Najuta kuoa mwanamke mlokole

Najuta kuoa mwanamke mlokole

Miezi miwili iliyopita nilipelekwa polisi na wazazi wa mke wangu, kwa kosa la kumpiga binti yao karibu nimuue, ndugu walikuja kunitoa

Iko hivi;
Huyu binti nilimuoa miaka miwili iliyopita na tuna mtoto mmoja, yeye na wazazi wake wote wameokoka, Hivi sasa naweza kusema kwamba mke wangu ameolewa na kanisa na si mimi.

Akitoka kazini saa kumi na moja jioni anakwenda kwenye maombi kanisani hadi saa tatu , na hii ratiba ni kila siku Monday to Friday, Jumamosi pia wanakwenda Jumapili ni kutwa nzima, wakati mwingine kuna mkesha katikati ya wiki, hali hii, imefanya ashindwe hata kupataa muda wa kumlea mtoto wetu wa mwaka alielazimika kumwachisha ziwa akiwa na miezi mitatu kutokana kubanwa na mambo ya kanisa.

Mtoto huyu ni kama amebadilishiwa mama, maana sasa analelewa na house girl wetu kwa hali na Mali
Ilifika pahala nikashindwa kuvumilia hali hii na nikamuita na kumueleza hali halisi na kumtaka abadilishe ratiba zake, akadai kwamba hana jinsi kwa kua ratiba ya kanisa kwake haina substitute , nikamwambia ni amri sio ombi

Akaendelea hivyo hivyo, kwa Mara ya kwanza nilimpa kipigo kwa kukaidi amri yangu, niliendelea kumpiga mara kwa Mara sababu ikiwa ni kanisa, kila tunapoitwa kusuluhishwa wazazi wake humtetea na kudai walikosea kunipa mm binti yao, ikawa tunagombana na wazazi wake vikaoni hadi nikaamua kuachana na vikao.

Mwanzoni mwa mwezi wa sita alidai kuna mkesha wa maombi siku hiyo na hivyo atalala huko, nikamwambia ukitoka huko utafute nyumba nyingine, baadae mama yake akanipigia kwamba kuna mkesha hivyo wote watalala church kwenye mkesha, nikamjibu haiwezekani wamruhusu wife arudi kwa kuwa ana mtoto mdogo, akakata simu

Kweli, wife hakurudi, ila kila saa alikua akinipigia simu karibu usiku kucha nami sikua napokea naiangalia tu hadi inakatika hadi saa kumi alfajiri, alikuja amesindikizwa na dada yake maana walijua nimekasirika sana

Walipofika tu niliwakamata wote wawili na kuwapa kipigo kizito sana hadi wife kuzirai, dada mtu aliniponyoka na kukimbilia main road huku nikiwa nimemtengua mbavu akapanda boda boda, saa moja wazazi wa wife wakaja nilikua nimemfungia stoo wakamchukua wakaenda nae.

Baadae wakanifuata kazini na polisi wakaniweka ndani kwa shambulio la kudhuru mwili, nilitoka kesho yake , kesi ikahamia Ustawi wa Jamii tuliitwa pale, mbele ya wazee wa pande zote, ikaamriwa kwamba binti arudi kwa wazazi wake hadi hapo baadae hali ikiwa nzuri, ila wazazi wake wakasema wanamchukua kimoja hawanihitaji tena, kwamba nisubiri taratibu za talaka, nikasema haina shida nipo tayari, tukaja nyumbani wakamchukua mtoto na hg na nguo zake wakarudi kwao

Nimeyasahau hayo naishi kwa auheni kiasi kwa sasa Ingawa bado nina msongo, surprisingly Friday wife akanifuata kazini hatukua tumeonana for two months, roho yangu iliingia kitu flani hata mtoto wangu sikutaka hata kuwa naenda kumuona ingawa pale ustawi wa jamii niliruhusiwa

Wife akaniomba tuongee, akasema anahitaji turudiane, akadai anaomba arudi home kwangu hata kesho yake ikiwezekana, kwamba ananipenda, kwamba tutarekebisha tu, nikamwambia haiwezekani simtaki tena

Wadau wana Jf, nimemwambia atafute Mme mwingine kanisani kwao ndo watawezana na sio Mimi, mke wa hivi hanifai, hata mshahara wote anapeleka huko, hilo kanisa Jumapili moja tu kuna sadaka kama 12 hivi tangu asubuhi hadi jioni, unaweza kwenda na laki mbili usirudi hata na shilingi jioni, bado katikati ya wiki, halafu wachungaji wanaishi kifajari.

Huyo mchungaji wa hilo kanisa ameshawateka akili, mimi binafsi nilikua huko nikahama kutokana na hiyo biashara ya kutakiwa kushinda huko 24/7 na pia kutumia sehemu kubwa ya mapato yangu kanisani badala ya kujenga familia, kanisa gani wanaomba hadi salary slip? Na usipowapa watakusema sana kwamba umepotea njia na kadhalika
Kanisa gani halijali ndoa za watu?

Sio kwamba sipendi mke wangu aende kanisani, aende kwa kiasi na ratiba akizingatia kuwa yeye ni mama wa familia, inapaswa kwenda kanisani unashiriki na wenzako mchana au jioni unarudi home, jumatano unakwenda kwa maombi masaa mawili, six jioni unarudi kwako, there will be nothing wrong, lakini huwezi kwenda kushinda huko 24/7. Seven days a week, inakuja kweli hiyo?

Hata dada wa mke wangu niliempiga, mumewe pia alikuja kwangu na malalamiko kama haya ya kwangu, nimeamua simtaki tena, kwanza akili yangu imeshachanganyikiwa,
Nonsense

Ni bora nirudi kwa Rachel, alinivumilia tangu chuo hadi mtaani nikamtendea vibaya nikaoa mlokole nisiemjua, kwa kweli najuta sikujua nachofanya.
Justification ya kuacha mke ipo kwenye hio aya ya mwisho! Mengine mbwembwe na porojo tu! Umemmisi Recho
 
Tatizo mkuu, mke uliempata sio chaguo lako. We ungemuoa huyo Rachel unaefanana nae tabia. Huwezi kuwa na mke mlokole wakati we sio mlokole, Tafuta wa kufanana naww na huyo mke wako ni mzuri kwasababu anahofu ya Mungu. Achana na wadangaji utapotea
 
Nasoma huku kama nakuona unavyoongea,.msamehe bwana atajirekebisha
 
Huyo mke shida,ila nawe mwnangu unadunda sana ,mpaka shemeji umetengua
 
Mpaka slip salary hapo hakuna ulokole hapo, mke o kapumbazwa akili na huyo mchungaji wa uongo
 
Hapo ni nguvu ya karma Inafanya Kazi bora umesema na wewe ulishawahi mtenda huyo Rachel sasa yanakurudi
 
Pole sana, mimi nilioa mlokole afu nikambadilisha. Siku hizi vi reds na vi wine anasukuma kama kawaida.
 
Fanya maamuzi mapema akiendelea kubegup utakubal an itakua busnes as usual
 
Polee sana jamaa huyo mwanamke hakufai hata kidogo bora uishi peke yako kanisani daily?
Mimi nilishawahi kuwa na demu eti anaenda kukesha church nilimwacha bila sababu nikamwambia bwana kanionyesha hatutafika kokote so kheri tuwe marafiki
 
mwanaume kamili hapigi mke wala kulalamika. kama mtu anazingua unachukua njia yako. sioni hata haja ya kuwasema mabinti wa kilokole kwa sababu hukulazimishwa kuwa naye. kama na ameona mchungaji wake ni wa maana kuliko wewe chukua maamuzi magumu au mlowase. pia kuna ulokole na ugonjwa. ulokole hausemi mtu aharibu ndoa yake. hizo ni Imani za watu wasiojua wanachofanya. pia kisheria ukimuachisha mtoto maziwa kabla ya miezi sita unaharibu ubongo na kinga yake.
pia ungeenda kuongea na mchungaji wake. sio ustaarabu kupiga mke ambaye hulingani naye nguvu. pia hata wewe unaoneka una wenge jingi maana umempiga mke wako na kuja kumangaza hapa jf wakati yeye hawezi kujitetea. unapomsema mtu hakikisha naye yupo na anaweza kujitetea kama wewe. pia kwangu sioni tija ya ulichofanya hapa. mahusiano sio jela. mtu akizingua unajiachia kivyakooo
Acha tabia za Dar es Salaam, mwanamke akizingua lazima apigwe hata makofi kumkumbusha utii wa amri halali ya mume wake. Nyie ndio mke anawajibu vibaya mnashindwa kumnoa mnaanza kuomba ushauri kwa Chris Mauki
 
KWANINI UMPIGE MKEO?! KUMPIGA MKEO NI UDHAIFU, UJINGA NA USHAMBA.
Ninyi wawili mna mitazamo miwili tofauti, yeye anaona kanisa ni muhimu zaidi kwake na wewe unaona familia ni muhimu zaidi kwako kuliko kanisa. Mtazamo wake huu umetokana na malezi toka kwa wazazi wake (Hata wazazi wake walishakuambia kwamba wakati mwingine huwa wanalala kwenye mkesha kwa ibada). Hata na wewe mtazamo wako yawezekana umeuona kutokana na malezi au mapokeo jinsi unavyoishi na ulivyoyaona maisha kwa jamaa zako, n,k.

Ulichotakiwa kufanya ni kukaa chini na mkeo mpendwa (maana ulimchagua mwenyewe) na ulipaswa kuongea naye kwa upendo, heshima kama mwanandoa mwenzako na si kumuambia kwamba: 'ni amri na si ombi!'. Mlipaswa mjadiliane juu ya faida na hasara ya yote mawili - ingechukua muda lakini hatimaye mgepata suluhisho. LAKINI SIO KUMPIGA!

Kilichotokea ni kwamba kwa kuwa wewe ni dhaifu (huwezi kujenga hoja) ulishindwa kujenga hoja ya maana, ili kumshawishi mkeo aone umuhimu wa familia kwanza badala ya kanisa. Baada ya kushindwa kumshawishi ikabidi utumie nguvu (Maana ndicho hicho tu ulichonacho) na kuanza kumpiga.

Sasa unataka kukimbilia kwa Rachel, ili naye mkitofautiana mitazamo uanze kumpiga kama ulivyofanya kwa mkeo. Rachel labda yeye hataenda kwenye mikesha ya ibada, lakini lazima atakuwa na kitu/mtazamo tofauti kuliko wewe, utafanyaje? Naye utampiga? Utapiga wanmgapi!!!

Utawakimbia wangapi? Kwanini unakimbia matatizo??!
Mkeo sasa amekupa fursa ya kukaa naye mrekebishe mambo, tena amesema anakupenda na anataka kurudi nyumbani, sio ndicho ulichokuwa unakitaka?! Umeshazaa mtoto mmoja na mkeo, unataka ukamzalishe Rachel naye mtoto?, mgombane, umpige na kisha umwache! Utakuwa na watoto wawili na kila mtoto na mama yake, si ndio!!??

Rachel, huko uliko kama unanisikia akija huyu jamaa usimkubali, mwambie arudi kwa mkewe!

ACHANA NA RACHEL, USIENDE KUMHARIBIA MAISHA YAKE. YAANI WEWE UVURUGE HUKO, NA YEYE AKAE KUKUSUBIRI WEWE TU, HAPANA!. MRUDIE MKEO, WEKENI MEZANI HOJA ZENU (KANISA VS FAMILIA) NA KISHA MZIREKEBISHE. LEENI MTOTO WENU NA IKIWEZEKANA MUONGEZE MTOTO MWINGINE NA MWINGINE .

MWISHO - ACHA TABIA YA KUMPIGA MKEO, SHEMEJI ZAKO NA WAKE WA WENZIO
Acha kuiga akili za kizungu, kwa waafrika mke akileta kimdomo ruksa kumpiga vikofi vichache ili kumkumbusha kutii amri halali ya mume wake. Mm napinga kumpiga mke kikatili had akavimba au kutoka dam
 
So ndani usiku mzima alikuwa anakuacha na house girl? Me ningempa mimba alafu na mke nafukuza.
Sasa kama yeye ndio anajua baba anakulaje leo..anakuandalia chakula..anakufulia nguo..na anakulelea mwanao... yeye si ndio mke sasa kuna haja gan ya kuishi na huyo mtumwa wa mchungaji?
Akili kumkichwa.. najua ma house girl wanakuaga wachafchafu kihasi..

USHAURI WANGU HUDUMA ZOTE NZURI ULIZOKUA UKIMPA MKE HAMISHIA KWA HOUSEGIRL ASUKE VIZURI MNUNULIE MAVAZI YAKUTOSHA MFANYISHE MAZOEZI ALE VEMA NA AMINI UTAMPENDA MAANA HAKUNA MSICHANA MBAYA DUNIAN.
 
Mtu yoyote akishakuwa extremist katika jambo lolote ni shida.

Me nna mother mdogo, ndugu zake walimfungulia biashara ya duka ili zipatikane hela za kukidhi lengo flan.

Cha ajabu, dukani anakaa muda mchache sana. Muda mwingi anafunga duka sababu ya kwenda church.

La kushangaza zaidi daily lazima atoke na sadaka, na kila hela inayoingia anatoa fungu la 10 anapeleka church (badala ya kusubiria faida).

Duka halikuchukua miezi mingi likafa.
 
Tafuta mwingine wa kukesha bar, kupata mwanamke mwenye hofu ya Mungu ni neema tu mambo mengine nnaweza kuyajenga tarabu.....
 
Back
Top Bottom