Najuta kuoa mwanamke mlokole

Najuta kuoa mwanamke mlokole

Miezi miwili iliyopita nilipelekwa polisi na wazazi wa mke wangu, kwa kosa la kumpiga binti yao karibu nimuue, ndugu walikuja kunitoa

Iko hivi;
Huyu binti nilimuoa miaka miwili iliyopita na tuna mtoto mmoja, yeye na wazazi wake wote wameokoka, Hivi sasa naweza kusema kwamba mke wangu ameolewa na kanisa na si mimi.

Akitoka kazini saa kumi na moja jioni anakwenda kwenye maombi kanisani hadi saa tatu , na hii ratiba ni kila siku Monday to Friday, Jumamosi pia wanakwenda Jumapili ni kutwa nzima, wakati mwingine kuna mkesha katikati ya wiki, hali hii, imefanya ashindwe hata kupataa muda wa kumlea mtoto wetu wa mwaka alielazimika kumwachisha ziwa akiwa na miezi mitatu kutokana kubanwa na mambo ya kanisa.

Mtoto huyu ni kama amebadilishiwa mama, maana sasa analelewa na house girl wetu kwa hali na Mali
Ilifika pahala nikashindwa kuvumilia hali hii na nikamuita na kumueleza hali halisi na kumtaka abadilishe ratiba zake, akadai kwamba hana jinsi kwa kua ratiba ya kanisa kwake haina substitute , nikamwambia ni amri sio ombi

Akaendelea hivyo hivyo, kwa Mara ya kwanza nilimpa kipigo kwa kukaidi amri yangu, niliendelea kumpiga mara kwa Mara sababu ikiwa ni kanisa, kila tunapoitwa kusuluhishwa wazazi wake humtetea na kudai walikosea kunipa mm binti yao, ikawa tunagombana na wazazi wake vikaoni hadi nikaamua kuachana na vikao.

Mwanzoni mwa mwezi wa sita alidai kuna mkesha wa maombi siku hiyo na hivyo atalala huko, nikamwambia ukitoka huko utafute nyumba nyingine, baadae mama yake akanipigia kwamba kuna mkesha hivyo wote watalala church kwenye mkesha, nikamjibu haiwezekani wamruhusu wife arudi kwa kuwa ana mtoto mdogo, akakata simu

Kweli, wife hakurudi, ila kila saa alikua akinipigia simu karibu usiku kucha nami sikua napokea naiangalia tu hadi inakatika hadi saa kumi alfajiri, alikuja amesindikizwa na dada yake maana walijua nimekasirika sana

Walipofika tu niliwakamata wote wawili na kuwapa kipigo kizito sana hadi wife kuzirai, dada mtu aliniponyoka na kukimbilia main road huku nikiwa nimemtengua mbavu akapanda boda boda, saa moja wazazi wa wife wakaja nilikua nimemfungia stoo wakamchukua wakaenda nae.

Baadae wakanifuata kazini na polisi wakaniweka ndani kwa shambulio la kudhuru mwili, nilitoka kesho yake , kesi ikahamia Ustawi wa Jamii tuliitwa pale, mbele ya wazee wa pande zote, ikaamriwa kwamba binti arudi kwa wazazi wake hadi hapo baadae hali ikiwa nzuri, ila wazazi wake wakasema wanamchukua kimoja hawanihitaji tena, kwamba nisubiri taratibu za talaka, nikasema haina shida nipo tayari, tukaja nyumbani wakamchukua mtoto na hg na nguo zake wakarudi kwao

Nimeyasahau hayo naishi kwa auheni kiasi kwa sasa Ingawa bado nina msongo, surprisingly Friday wife akanifuata kazini hatukua tumeonana for two months, roho yangu iliingia kitu flani hata mtoto wangu sikutaka hata kuwa naenda kumuona ingawa pale ustawi wa jamii niliruhusiwa

Wife akaniomba tuongee, akasema anahitaji turudiane, akadai anaomba arudi home kwangu hata kesho yake ikiwezekana, kwamba ananipenda, kwamba tutarekebisha tu, nikamwambia haiwezekani simtaki tena

Wadau wana Jf, nimemwambia atafute Mme mwingine kanisani kwao ndo watawezana na sio Mimi, mke wa hivi hanifai, hata mshahara wote anapeleka huko, hilo kanisa Jumapili moja tu kuna sadaka kama 12 hivi tangu asubuhi hadi jioni, unaweza kwenda na laki mbili usirudi hata na shilingi jioni, bado katikati ya wiki, halafu wachungaji wanaishi kifajari.

Huyo mchungaji wa hilo kanisa ameshawateka akili, mimi binafsi nilikua huko nikahama kutokana na hiyo biashara ya kutakiwa kushinda huko 24/7 na pia kutumia sehemu kubwa ya mapato yangu kanisani badala ya kujenga familia, kanisa gani wanaomba hadi salary slip? Na usipowapa watakusema sana kwamba umepotea njia na kadhalika
Kanisa gani halijali ndoa za watu?

Sio kwamba sipendi mke wangu aende kanisani, aende kwa kiasi na ratiba akizingatia kuwa yeye ni mama wa familia, inapaswa kwenda kanisani unashiriki na wenzako mchana au jioni unarudi home, jumatano unakwenda kwa maombi masaa mawili, six jioni unarudi kwako, there will be nothing wrong, lakini huwezi kwenda kushinda huko 24/7. Seven days a week, inakuja kweli hiyo?

Hata dada wa mke wangu niliempiga, mumewe pia alikuja kwangu na malalamiko kama haya ya kwangu, nimeamua simtaki tena, kwanza akili yangu imeshachanganyikiwa,
Nonsense

Ni bora nirudi kwa Rachel, alinivumilia tangu chuo hadi mtaani nikamtendea vibaya nikaoa mlokole nisiemjua, kwa kweli najuta sikujua nachofanya.
Mkuu pole kwa masahibu.
Ningependa nishauri ila kabla sijafanya hivyo, nataka kujaua anaabudu Kanisa gani na wapi? Ni TAG, EAGT, KKKT,..n.k na kanisa lake ni wapi e.g Kariakoo, Mbagala,...?
 
Heri shetani unayemjua kuliko malaika usiyemjua.
 
Duu hawa watu wanaojiita wameokoka ni mashwetani,ninao dada zangu karibia ya wote wameingia huko yani ni shida kuanzia kwa family zao hadi kwa wazazi.then wakisha kua walokole wanakua na roho mbaya na unafki wa kupitiliza..kikubwa fanya maamuz ya kiume ukicheka na nyani utavuna mabua mkuu.huyo ni mwanzo wa kuyumbisha maisha yako na familia kwa jumla.mungu kakutoa tongo tongo kugundua hlo ukibaki unamng'ang'ania utajajuta.Yani wanakuweka had ndani then unacheka nao aisee!.Kweli tunaangamia kwa kukosa maarifa
 
Malipo hapa hapa duniani, kama ulivyomtenda recho ndivyo yanavyokukuta wewe
 
Shida ya kuish na ukweni jirani kibongo bongo amri zinakuwa zinatoka Vatican
Walokole wanapumbaza waumini sana
Kuna shangaz yangu sasa vitu vyote amemalizia kwa kakobe, mwishoni mwa mwaka jana alipanga kuuza gari lake!
Duuh ukristo siku hizi ni kudai hela tu, michango michango michango daily.
Pole ndugu
 
achene kulaumu watumishi wa Mungu wakati hata hamjui ukweli wa makanisa na kazi inayofanyika huko. wengi makanisa yenu ni JF, facebook nk. jamaa kasema yeye tu lakini hatujamsia mke wake na mnaanza kuhukumu makanisa kuwa yanaharibu watu. pia kanisani kuna sera ambayo sio rasmi. oeni wa kwenu maana mnajuana vizuri. wewe ukiwa mlokole ukaoa mkarismatic lazima kuna mambo mpishane hasa hisia zinapoanza kukata na kuanza kujitambua kama umeharisha njea ya shimo la choona maji yamekatika. ndoa sio dharura na wala sio kitu cha kukimbilia kama hujakuwa na uhakika
Unasema utadhani sisi tunaishi nje ya Dunia
Makanisa yamezidi michango, wachungaji wengi ni wezi, wanawalaghai waumini kwa mistari ya kuwaletea hofu kisha watolea kila kitu na wao wabaki kuish kwa imani tu.
Sisi wenyew ni waumini na tuna ndugu wamefilisika.
 
Ulikosea kutofikiria mbele zaidi.. yaani maisha baada ya ndoa.

Naamini hizo ratiba alikuwa nazo pengine kabla ya kukutana na wewe, lkn pia ktkt uchumba wenu bado zilikuwepo kwa namna moja au nyingine ukapuuza. Na hayo ndio matokeo yake.

Cha msingi mpige ban ya maana hadi akili ikae vizuri, ajue kutofautisha maisha ya ndoa na maisha ya kanisani, kwani kila kitu kina muda wake na umpe chance nyingine endapo hatojirekebisha mrudie tu Rachel wako kama bado hajaolewa
 
Sio vizuri kuwalaumu watumishi wa Mungu maana haya ni maelezo ya upande mmoja, hatujamsikia mke wako naye akijieleza. Lakini mwisho wa siku binti aliyeokoka kweli kweli ni mwanamke bora wa kuoa. Kwani kuokoka kutamfanya [kila mwanamke] kuwa mtii kwa mme wake. Lakini wewe inaonekana ni kahaba wa kiume mwenye hadi wanawake wa akiba ktk mazingira hayo mlokole mtashindana tu usikute ameshakuona ktk ulimwengu wa Roho ukijirusha na hao wanawake zako wa akiba alipokuambia ukaja juu.
.
Hapo kwenye rangi....

Kuna ulokole unaowaziba akili baadhi ya watu kiasi cha kuwafanya mabwege. Natoa mfano. Mlokole anagombana na mwanandoa mwenza au bosi wake ofisini; kisha anakwenda Kanisani na kumwambia Mchungani "niombee, nyumbani/ofisini kuna moja, mbili, tatu." Mchungaji anamwombea, kisha mchungaji huyo anapelekea taarifa hizo kwa wachungaji wenzake au kwa Bosi wa Bosi. Hapa bosi wa bosi au mchungaji wa mchungaji wanamrukia bosi au mume. Ni majungu juu ya majungu. Hivyo ndivyo Makanisa ya kikachero yaliyoanzishwa siku hizi yanavyofanya kazi. Ni vurugu tupu. Hivyo, sio kanuni ya jumla kwamba, "kuokoka kutamfanya [kila mwanamke] kuwa mtii kwa mme wake." Ulokole mwingine ni chanzo cha migogoro ya kijamii na kiofisi. Ni ulokole wa kijinga tu.
 
Hii Dunia ina maajabu mengi sana,waweza muoa Kahaba na akatulia lkn mlokole mkashindwa kuelewana!
 
Achana na chakula ya kanisa,kam wewe sio mlokole huwezi kuwa na mlokole,ndege wafananao huruka pamoja.
 
.
Hapo kwenye rangi....

Kuna ulokole unaowaziba akili baadhi ya watu kisi cha kuwafanya mabwege. Natoa mfano. Mlokole anagombana na mwanandoa mwenza au bosi wake ofisini; kisha anakwenda Kanisani na kumwambia Mchungani "niombee, nyumbani/ofisini kuna moja, mbili, tatu." Mchungaji anamwaombea, kisha mchungaji huyo anapelekea taarifa hizo kwa wachungaji wenzake au kwa Bosi wa Bosi. Hapa bosi wa bosi au mchungaji wa mchungaji wanamrukia bosi/mume. Majungu juu ya majungu. Hivyo ndivyo Makanisa ya kikachero yaliyoanzishwa siku hizi yanavyofanya kazi. Ni vurugu tupu. Hivyo, sio kanuni ya jumla kwamba, "kuokoka kutamfanya [kila mwanamke] kuwa mtii kwa mme wake." Ulokole mwingine ni chanzo cha migogoro ya kijamii na kiofisi. Ni ulokole wa kijinga tu.
Naunga mkono hoja yako. Hawa walokole wanakuja sera za kif@l@ sana. Wanapotea kwa kutokujua maandiko wanamwamini mchungaji kuliko kitabu/Biblia. Hovyo sana
 
uko sahihi news 100. ila kama karud anataka muongee msikilize na akikubali afuate mashart na namkae mpange mpango kaz wa shirika wa maisha. na kama tatizo ni hilo tu hana jingine kaa nae usikubali kuoa mke mwi gine utaingia choo cha kike
 
Sijasoma mpaka mwisho maana nimeshindwa kuvumilia unyama wako, pumbaf* saana wewe, hata mwanamke akosee vipi huwezi kumpiga kiasi hicho
 
Enyi wake watiini waumezenu.
Enyi kina baba ishini na wakezenu kwa akili
 
Back
Top Bottom