Najuta Kumkwaza mke wangu

Saguda47

JF-Expert Member
May 1, 2016
10,766
18,620
Ndugu zanguni Assalam!

Natumai mu-wazima wapendwa wengi wetu mkisherehekea pasaka.

Iko hivi, imetokea tatizo kati yangu na mke wangu. Kiukweli nikiri kuwa mimi ndio chanzo cha tatizo. Jana tulipishana kidogo kauli nikatoa matamshi yasiyofaa dhidi yake!! Kiukweli nilipomwambia hizo kauli alianza kulia na kulalamika kuwa simpendi japo alinivumilia sana hasa kipindi nikiwa na hali mbovu kimaisha. Nilipoyasikia hayo nikaingiwa na huzuni na huruma kubwa, nilimbembeleza jana nikadhani yameisha!

Asubuhi tena kaanza kulia, yaani nimebembeleza sana!! Ndio saivi naona katulia na kunielewa. Ukweli niseme huyu mwanamke nampenda sana na najivunia yeye kwa mchango mkubwa maishani mwangu. Toka tuoane naye sijaona tatizo la kunikwaza kihivyo. Ananipenda na ananishauri mazuri na ninafanikiwa.

Najuta sana jamani, tuwapende wake zetu. Muda mwingine sisi ndio wasababishi wa migogoro kwenye ndoa zetu. Aisee nimejifunza nitampenda zaidi na zaidi mke wangu huyu.

Pasaka njema!!
 
Hata mimi nikimkosea mke wangu kisha akalia huwa ananipa shida sana ila hajui jinsi ninavyoumiaga(na hili sitamwambia maana anaweza akaitumia hii vibaya).
Binadamu kukoseana ni kawaida,kujua kuwa umekosa ukakiri na kuomba msamaha ni jambo jema sana.
Niwatakie maisha mazuri na pasaka njema pia.
 
Bora kula chapati iliyoungua ukimaliza kula utasahau kuliko kutamkiwa maneno makali ya kuunguza moyo hua ni ngumu kusahau...tuwe makini na kauli zetu...BTW hongera kW kutambua kosa na kulijutia huo ni uungwana...pasaka njema wana jf
 
Amin/ Amina
 
Mkuu tulipishana kauli nikajibu kwa jazba kuwa "..usiniletee ujinga we Malaya.." Ndo nikaharibu kabisa yaani, ubabe haufai mkuu
Mkuu bora ungempga kuliko kutukana ni,...."Malaya "

Nakuhakikishia hilo tusi ataliweka moyoni kwa miaka mingi sana

Tena ukute kuna kijamaa huwa kinamtongoza anakataa kwa kusema, ameolewa, usishangae anabadili mawazo maana maneno hujenga na wewe mtu aliyekuamini na kujivunia ukamtukana Malaya

Ngoja akathibitishe huo umalaya si ushatunuku beji ya umalaya
 
Bora kula chapati iliyoungua ukimaliza kula utasahau kuliko kutamkiwa maneno makali ya kuunguza moyo hua ni ngumu kusahau...tuwe makini na kauli zetu...BTW hongera kW kutambua kosa na kulijutia huo ni uungwana...pasaka njema wana jf
Dahhh!! Mke wangu hanaga makuu ni mtu wa maono ya mbali!! Sijui ibilisi gani kanivagaa
 
Mkuu bora ungempga kuliko kutukana ni,...."Malaya "

Nakuhakikishia hilo tusi ataliweka moyoni kwa miaka mingi sana

Tena ukute kuna kijamaa huwa kinamtongoza anakataa kwa kusema, ameolewa, usishangae anabadili mawazo maana maneno hujenga na wewe mtu aliyekuamini na kujivunia ukamtukana Malaya

Ngoja akathibitishe huo umalaya si ushatunuku beji ya umalaya
Isiwe hivyo naomba
 
Back
Top Bottom