Najitoa... CHADEMA Najiunga... CCM

Najitoa... CHADEMA Najiunga... CCM

Sijaona hoja kuu ya kunifanya nijiunge CCM, hizi kamata mwizi kamata mwizi sioni kama zinaweza kunishawishi....

Bado naiona CCM ni ile ile....
 
Mimi huwa chadema wakizingua nawapa za uso.

CCM wakizingua nawapa pia za uso, ila kwa sasa kipaumbele ni kuikosoa CCM na kuishauri CCM. CCM ndio wenye dola, ndio watawala, ndio wakusanya kodi, ndio wapanga bajeti, ndio wenye wabunge wengi.. Nikiwa kama mwananchi wa kawaida kazi yangu namba moja ni kuikosoa CCM na kuishauri lakini si kuisifia na kuipigia makofi...

Kazi ya CCM kama watawala wenye dola ni kuhakikisha maendeleo yanapatikana tanzania, kuhakikisha tanzania haina umasikini na watu wake wanaishi kwa furaha... Hizi vurumai zote zinazoendelea zinaletwa na umasikini & maradhi..

Malalamiko ya watanzania toka uhuru bado ni yale yale tu, umasikini, maradhi,uongozi bora, miundombinu mibovu, ukosefu wa umeme imara, elimu duni, toka 1961 vinavyolalamikiwa ni hivyo mpaka leo 2017 malalamiko ni hayohayo, jibu ni CCM kushindwa kutimiza wajibu wake toka 1961..

Tuache ukada na unafiki, tuuvae uzalendo sote ni watanzania, maendeleo ya Tanzania ndio maendeleo ya watanzania, tusiwe mashabiki wa vyama baadala yake tutumie akili kupima.. Fikiri mara mbili kiwango cha umasikini ni kikubwa..
 
Una maana gani ? Chadema hakuna BUKU 7 FC , Japo tunatambua kwamba kwamba ccm inagharamia vijana wake mitandaoni , ninazo taarifa kwamba wewe binafsi sherehe yako ya kuzaliwa uliyoifanya hivi karibuni iligharamiwa na CCM .
Ha ha haaa! Aisee kumbe ni kweli ninyi mnatunga uongo. Duh ! Kumbe rais mstaafu Dr. Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa sahihi kusema kuna viwanda vya uongo nchini. Yaani kama kweli kambi yenu inahitaji ku-retain idadi ya wawakilishi come 2020; Nilazima wapanga mikakati kwenye maskani zenu mchujane. Yaani mnajenga hoja kwenye uongo tena usio na mashiko!? Ili nikosa kubwa sana kwenye mikakati ya kupata kuungwa mkono hasa mnapofanya makosa kama haya kwenye sehemu ambapo watu makini wanapita.

Kwa staili hii ya uendeshaji shughuli zenu za kuungwa mkono, sasa nina uhakika kwa kiasi kikubwa. Atakayesimamishwa dhidi yenu 2020 atapata zaidi ya milioni 17 za kura kumbuka inakadiriwa karibu ya watu 25 mil watajiandikisha kwenye uchaguzi huo.
 
Huu ni ulimbukeni kama ulimbukeni mwingine tu, hukuwa na haja ya kuutangazia umma maana wakati ulipoamua kuwa na msimamo wa awali hukutueleza hapa!

Pili ni ujinga wa haja kuwa upande wa kukosoa upande fulani kisa tu umeamua kuwa mkosoaji, kwani ukiamua kuwa mzalendo ukawa unakosoa pande zozote ambazo unaona haziendi sawa unapungukiwa nini?
Mkuu wala sio ujinga, binadamu tumeumbwa kuwa na mawazo tofauti, la msingi kila mmoja aamue kipi kinaendana nae. Hivyo kutakuwa na upande A, wapinzani wao upande B, na wale ambao wako neutral upande C. Bahati mbaya kusoma michango ya A na B unatakiwa uwe muangalifu kwani wengi wao wanaongeza chumvi au sukari. Kwenye A na B ndiyo kunakuwa na michango kadha ya ajabu sana-mtu haangalii kilichosemwa ni kipi bali nani amesema.
 
Babeli mimi najulikana na kama kuishi kwa kutegemea mitandao basi ningeshakufa kitambo. Hivi kati ya Babeli na Allen Kilewella nani akitafutwa atapatikana kirahisi. Mimi ni machinga na ukija hapa Iringa wala hupati shida kunipata. Wewe babeli unapatikanaje?
Kupatikana kufanyaje
 
Back
Top Bottom