama umeharisha njea ya shimo la choona maji yamekatika. ndoa sio dharura na wala sio kitu cha kukimbilia kama hujakuwa na uhakika
Naona mchungaji povu
 
Hilo swala ni gumu kiasi ila linaweza kusuluhishika bila ya kuachana......

Kwanza,kaa chini tafakari kwa kina jinsi ulivyotoka mbali na mkeo huyo ambae ni zawadi kutoka kwa mungu paka kufikia hatua hiyo....

Pili hata siku moja usije kulaumu kwa mwenyezi mungu eti umeoa mke mlokole ni kosa kubwa, usirudie tena

Kaa chini jipange kuwa na mazungumzo ya familia ya pande mbili wazaz wa mkeo na wazaziwako, pia viongoz wa din wa upande wa mkeo mtafakari kwa kina juu ya swala husika...nadhani mnaweza kufikia suluhisho ambalo litasaidia....

Pia wewe mwenyewe kaa chini ongea na mke wako kwa upole, USIRUDIE KUMPIGA MKE WAKO, HILO NI KOSA KUBWA KULIKO ALILOANYA MKEO..

Cha muhimu tafakar zaidi njia ya kutatua bila ya kuwaza kuvunja ndoa......
Huyo hajaoa mke mlokole ila ameoa mke kiburi
 
Ndugu yangu, toa ushaur wako kumsaidia kuweka sawa familia yake, hayo mambo uko kanisa gan, sehemu gan haina maana. Kikubwa ni USHAURI wako hidden ID's
Nikijua yuko wapi, nitamshauri ni mtumishi gani wa Mungu akamuone, alieye karibu na sehemu aliyoko. Hata hivyo, watumishi wafuatao nina ukhakika wanaweza kumsaidia: Mwalimui Mwakasege; Mchungaji Mosses Maghembe-TAG Ukonga/ Makao Makuu; Mchungaji Ernest Mayala,TAG Tabata Kisukulu. Kwa kuanzia anaweza kuwaona hao, ila wapo wengi, list ni ndefu
 
Mimi mlokole lakini ulokole wa hivi sijawahi uona, labda kwa sababu makanisa ni tofauti,kanisani yanaenda mara 2 kwa wiki tena Kuanzia saa 9-11, mikesha mara chache tu, Mwanamke asiyemtii mumewe katika mambo ya msingi hafai maana kumtii mume ni amri na sio ombi
 
Lakini huyu mtoa mada atupe mrejesho maana imekuwa siku mingi tangu 2015
 
Back
Top Bottom