Najuta kuoa mwanamke mlokole

Najuta kuoa mwanamke mlokole

duhhh polee mzee mzima ila but kuna nafasi naona mnaweza kukaa na kupanga mkayamaliza!

Vipo vinavyovumilika na visivyo.
Kosa kubwa ni mke kuwashilikisha wazazi.
Halafu,kama unachokisema ni kweli unastahili pongezi.Wazazi wakasema subiri taratibu za taraka!Wambie wafanye haraka, huyo hafai.Hajitambui,na hajielewi.
Wewe msaidie tu kulea mtoto,bila kinyongo,lakini swala la kurudiana nae acha.Sheria imeingilia, wazazi wake wameingilia, we ni mwanaume usiende kuliombea ushauri,amua mwenyewe. Kwani kama hakugundua kosa lake,akkubari wazazi wake wakudhalilishe,unategemea leo ndo wameacha? Labda;kama wataitisha kikao cha wazee na wale polisi na ustawi wa jamii wakakili kosa lao na kumpotosha mtoto wao,unaweza.Ila hata akibadilika atakuwa tu anakuogopa siyo kwamba amebadilika
 
mwanaume kamili hapigi mke wala kulalamika. kama mtu anazingua unachukua njia yako. sioni hata haja ya kuwasema mabinti wa kilokole kwa sababu hukulazimishwa kuwa naye. kama na ameona mchungaji wake ni wa maana kuliko wewe chukua maamuzi magumu au mlowase. pia kuna ulokole na ugonjwa. ulokole hausemi mtu aharibu ndoa yake. hizo ni Imani za watu wasiojua wanachofanya. pia kisheria ukimuachisha mtoto maziwa kabla ya miezi sita unaharibu ubongo na kinga yake.
pia ungeenda kuongea na mchungaji wake. sio ustaarabu kupiga mke ambaye hulingani naye nguvu. pia hata wewe unaoneka una wenge jingi maana umempiga mke wako na kuja kumangaza hapa jf wakati yeye hawezi kujitetea. unapomsema mtu hakikisha naye yupo na anaweza kujitetea kama wewe. pia kwangu sioni tija ya ulichofanya hapa. mahusiano sio jela. mtu akizingua unajiachia kivyakooo
Umejibu vema sana
 
Nashauri mkae muongee kumbuka mtoto kulelewa na baba au mama mwingine ni shida. Ila pia kama anakusumbua sana basi tafuta mwingine.
 
Sawa...aisee kuna mwingine yupo huku na hajaolewa ila kanisani karibia kila siku. Yaani utasikia siwezi kosa kanisani...namshukuru sana Mama yake anampelekaga shamba siku za katikati ya siku...ndio kiherehere huisha kiasi. Lakini mama akizembea mtu hushinda kanisani. Huyu kiumbe ana miaka 35 na yupo kwa mama yake analelewa kula kulala...yaani wanawake Mungu awafungue kwakweli!!!!!... Anakataa hadi wa kumuoa huo umri na anachagua...hahhaaa. Pole sana kiongozi kwa huyo mkeo...hao watu wanakuaga nusu matahira nusu mtu!!!...Luna wengine wakiokoka inakuwa ni msaada kwa wengine na familia zao....lakini wengine inakuwa ni mzigo wa misumali. Lirudishe kwao kwanza ili likasali vizuri
 
Nimefurahi sana kwamba ndoa inapitia changamoto ndio utu uzima huo .

Pole kwa kukosa uelewa Wa kutosha mke kalala kanisani ukapiga mpaka kazimia je angelala kwa mwanamume?

Jitafakari kwa kina halafu muite mkeo kaeni tafakarini pamoja kwa undani maana nyie ndio wanandoa wenyendoa yao .baada ya hapo mfikie muafaka kwa pamoja wekeaneni masharti ili kulinda ndoa yenu .

Baada ya hapo itisheni familia zenu wazazi ongeeni nao wakiwepo wekeni bayana makubaliano yenu ,nafikiri utakua mmemaliza.

Anzeni maisha mapya ya Furaha kama ikishindikana msipigane mwambie arudi kwao tu ndio utakua vizuri .


Ukipiga utajikuta unabomoa halafu garama yake ni Kubwa mno
 
Kila kitu kikizidi inakua hatareeeee. Alitaka ndoa ya nini angeishi km mtawa tuu ili ashinde vizuri huko knsn kuliko kumtesa mtoto.
 
Miezi miwili iliyopita nilipelekwa polisi na wazazi wa mke wangu, kwa kosa la kumpiga binti yao karibu nimuue, ndugu walikuja kunitoa

Iko hivi;
Huyu binti nilimuoa miaka miwili iliyopita na tuna mtoto mmoja, yeye na wazazi wake wote wameokoka, Hivi sasa naweza kusema kwamba mke wangu ameolewa na kanisa na si mimi.

Akitoka kazini saa kumi na moja jioni anakwenda kwenye maombi kanisani hadi saa tatu , na hii ratiba ni kila siku Monday to Friday, Jumamosi pia wanakwenda Jumapili ni kutwa nzima, wakati mwingine kuna mkesha katikati ya wiki, hali hii, imefanya ashindwe hata kupataa muda wa kumlea mtoto wetu wa mwaka alielazimika kumwachisha ziwa akiwa na miezi mitatu kutokana kubanwa na mambo ya kanisa.

Mtoto huyu ni kama amebadilishiwa mama, maana sasa analelewa na house girl wetu kwa hali na Mali
Ilifika pahala nikashindwa kuvumilia hali hii na nikamuita na kumueleza hali halisi na kumtaka abadilishe ratiba zake, akadai kwamba hana jinsi kwa kua ratiba ya kanisa kwake haina substitute , nikamwambia ni amri sio ombi

Akaendelea hivyo hivyo, kwa Mara ya kwanza nilimpa kipigo kwa kukaidi amri yangu, niliendelea kumpiga mara kwa Mara sababu ikiwa ni kanisa, kila tunapoitwa kusuluhishwa wazazi wake humtetea na kudai walikosea kunipa mm binti yao, ikawa tunagombana na wazazi wake vikaoni hadi nikaamua kuachana na vikao.

Mwanzoni mwa mwezi wa sita alidai kuna mkesha wa maombi siku hiyo na hivyo atalala huko, nikamwambia ukitoka huko utafute nyumba nyingine, baadae mama yake akanipigia kwamba kuna mkesha hivyo wote watalala church kwenye mkesha, nikamjibu haiwezekani wamruhusu wife arudi kwa kuwa ana mtoto mdogo, akakata simu

Kweli, wife hakurudi, ila kila saa alikua akinipigia simu karibu usiku kucha nami sikua napokea naiangalia tu hadi inakatika hadi saa kumi alfajiri, alikuja amesindikizwa na dada yake maana walijua nimekasirika sana

Walipofika tu niliwakamata wote wawili na kuwapa kipigo kizito sana hadi wife kuzirai, dada mtu aliniponyoka na kukimbilia main road huku nikiwa nimemtengua mbavu akapanda boda boda, saa moja wazazi wa wife wakaja nilikua nimemfungia stoo wakamchukua wakaenda nae.

Baadae wakanifuata kazini na polisi wakaniweka ndani kwa shambulio la kudhuru mwili, nilitoka kesho yake , kesi ikahamia Ustawi wa Jamii tuliitwa pale, mbele ya wazee wa pande zote, ikaamriwa kwamba binti arudi kwa wazazi wake hadi hapo baadae hali ikiwa nzuri, ila wazazi wake wakasema wanamchukua kimoja hawanihitaji tena, kwamba nisubiri taratibu za talaka, nikasema haina shida nipo tayari, tukaja nyumbani wakamchukua mtoto na hg na nguo zake wakarudi kwao

Nimeyasahau hayo naishi kwa auheni kiasi kwa sasa Ingawa bado nina msongo, surprisingly Friday wife akanifuata kazini hatukua tumeonana for two months, roho yangu iliingia kitu flani hata mtoto wangu sikutaka hata kuwa naenda kumuona ingawa pale ustawi wa jamii niliruhusiwa

Wife akaniomba tuongee, akasema anahitaji turudiane, akadai anaomba arudi home kwangu hata kesho yake ikiwezekana, kwamba ananipenda, kwamba tutarekebisha tu, nikamwambia haiwezekani simtaki tena

Wadau wana Jf, nimemwambia atafute Mme mwingine kanisani kwao ndo watawezana na sio Mimi, mke wa hivi hanifai, hata mshahara wote anapeleka huko, hilo kanisa Jumapili moja tu kuna sadaka kama 12 hivi tangu asubuhi hadi jioni, unaweza kwenda na laki mbili usirudi hata na shilingi jioni, bado katikati ya wiki, halafu wachungaji wanaishi kifajari.

Huyo mchungaji wa hilo kanisa ameshawateka akili, mimi binafsi nilikua huko nikahama kutokana na hiyo biashara ya kutakiwa kushinda huko 24/7 na pia kutumia sehemu kubwa ya mapato yangu kanisani badala ya kujenga familia, kanisa gani wanaomba hadi salary slip? Na usipowapa watakusema sana kwamba umepotea njia na kadhalika
Kanisa gani halijali ndoa za watu?

Sio kwamba sipendi mke wangu aende kanisani, aende kwa kiasi na ratiba akizingatia kuwa yeye ni mama wa familia, inapaswa kwenda kanisani unashiriki na wenzako mchana au jioni unarudi home, jumatano unakwenda kwa maombi masaa mawili, six jioni unarudi kwako, there will be nothing wrong, lakini huwezi kwenda kushinda huko 24/7. Seven days a week, inakuja kweli hiyo?

Hata dada wa mke wangu niliempiga, mumewe pia alikuja kwangu na malalamiko kama haya ya kwangu, nimeamua simtaki tena, kwanza akili yangu imeshachanganyikiwa,
Nonsense

Ni bora nirudi kwa Rachel, alinivumilia tangu chuo hadi mtaani nikamtendea vibaya nikaoa mlokole nisiemjua, kwa kweli najuta sikujua nachofanya.
Ndg Re hujafanya vizuri!
Kanisani kuna wazee kuna uongozi kwa nini hukupeleka issue yako ipatiwe ufumbuzi??
Inaonyesha hata maadili ya wokovu huna, si busara kupiga mkeo.
Maombi yanajenga mji, mkeo anakuombea ili ubadilike, tuliza akili uwe na hekima ujenge mji wako, usiubomoe.
Ni PM kama sio porojo tuelewane!!
 
Enyway umeongea upande mmoja Wa shilingi, yaani upande wako, but hatujui upande wake anasemaje kwa yote hayo. Kama sio tungo basi ujue hapo ulifanya inshu mbaya.

Mambo ya dini kwa wenye dini zao, ukute angeolewa na MTU Wa sampuli yake muda wote wangekuwa huko kwenye misa.

Wewe unaoa mtu Wa misa ilihali wewe si MTU Wa misa wapi na wapi..!
Huyu bwana kaeleza vizuri tu. Kwake tatizo siyo mke kwenda kanisani. Tatizo ni kutokuwa na ratiba ya kuunganisha umuhimu wa kanisa na majukumu ya familia. Huwezi kumuachisha ziwa mtoto wa miezi 3 ili ukeshe kanisani. Hilo siyo kanisa......
 
Kwanza nakupa pole mkuu.Makanisa yamekuwa chanzo cha kuharibu familia nyingi miaka hii,Natoa story Fupi kwa hapa kazini kuna mama ambaye nipo naye ofisi moja huyu mama ni mwathirika lakini hataki kutumia dawa sababu mchungaji anamkataza
 
mwanaume kamili hapigi mke wala kulalamika. kama mtu anazingua unachukua njia yako. sioni hata haja ya kuwasema mabinti wa kilokole kwa sababu hukulazimishwa kuwa naye. kama na ameona mchungaji wake ni wa maana kuliko wewe chukua maamuzi magumu au mlowase. pia kuna ulokole na ugonjwa. ulokole hausemi mtu aharibu ndoa yake. hizo ni Imani za watu wasiojua wanachofanya. pia kisheria ukimuachisha mtoto maziwa kabla ya miezi sita unaharibu ubongo na kinga yake.
pia ungeenda kuongea na mchungaji wake. sio ustaarabu kupiga mke ambaye hulingani naye nguvu. pia hata wewe unaoneka una wenge jingi maana umempiga mke wako na kuja kumangaza hapa jf wakati yeye hawezi kujitetea. unapomsema mtu hakikisha naye yupo na anaweza kujitetea kama wewe. pia kwangu sioni tija ya ulichofanya hapa. mahusiano sio jela. mtu akizingua unajiachia kivyakooo
Aisee jamaa yangu wewe unatoka kwetu mwambao au sio
 
Kama karudi mpokee ila mkae chini kupanga ratiba ya church au kama hilo dhehebu unaona sio sharti mojawapo la wewe kumrudisha ndoani ahamie kanisa unalo sali wewe, kumbuka huyo ni mkeo na ana mtoto wako pia
 
Nimefurahi sana kwamba ndoa inapitia changamoto ndio utu uzima huo .

Pole kwa kukosa uelewa Wa kutosha mke kalala kanisani ukapiga mpaka kazimia je angelala kwa mwanamume?

Jitafakari kwa kina halafu muite mkeo kaeni tafakarini pamoja kwa undani maana nyie ndio wanandoa wenyendoa yao .baada ya hapo mfikie muafaka kwa pamoja wekeaneni masharti ili kulinda ndoa yenu .

Baada ya hapo itisheni familia zenu wazazi ongeeni nao wakiwepo wekeni bayana makubaliano yenu ,nafikiri utakua mmemaliza.

Anzeni maisha mapya ya Furaha kama ikishindikana msipigane mwambie arudi kwao tu ndio utakua vizuri .


Ukipiga utajikuta unabomoa halafu garama yake ni Kubwa mno
Kikao na mke!!! Kikao na wazazi!!!! Hiyo ni ndoa au tawi la chama cha mapinduzi?

Mke kama hajui sababu za kuolewa hamna jinsi arudi tu nyumbani kwao.
 
Hapo okokeni wote muwe mkishinda church ndo mtaendana
 
achene kulaumu watumishi wa Mungu wakati hata hamjui ukweli wa makanisa na kazi inayofanyika huko. wengi makanisa yenu ni JF, facebook nk. jamaa kasema yeye tu lakini hatujamsia mke wake na mnaanza kuhukumu makanisa kuwa yanaharibu watu. pia kanisani kuna sera ambayo sio rasmi. oeni wa kwenu maana mnajuana vizuri. wewe ukiwa mlokole ukaoa mkarismatic lazima kuna mambo mpishane hasa hisia zinapoanza kukata na kuanza kujitambua kama umeharisha njea ya shimo la choona maji yamekatika. ndoa sio dharura na wala sio kitu cha kukimbilia kama hujakuwa na uhakika
Imeandikwa mpende jirani yako kama unavyoipenda nafsi yako lakini huyu hata mtoto wake mwenyewe hakika haipendi.

Si vyema kutetea manyanyaso mtoto anayoyapata kwa kivuli cha dini.

Na hakika ninasadiki haiwezi kuwa sawa, ikiwa ni sawa je wachungaji wa kesho watatoka wapi kama watoto wa waumini hawapati upendo na malezi ya wazazi wao.

Hakika watalaaniwa wazazi wapumbav namna hii

Uko sawa baba mtoto, ila kumbuka kuua hakufundishi, imeshindikana achana nae lea mwanao

Juzijuzi tu hapa kuna mtumishi mmoja aliwapa mimba wake za watu zaidi ya ishirini kama mnakumbuka na magazeti yaliandika eti anajibu shutuma kwa kusema He was delivered by Holy spirit to bless them kweli?!!

Mazingira hayo ni miongoni mwa vishawishi pia
POLE, POLE SANA
 
TANGAZO TANGAZO TANGAZO,
Tunaomba na wanaofaid ndoa hata kdg humu JF mjitokeze, tupeane matumain hata kdg.


Mana JF kila siku nikukatishana tamaa za kuoa, Haijalishi iwe kweli au si kweli, ila 90% ya thread za mapenz humu ni za kutendwa, kuachwa au hata visa vya mauaji kwenye ndoa.

Chama changu cha CHAPUTA kinazid kufanya usajili kila asubuh, tumeshaizd CCM kwa wing asaiv

POLE KWA WOTE WALIOTENDWA NA WALIOTEKWA KWENYE MAPENZI/NDOA
 
Hahaaaaaa kwanza nimecheka sana bro na Pili ulochokifanya n cha kiuanaume mwanaume lazma uwe na mu stand huyo Shem ka kwel alikuwa anaomba angeomba Hyo hali ya ugomvi isitokee lkn inaonekana huko Church walikuwa wapiga dili tu

Swla la kurudiana nae siwez kukushaur ww hapo amua vp anakufaa au hafai bas



Ila. Na imagine hicho kisago ulichowatwisha yy na Dada mtu nacheka sana hahaaaaaa
 
Back
Top Bottom