Najuta kuoa hususani katika umri mdogo nilionao

Najuta kuoa hususani katika umri mdogo nilionao

Bos ndoa zetu pia ziko ivyo yaan home sio sehem salama kabisa ni full stress aisee mtu ananuna bila mpangilio na kuongea kama chiriku
Hahahah ndoa za kibongo ni matatizo matupu. Lengo la kuoa ni kujenga familia bora yenye furaha na amani ila utashangaa badala ya furaha na amani inakuwa ni kero na matatizo na kichocheo mara nyingi huwa ni mke.

Good communication matters, ila mke anakuwa muasisi wa ligi, hataki ufanye kinyume na anavyojiskia yeye hata kama anakosea. Ukimkosoa tu umeanzisha tatizo. Utanuniwa for days!!! Huu usenge ndio unaonifanyaga nimtie mtu makofi 😎😎😎 mwisho nionekane mshenzi. You have issues sema, usijinunishe tu kama paka mwenye mimba ukidhani ndio suluhu.
 
SK2016, Siku zote mke akisema muachana au ataondoka kwao hapo kuna mambo mawili.

1 kwao Ndugu zake wanamjaza kiburi kwamba kama vipi arudi nyumbani.
2 kuna jamaa linamjaza upepo wa kiburi na bila mwanamke kujua kwamba huyo mwanaume anampenda kwakuwa yuko kwa mme wake.
Fanyia kazi hayo Mkuu utapata jibu,

Sent using Jamii Forums mobile app
3. Anajihisi anaweza kusavaivu bila wewe.

4. She dont Love u. Either hisia zimeisha
 
Siku zote mtafutaji ana nidhamu ili apate anachotaka ila hali huwa tofauti endapo alishakipata anachotaka nidhamu huanza kuwa hafifu.
ni kweli ingawa pia wapo ambao nidhamu zao hua hazishuki hata baada ya kupata wanachotaka
 
Mwanamke wako ni mchoyo. Hii sifa inatosha kabisa kum disqualify kuwa mke.

Its Obvious mwanamke wako ni mbinafsi sana na hata ndugu zako watakuwa hawakanyagi hapo kwako ila wake wanakuja kujigalagaza kabisa hapo na mamisosi na kila kitu. Hii tabia ni personal, huenda ni athari za malezi mabovu ila ulipaswa uyajue hayo kabla hujaoa. Kuna uzi wangu flani kuhusu Volunteer program. Upitie utaelewa kitu ambacho ulikikosea.

To go about with decisions itategemea je upo tayari kuendelea kuishi na stress za mtu ambaye ulitarajia atakuwa patner katika maisha yako ama la?!
tuwekee link ya huo uzi niupitie
 
Hahahah ndoa za kibongo ni matatizo matupu. Lengo la kuoa ni kujenga familia bora yenye furaha na amani ila utashangaa badala ya furaha na amani inakuwa ni kero na matatizo na kichocheo mara nyingi huwa ni mke.

Good communication matters, ila mke anakuwa muasisi wa ligi, hataki ufanye kinyume na anavyojiskia yeye hata kama anakosea. Ukimkosoa tu umeanzisha tatizo. Utanuniwa for days!!! Huu usenge ndio unaonifanyaga nimtie mtu makofi 😎😎😎 mwisho nionekane mshenzi. You have issues sema, usijinunishe tu kama paka mwenye mimba ukidhani ndio suluhu.

ndoa za cku hz ni visanga
 
Hahahah ndoa za kibongo ni matatizo matupu. Lengo la kuoa ni kujenga familia bora yenye furaha na amani ila utashangaa badala ya furaha na amani inakuwa ni kero na matatizo na kichocheo mara nyingi huwa ni mke.

Good communication matters, ila mke anakuwa muasisi wa ligi, hataki ufanye kinyume na anavyojiskia yeye hata kama anakosea. Ukimkosoa tu umeanzisha tatizo. Utanuniwa for days!!! Huu usenge ndio unaonifanyaga nimtie mtu makofi [emoji41][emoji41][emoji41] mwisho nionekane mshenzi. You have issues sema, usijinunishe tu kama paka mwenye mimba ukidhani ndio suluhu.
[emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mkuu itakuwa ndo walivyoambiwa kwenye Kitchen part...!!
 
ni kweli ingawa pia wapo ambao nidhamu zao hua hazishuki hata baada ya kupata wanachotaka
Ni kweli ila ni wachache sana hasa kwa ulimbukeni uliotujaa wabongo.

Imagine mwanaume anavyokuwaga mnyenyekevu akiwa kapuku akipata hela anasahau kwamba alikula dagaa na tembele na mkewe wakafika walipofika. Hali kadhalika mke nae anakuwa na adabu kabla hajaolewa na kusomeshwa, akishatafutiwa na kazi anamuona mume boya wa mwisho ila HR ndio mtu wa maana na wanaanza kuchakatana kinyemela.
 
Kama analazimisha kuondoka mwache aondoke Ila hakikisha unajua anaondoka kwenda wapi.

sio anaondoka kwenda kwa kajamaa Fulani wanakulana wakigombana kidogo anaomba msamaha wa kurudi na wewe unampokea.

kitu kingine usione haya kumnasa vibao vya hapa na pale huwa Wana tabia za kupima upepo hawa.

kubwa kuliko vyote mkalishe chini mpe terms and condition zako kwenye suala zima la familia yenu Kisha kaa kwa kutulia anyoee au asuke.

nimemaliza.[emoji3578][emoji3578]
 
Ni kweli ila ni wachache sana hasa kwa ulimbukeni uliotujaa wabongo.

Imagine mwanaume anavyokuwaga mnyenyekevu akiwa kapuku akipata hela anasahau kwamba alikula dagaa na tembele na mkewe wakafika walipofika. Hali kadhalika mke nae anakuwa na adabu kabla hajaolewa na kusomeshwa, akishatafutiwa na kazi anamuona mume boya wa mwisho ila HR ndio mtu wa maana na wanaanza kuchakatana kinyemela.
rafiki angu umeandika kwa hisia kweli
 
Ndoa za watu hazina tatizo lolote, wewe ndo ulifeli kwny uchaguzi wa mke wa kuoa na utajuta maisha yako yote kama mwanzo ndo huo....

Kuna wakati mnaoa vichaa bila kujua.
 
Mwanamke wako ni mchoyo. Hii sifa inatosha kabisa kum disqualify kuwa mke.

Its Obvious mwanamke wako ni mbinafsi sana na hata ndugu zako watakuwa hawakanyagi hapo kwako ila wake wanakuja kujigalagaza kabisa hapo na mamisosi na kila kitu. Hii tabia ni personal, huenda ni athari za malezi mabovu ila ulipaswa uyajue hayo kabla hujaoa. Kuna uzi wangu flani kuhusu Volunteer program. Upitie utaelewa kitu ambacho ulikikosea.

To go about with decisions itategemea je upo tayari kuendelea kuishi na stress za mtu ambaye ulitarajia atakuwa patner katika maisha yako ama la?!
Mkuu umenena vyema lkn mchoyo pia mtu! hata mimi mchoyo kwa mengi isipokuwa familia yangu tu, ila sipendi kuitwa hivo!

Atumie huo uchoyo wa mke wake km fursa, dhidi ya maadui, ili mali yake isitawanyike kwa rafiki na ndugu! asimuache, unajua ndg ni adui mbaya sana, ke wana siri sana labda walishaomba! akaona awa block ki ivo? hata ma wifi wanaweza kula mchongo ili kumuachanisha!

ke'' asiye mchoyo utakaa chini mwenyewe atagawa chakula chote, na kila kinacho faa kwa kila jirani mwenye shida, dose dawa za mwanao atazigawa kwakila mtoto mgonjwa. mhusika aache stress!

Ndg za mume ni rahisi kujitafunia mambo! hata kwa mbinti zako! lkn wa kikeni ngumu mno! hata leo hii haupo wajomba wakomaa bila ubaguzi.
 
Hahahah uchoyo unaoongelea wewe ni positive ila sio uchoyo wa kijinga wa kuficha chakula. Kinachotakiwa ni kiasi tu kwa kila jambo na wala si choyo. Hao unaowasemea wewe ni vimwaga au wapenda sifa...Kuwa mpenda sifa haihusiani na kutokuwa mchoyo.

Mke anayejitambua hawezi kuficha vyakula au kukataa kupika chakula wageni wakija.
 
Mwanamke mchoyo anafukuza baraka hafai kabisa
 
Mkuu anavyo kutishia anaondoka wewe usipanic wala usionyeshe kumtaka Sana .. SIKU akikuambia naondoka mwambie sawa wewe ondoka Kama ndio umeamua hivyo, tena mjibu kwa ujasiri mkubwa hata akianza kupanga nguo usimzuie.. nakushauri hivi ili kujizuia Kama no muda wakazi wewe nenda kazini na usimtafute kabisa kujua Kama ameondoka , Kama sio muda wakazi tafuta mahali pamechanganyia nenda kapate maji kidogo au kaoshe macho zeni urudi mida ya saa tano usiku.
NOTE: UKIMKUTA HAJAONDOKA USIMSEMESHE INGIA NDANI ULALE NA SIKU AKIRUDIA KUKUAMBIA NAONDOKA HAKIKISHA UNAMCHAPA HASWA HASWA UTOTO UTAMWISHA .

mm wangu alikua anapenda kuniambia anaondoka au tu achane nikawa mkimnya tuu siku moja jamaa yangu akanambia jaribu hiyo mbinu wewe akikuambia anaondoka mwambie sawa, niliwaza Sana ila baadae nikakubaliana ... Siku kajichanganya Nika mjibu sawa nenda nafunguo mpe jamaa yangu (jirani mwenzetu nilikua na muheshimu Sana) zeni nikaondoka zangu nikatoka nje ya wilaya maana nilikua free nikatafuta na chumba cha wageni nikalala huko nirudi kesho yake.. Cha ajabu Hadi Leo hii HAJAONDOKA nakila akiwa na mimi faraga ananiomba msamaha akidai alinikosea Sana maana sijui kichwani mwake anafikiria Nini ....
 
Mwanamke mchoyo anafukuza baraka hafai kabisa
Mkuu watu ni wachoyo hata walioko ndani ya Malango yako, kwa mkono Wako, siku pata matatizo kazini au cheti fake uone muziki wake! utajua uchoyo wa Mkeo ni cha mtoto. watakucheka hao! kukusimanga waziwazi, mpaka ujifie! ndo maadui hao! mkeo anakulinda!

Huku unachekwa! Vitoto vyako ndo kabisaa! ''Baba enu alichezea maisha'' vitaolewa mapema! English Media vitatoka, but endelea ufurahie huu muziki!

Wakati marehemu baba yako akiwa na maisha murua huko Mkoani jamaa walijaa home kwenu, wanapitia hapo wakienda shule wanapata cha juu! hao hao ukikutana nao Bongo yamesha wanyookea, hawataki kukujua, akijitahidi utaishia mlangoni wima! ukiishi kwake atakutoza hela ya umeme! chakula nk!

Kumuacha Mkeo Mzuri mzuri! kwa kitu kidogo! haiswii! umeshindwa kuishi nae kwa akili Mkuu! kituko ni pale upatapo mpya, yaani hakupi papuchi yake, eti unamchakaza! ukirudi angukia kule tayari kesha olewa, hapo chacha!!! Omba sana kwa Mungu! uvumilivu ndo siraha pekee!
 
Hahahah uchoyo unaoongelea wewe ni positive ila sio uchoyo wa kijinga wa kuficha chakula. Kinachotakiwa ni kiasi tu kwa kila jambo na wala si choyo. Hao unaowasemea wewe ni vimwaga au wapenda sifa...Kuwa mpenda sifa haihusiani na kutokuwa mchoyo.

Mke anayejitambua hawezi kuficha vyakula au kukataa kupika chakula wageni wakija.
Mkuu cha msingi kumuomba Mungu, wewe umfanye mkeo awe ''prayer warrior'', ili usiwe na jicho la negativism dhidi yake, ukifikiri na kijiuliza je? km mwanangu akiwa km hivi je nitamkataa? ili amchukue nani?

kikubwa usiangalie padoogo ni kuchukuliana madhaifu yenu! wewe unayo maudhaifu anayo kuvumilia, ajabu yeye pia anakuona mbinafsi ila amekukubali! hasemi tu, kitu hiki waafrica wote hawajiulizagi! ila kuyaona ya wengine wao! kwa kifupi aweza kuwa mchoyo sawa!! lkn bado akawa na haya ;

1. Mlezi mzuri wa Afya ya familia ikiwa ni pamoja na wewe Baba,

2. Mpole,Mrembo, ana afya nzuri, siyo mgonjwamgojwa! anakuzalia vitoto vizuri, afya nzuri, unavifurahia uwepo wao kwako!

3. Siyo malaya, utalea watoto wasio wako!!! macho kumchuzi. anakuepusha na magonjwa, ulinzi huo anakupa!

4. Siyo mchawi, naomba kusema ''Limbwata linachakaza Akili na mwili sanasana'' km hujawahi kula maji ya mahiti hapa utakula!!

5. Mvumilivu, mwaminifu, umepata mshiko umekosa yupo na wewe!

6. Mcha Mungu. '' ni chanzo cha maarifa''

7. Mbunifu na mchapa kazi. ili kuongeza kipato chako! hata ukifa leo huna wasiwasi familia itasongeshwa! atakuuguza na atakuzika, siyo unakufa huku mke hana habari! ndo kwanzaa anajirusha Dubai!

8. Nyota yake inawaka kwako, hapa usiombe kuoa mke wa mlango wa nane, kule Tanga wanajua hii makitu.

Hapa mkuu wewe ndiyo upime sasa uzito unaelemea wapi? endapo ni mchoyo then ana madhaifu mengi km haya Mungu atakuepusha tu, na utamgundua kirahisi wkt wa uchumba!

Lkn pia unaweza mwacha akijua udhaifu wako binafsi usioujua, sababu hajakwambia, lkn wewe umemwambia ni rahisi yeye kujirekebisha huko mbele, Dume lingine ndo litapata faida! atadumu ktk ndoa mpya!
 
Emb chunguza kwanza unamridhisha mkeo kitandani? Au unakaa mda gani kukutana nae kimwili? Wanaume wengi hawajui na wanawake ni ngum kusema wazi kua humridhishi chunguza ilo kwanza
 
Habari wakuu,

Natumai mko na furaha na amani tofauti na mimi

Hapo nyuma nilikuwa nawashangaa sana vijana wengi tu ambao wanaponda sana kitu kuoa.

Nilikua nikiwabeza sana na kuhisi kama wamechanganyikiwa hivi kutokana na experience yangu katika ndoa kwani ilikuwa ni maisha mazuri sana na yenye amani mno.

Ila sasa najutaa, nasema tena najutaaaa!

Mimi ni kijana wa miaka 28 na ni muajiriwa Serikalini. Pia najishughulisha na uwekezaji katika kilimo so kipato changu ni cha wastani sio kibaya kihivyo.

Kisa cha kuleta huu uzi ni mke wangu kuwa na tabia za ajabu za kununa nuna kila siku bila hata ya sababu ya msingi.

Akinuna anakaa siku mzima hanisemeshi na kunitumia sms za vitisho na kunishikilia kwamba nimuache ingawa huwa simjibu lolote.

Jana kuna workmate wangu (me) ambaye ni jirani yetu, mke wake amepata dharura kidogo so hayupo.

Wakati natoka job nikaona si mbaya kwa vile nilimsikia anataka kwenda hotelini kula nikaona niongee na wife ili aje kupata chakula cha mchana tu home.

Tatizo lilianzia hapo. Wife hakuridhika na hilo akaniambia hataki, kwanini sikumpa taarifa mapema? Ila nikamuelewesha kama imekuwa ni dharura na kwa vile ni chakula cha mchana tu haina shida.

Akakubali ki roho upande ila akanihakikishia kwamba chakula kikiwa kidogo usiku yeye hatopika tena chochote kile kwani amechoka. Nikakubaliana na yeye yakaisha, jamaa akaja kula na kuondoka.

Usiku tumekaa mezani tunataka kula wife akaanza kulalama kwamba chakula kimekuwa kidogo na kwa sababu nilileta mtu bila mpangilio. Nikamuambia “wewe kula mimi usiku sipendi chakula kizito so nitakula bites tu”

Bado akawa analalama, nikamuambia hivi mbona nyinyi wanawake huwa mnajali sana kuhusu chakula?

Heee! Kesi ilianza hapo yaani aligoma kula na hadi sasa ninavyosema hajala. Hakulala chumbani na nahisi kampigia mama yake kumpasha uongo kwamba namnyanyasa.

Yaani hivi ninavyokuambia nipo kazini ila hizo sms zinazoingia kwamba sijui nimuache, sijui nikirudi leo yeye sitomkuta na keshanielekeza ambapo nitakuta funguo ya nyumba na maneno kila aina kwa kweli.

Yaani kama kawaida principle yangu mimi huwa sijibu sms za kijinga (nipo tu kimya). Asubuh nilijihudumia kila kitu nikatoka kuja kazini

Sasa najiuliza kosa langu mimi ni lipi hapo?

Yaani najuta, umri huu nilitakiwa nile bata na kutumia ujana wangu vizuri ila daily stress za kipumbavu tu yaani kila siku mtu ananunanuna bila sababu za msingi.

Yaani nimechoka nasubiria nikipigiwa simu na wakwe tu basi natoa talaka direct.

Sent using Jamii Forums mobile app
=====
MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU:

--------------

--------------

--------------

--------------

--------------

--------------

--------------
Hicho ni kichaa cha mimba, onana na watalaamu.
 
Back
Top Bottom