Najuta kuoa hususani katika umri mdogo nilionao

Najuta kuoa hususani katika umri mdogo nilionao

SK2016, Siku zote mke akisema muachana au ataondoka kwao hapo kuna mambo mawili.

1 kwao Ndugu zake wanamjaza kiburi kwamba kama vipi arudi nyumbani.
2 kuna jamaa linamjaza upepo wa kiburi na bila mwanamke kujua kwamba huyo mwanaume anampenda kwakuwa yuko kwa mme wake.
Fanyia kazi hayo Mkuu utapata jibu,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini pia Mkuu kuoa mapema sio tatizo kabisa! Tatizo ni aina gani ya mke uliyempata au wewe mwenyewe uko namna gani? Je mlikuwa katika nafasi ya kuoana au mlioana kwa msukumo ya hamu ya mapenzi tu? Je ulioa kwakuwa una kazi utaweza kumhudumia? Hayo yote ni ya kuangalia wapo walioa mapema na wanaishi vizuri tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nahis hii ni point , cause umri wake ni 24

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndoa nyingi za sasa changamoto kubwa ni hiyo..Mazingira yanachangia kwa asilimia kubwa. Ukitaka kuthibitisha hilo jaribu kumchukua ndugu yako wa kike mwenye umri chini ya 25 ishi naye kwa ukaribu na usisite kumkanya kila anapokosea...Kuna vijitabia utaviona kwake.Wewe ni kaka kwa mumewe je?
 
Hapa yako mawili: moja: huyo mwanamke ulimtoa wapi? Ulipata muda wa kukaa naye katika uchumba au urafiki angalau mwaka? Wewe unaenda unaingia kichwakichwa bila kumjua hata kujua malezi yake eti unaoa? Pambana na hali yako! Vijana mmeishaambiwa kwa vile hamtaki kutafutiwa wake wa kuoa na wazazi wenu (kama zamani) basi mkijichagulia kuwa na muda wa kujihakikishia huyo unayeoa atakufaa? Mke/mme akizingua inatesa sana maana mmeishaungana kiroho na kinafsi lazima uteseke. Chakukushauri inaonekana wewe umekaa kizembekizembe! Mke akikuletea nyodo unampa kisago kimoja cha nguvu! Au kama huwezi fukuza aende kwao na ingiza mchepuko ili akili zimkae vizuri
 
Back
Top Bottom