Najuta kumpa ndugu yangu PS (playstation), kawa kama Teja

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
Kawa kama zombi

Niliwahi kununua playstation Kwa mwanafunzi flan hivi wa chuoni alikuwa anadaiwa ada na hana pesa, aliniuzia hio mashine Kwa laki 3 na nusu, lengo langu lilikuwa niiuze hata kwa laki 5 maana hii mashine inauzwa takribani laki 8 madukani, kazi zilinitinga nikawa nimeiweka tu sebleni.

Sasa Kuna ndugu yangu huyu kamaliza form 4 mwaka jana anaenda kuanza chuo mwezi huu alikuja kunisalimia mwezi wa 7 hivi, aliiona hio ps na akaanza kuitumia, ilibidi akae siku 4 lakini game lilimnogea alikaa wiki, anavyoondoka aliniomba sana nimpe mashine, nikampa ila nikamwambia aitunze atairudisha akienda chuo.

Mwezi uliopita nimepigiwa simu na mama yake analalamika nimemuharibu mtoto wake, muda mwingi anacheza ps, kulala saa Saba usiku, kapoteza umakini na kawa kama Teja.

Ilibidi mama yake amnyang'anye hio ps kaifungia sehemu anayoijua yeye kaniambia siku nikiihitaji atanisafirishia.

Baada ya kufungiwa hio ps dogo akaanza kwenda kucheza kwa rafiki zake wenye ps, muda ambao marafiki zake hawapo kaanza kwenda kwenye frem za mtaani wanazochezesha ps kwa hela.

Sasa huku kwenye frem wanazochezesha ps huwa wanalipia pesa kwahiyo dogo kaanza kuiba Hela nyumbani Ili aende kucheza, kukiwa hakuna pesa anaweza kuuza vitu vidogo vidogo, baba yake alipogundua alimtembezea kipigo cha haja lakini bado hasikii.
 
I have been there, namna nzuri ni kumuachia acheze mpaka hamu imuishe.

Akimaliza hapo yeye mwenyewe ataona ni kitu cha kawaida.

Inahitaji kumvumilia kweli.

Mimi nilikuwa nakesha na sio utani yaani kuanzia asubuhi mpaka asubuhi tena (hii ni literally na sio figuratively)

Ila sasa hivi ninaitazama hapa hata wiki inapita sijacheza game
 
Kuna madogo hapa nyumbani walinidanganya walisema anko tununulie PS tunaweka CD za masomo and bla bla pia Kuna games za hesabu na nini kumbe Yananipiga kamba Sasa na uzee huu nikazama mfukoni wakaenda kununua aisee kila siku yanalala saa Saba ukipita karibu na chumba Chao unasikia tu Mara Ronaldo with the ball..nampango wa kuichukua kuifungia chumbani
 
Kwani haya magame yana raha gani juzi nimeona graduate mmoja katika zawadi alipewa option mbilii achague kati ya iPhone 14 na ps5 aka chagua game dadeki
Mkuu ni freemason na agenda zao za siri. Walianzisha haya magemu kimaksudi tu. Haya ma whatsapp TikTok, fb, tinder l, mastercard, visa, visa electron, fifa, worldcup, epl, dstv, KFC, McDonald's, Netflix, western union etc ni wao. Yani freemason wanavuruga sana akili za madogo. Haya magemu ya ps Smart911 anayajulia sana.
 
Mkku ni freemason na agenda zao za siri. Walianzisha haya magenu kimaksudi tu. Haya whatsapp TikTok fb tinder mastercard visa vis electron, fifa, worldcup, epl, dstv, KFC, McDonald's, Netflix, western union etc ni wao. Yani freemason wanavuruga sana akili za madogo. Hata magemu ya ps Smart911 anayajulia sana.
Aiseeee
 
Kuna madogo hapa nyumbani walinidanganya walisema anko tununulie PS tunaweka CD za masomo and bla bla pia Kuna games za hesabu na nini kumbe Yananipiga kamba Sasa na uzee huu nikazama mfukoni wakaenda kununua aisee kila siku yanalala saa Saba ukipita karibu na chumba Chao unasikia tu Mara Ronaldo with the ball..nampango wa kuichukua kuifungia chumbani
Hio mashine uwe unawaachia weekend tu hasa kama bado wanasoma, ikiwakolea inajenga uraibu mkubwa sana,
 
I have been there, namna nzuri ni kumuachia acheze mpaka hamu imuishe.

Akimaliza hapo yeye mwenyewe ataona ni kitu cha kawaida.

Inahitaji kumvumilia kweli.

Mimi nilikuwa nakesha na sio utani yaani kuanzia asubuhi mpaka asubuhi tena (hii ni literally na sio figuratively)

Ila sasa hivi ninaitazama hapa hata wiki inapita sijacheza game
Akiachiwa acheze Hadi imkinai hapo inategemeana na mtu Sasa, wengine Hadi iwakinai ni Baada ya miaka mingi.

Hili tatizo nimejaribu ku google linaitwa gaming addiction, ni tatizo kubwa sana hili.

Nadhani inabidi dogo apelekwe bush huko hakuna hata UMEME akae miezi 6 hivi
 
Back
Top Bottom