Najuta kuoa hususani katika umri mdogo nilionao

colin_morgan

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
2,443
2,894
Habari wakuu,

Natumai mko na furaha na amani tofauti na mimi. Hapo nyuma nilikuwa nawashangaa sana vijana wengi tu ambao wanaponda sana kitu kuoa. Nilikua nikiwabeza sana na kuhisi kama wamechanganyikiwa hivi kutokana na experience yangu katika ndoa kwani ilikuwa ni maisha mazuri sana na yenye amani mno.

Ila sasa najutaa, nasema tena najutaaaa! Mimi ni kijana wa miaka 28 na ni muajiriwa Serikalini. Pia najishughulisha na uwekezaji katika kilimo so kipato changu ni cha wastani sio kibaya kihivyo. Kisa cha kuleta huu uzi ni mke wangu kuwa na tabia za ajabu za kununa nuna kila siku bila hata ya sababu ya msingi. Akinuna anakaa siku mzima hanisemeshi na kunitumia sms za vitisho na kunishikilia kwamba nimuache ingawa huwa simjibu lolote.

Jana kuna workmate wangu (me) ambaye ni jirani yetu, mke wake amepata dharura kidogo so hayupo. Wakati natoka job nikaona si mbaya kwa vile nilimsikia anataka kwenda hotelini kula nikaona niongee na wife ili aje kupata chakula cha mchana tu home. Tatizo lilianzia hapo. Wife hakuridhika na hilo akaniambia hataki, kwanini sikumpa taarifa mapema? Ila nikamuelewesha kama imekuwa ni dharura na kwa vile ni chakula cha mchana tu haina shida.

Akakubali ki roho upande ila akanihakikishia kwamba chakula kikiwa kidogo usiku yeye hatopika tena chochote kile kwani amechoka. Nikakubaliana na yeye yakaisha, jamaa akaja kula na kuondoka. Usiku tumekaa mezani tunataka kula wife akaanza kulalama kwamba chakula kimekuwa kidogo na kwa sababu nilileta mtu bila mpangilio. Nikamuambia “wewe kula mimi usiku sipendi chakula kizito so nitakula bites tu”

Bado akawa analalama, nikamuambia hivi mbona nyinyi wanawake huwa mnajali sana kuhusu chakula? Heee! Kesi ilianza hapo yaani aligoma kula na hadi sasa ninavyosema hajala. Hakulala chumbani na nahisi kampigia mama yake kumpasha uongo kwamba namnyanyasa. Yaani hivi ninavyokuambia nipo kazini ila hizo sms zinazoingia kwamba sijui nimuache, sijui nikirudi leo yeye sitomkuta na keshanielekeza ambapo nitakuta funguo ya nyumba na maneno kila aina kwa kweli.

Yaani kama kawaida principle yangu mimi huwa sijibu sms za kijinga (nipo tu kimya). Asubuh nilijihudumia kila kitu nikatoka kuja kazini. Sasa najiuliza kosa langu mimi ni lipi hapo? Yaani najuta, umri huu nilitakiwa nile bata na kutumia ujana wangu vizuri ila daily stress za kipumbavu tu yaani kila siku mtu ananunanuna bila sababu za msingi. Yaani nimechoka nasubiria nikipigiwa simu na wakwe tu basi natoa talaka direct.

=====
MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU:

Mambo madogo sana hayo mkuu. Huna haja hata ya kupokea pole.

Communication baina yenu ndio tatizo na pmoja na ww kutosimamia nafas yako vyema. U have to agree in mtters regarding family orientation but whn u think u r not in gud terms, then u have to stand on what u think (n u r sure) is right.
Be bold ( not bull) in ur decisions and stand firm to show ur wife the right path.

Kuish na mwanamke unahitaji akili tu wala sio nguvu. Acha kujitia mawazo kwa mambo unayopaswa kuysimamia na kuhakikisha yanaenda sawa. Dig deep down to what is the root probem.

Kuhusu kukutumia message za kutishia pia mpe shule tu kuwa ni hatari sana kwake yeye mwenyewe.Maana hata lilitokea jambo baya kwako asilohusika yeye, hali itakua mbaya kwake.

Mikosi huwa inasubiri ufungue mlango tu iingie kuwatafuna, sasa ajitahid asiipe nafasi.
--------------
SK2016, Siku zote mke akisema muachana au ataondoka kwao hapo kuna mambo mawili.

1 kwao Ndugu zake wanamjaza kiburi kwamba kama vipi arudi nyumbani.
2 kuna jamaa linamjaza upepo wa kiburi na bila mwanamke kujua kwamba huyo mwanaume anampenda kwakuwa yuko kwa mme wake.
Fanyia kazi hayo Mkuu utapata jibu,

Sent using Jamii Forums mobile app
--------------
Lakini pia Mkuu kuoa mapema sio tatizo kabisa! Tatizo ni aina gani ya mke uliyempata au wewe mwenyewe uko namna gani? Je mlikuwa katika nafasi ya kuoana au mlioana kwa msukumo ya hamu ya mapenzi tu? Je ulioa kwakuwa una kazi utaweza kumhudumia? Hayo yote ni ya kuangalia wapo walioa mapema na wanaishi vizuri tu

Sent using Jamii Forums mobile app
--------------
colin_morgan,
Pole kwa maisha yako ya ndoa unayopitia. Je ndoa yenu ya kanisani? Kama ndivyo sisi wakristo ndoa zetu hazivunjiki kwa sababu nyepesi kama hizo isipokuwa kwa habari ya uasherati Pekee. Nafikiri hata kwa wenzetu bado hizo sababu hazina mashiko kuvunja ndoa.

Umesema una umri mdogo nakuhakikishia ww si mdogo mabubu zetu walioa na kuolewa wadogo mno.
Wanaokushauri naomba upime mno ushauri wao. Wengi hawako kwenye ndoa . Wako wapwekwe mioyoni mwao. Wana uchungu na kuumizwa. Pima kwa makini.

*Kipimo cha akili ya mwanaume ni uwezo wa kukaa na kummudu mkewe.

*usikae kimya mwenzako anapokupa complaints unatakiwa uya -address malalamiko na matatizo yenu. Muite mkalishe chini jadiliana naye. Hiyo ndiyo sifa ya kiongozi. Mwanaume kama kiongozi na kichwa cha familia hajifichi au kukimbia nyumba. Ita mkeo kaeni mezani mkiangaliana na myaongee. Tafadhali tumia skills of goods leadership. Unaweza kumtoa out mkeo nje ya mji mkayamaliza. Waswahili wanaoyajua mapenzi wanasema 'mwanamke hapigwi kwa fimbo bali kwa upande wa khanga '

Mkeo mpe attention. Mjali. Mpende basi umemaliza
*Halafu umeongelea makosa ya mkeo tu. Hujatuambia ya kwako lakini ndugu zako hapa jamvini wametiririka kukuridhisha. Tuambie mapungufu yako. Kumbuka unapomnyooshea mwenzako kidole kimoja vitatu vyote vinarudi kukusonda ww. Makosa yako yapi anayoyavumilia.je ni kwenye kumshirikisha? Je ni kwenye mawasiliano? Wapo wanaojua kubembeleza wanawake wao. Je ulishawahi kubembeleza mwenzako, kumletea zawadi ?
*Usijihesabie haki kwanza kwamba ww ni bora kuliko yeye. Analyse fairly without bias

Mwisho usitafute ushauri wa ndoa humu ndani nenda kawaone viongozi wenu wa dini haraka sana.
Mungu awasaidie mno mno. Hali si nzuri kama unavyoweza kudhani. Na hakuna baraka katika kuachana. Neno kuachana na lisiwepo katika midomo yenu.

Amina
--------------
Pole sana mkuu. Pia usijutie kuoa mkuu wangu. ila mkeo anahitaji jambo moja tu ambalo litakuwa LECTURE kwake katika maisha.

Kama hautojali fanya hivi. Mchukue mpeleke kwao kwanza akae kwa mama yake muda wa kutosha halafu wewe fanya mambo yako kimya kimya na usije mtafuta hata siku moja kwa simu labda akutafute yeye na akikutafuta husifanyenaen mazungumzo mengi , salamu tu basi . No msaada wowote ule .. From there atanyooka tu . hii haimaanishi mnaaachana bali mpumzishe kwako kwanza. aone ugumu wa kuishi nyumbani kwao na ugumu wa kuishi kwake upi ni mwepesi
--------------
colin_morgan,

Mtu mwenye visa ni vyema kuendelea kumu-ignore, muda utamueleza vizuri. Ingawa kama una mpunga wa kutosha na yeye ungempa stress za kifedha akili imkae sawa.

Akinuna weekend unakwenda zako Mombasa kula raha, wikiendi inayokuja unakwenda Mikumi alone.

Asipokupenda wewe apende hela zako na kuzionea wivu. Wakati mwingine kinachofanya hawa wanawake wawe na dharau ni kujua vipato vya waume zao kuwa ni vya kawaida (kati) ambacho kinalingana na chake au amekizidi, hivyo hakuna cha kumbabaisha nacho.
--------------
Mimi kwa uzoefu wangu naisi mkeo humkanyi anapokosea hutoi ile sauti ya kiume ndani ya nyumba mtu siyo lazima umpige kuna adhabu nyingi sana alivyokujibu kuwa hawezi kupika tena usingekula nyumbani na ungerudi ata kesho yake au usiku menen usiogope kununiwa ndani ya nyumba ayo ni maamuzi yake ukimuendekeza atakuwa anajinunisha kila Mara mimi wangu na mwambiaga ukinuna hutaniona apa ndani na nikijua unachepuka Mimi sina sura ya remi ongala fasta tu naopoa mwingine maisha yanaenda sijazaliwa na wewe Mimi

Sent using Jamii Forums mobile app
--------------
colin_morgan,
1. Mkeo bado mtoto, mvumilie na mwelekeze taratibu bila kuchoka.
2. Wakati unamuelekeza atakua anakuletea dharau, ipime dharau na ukiona imezidi mbutue kisawasawa but usimtoe damu.
3. Ukishampiga ujue itakua ni balaa, tulia, muache afanye atakacho na usimuombe msamaha mapema, ikipita wiki then kua karibu nae tena, usichoke maana atakua amenuna but badae mlete karibu zaidi, mbembeleze then muombe msamaha kua ni hasira tu, na mweleze kua ulimpiga kwasabb alikudharau sana kama mumewe.
4. Humpigi mashine vizuri akaridhika, hakikiasha anapata raha na ujue namna ya kumridhisha mkeo.
5. Endelea kumwelekeza namna ya kuwasiliana vizuri, usimpige tena! But piga mashine aisee!
 
Mambo madogo sana hayo mkuu. Huna haja hata ya kupokea pole.

Communication baina yenu ndio tatizo na pmoja na ww kutosimamia nafas yako vyema. U have to agree in mtters regarding family orientation but whn u think u r not in gud terms, then u have to stand on what u think (n u r sure) is right.
Be bold ( not bull) in ur decisions and stand firm to show ur wife the right path.

Kuish na mwanamke unahitaji akili tu wala sio nguvu. Acha kujitia mawazo kwa mambo unayopaswa kuysimamia na kuhakikisha yanaenda sawa. Dig deep down to what is the root probem.

Kuhusu kukutumia message za kutishia pia mpe shule tu kuwa ni hatari sana kwake yeye mwenyewe.Maana hata lilitokea jambo baya kwako asilohusika yeye, hali itakua mbaya kwake.

Mikosi huwa inasubiri ufungue mlango tu iingie kuwatafuna, sasa ajitahid asiipe nafasi.
 

Similar Discussions

81 Reactions
Reply
Back
Top Bottom