Najikuta nina stress kupindukia

Pole sana, yani hata mimi soon nitaomba ushauri maana nishaanza kuwa na stress kwasasa ndio maana sahv nishaanza kuwa naingia sanaa humu JF ili kupoteza tu mawazo maana nishaona hali tata sasa.
 
Never loose hope always! Anza upya kumbuka mazuri uliyofanya jipange upya ,soma vitabu ,endelea kutafuta fursa,fanya mambo yanayokupa furaha na usikumbuke machungu o kutafuta wa kulaume. Have free mind dude.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Time heals all wounds ..
Waliosema huo usemi hawajakosea..
Mimi nimewahi pitia hiyo leo ukiniambia nikwambie kilichokuwa kinanisumbua hata sikikumbuki ..imagine that..
Itapita miaka utasahau hata nini kilikuwa kinakupa stress...

Shida zingine tunapitia ili tuweze kuthamini hata kidogo tunachokipata...

Huwezi thamini kuwa na TV kama kila siku unaayo..au kulala nyumba haivuji kama hujawahi ona watu wamehama nyumba mvua ikinyesha
Dah!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Stress full stress kwasasa yan nyie acheni tu ndugu zanguni ngoja ninyamaze tu tuongeze bidii,
Pole sanaaa ,yan hata mimi soon nitaomba ushauri maana nishaanza kuwa na stress kwasasa ndio maana sahv nishaanza kuwa naingia sanaa humu jf ili kupoteza tu mawazo maana nishaona hali tata sasa.
 
Doh, ina maana unskosa amani pasi na kuwepo na chanzo chochote cha moja kwa moja?
Hapo ni shida sasa.
Ila unaposhikwa na hisia za kuchoka maisha ni lazima kuna kitu kibaya au cha kuumiza unachodhani utakiepuka wewe ukiondoka, ni kipi hicho? Kuanzia hapo watu wanaweza kupata pa kuanzia.
Nimejikuta na hali hiyo kaka angu, hata watu huwa wananiuliza nawambia hakuna chanzo, basi wengine hudai huenda nimerogwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi kesi zimekuwa nyingi sana esee....sijui tatizo ni nini.
Pole mkuu.
Nini hasa tatizo?
We unafikiri nchi ikiongozwa na mwehu watu watakosa kusononeka?

Hata subconsciously tu uongozi wa nchi unachangia watu kusononeka.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Nimesoma nilipofika pale “hata kazini” nikajisemea kumbe anakazi sasahivi nipo YouTube naangalia JeJe JeJeJe JeJe oooh nononooo

Portfolio | 2020
 
Pole sana, hutokea hasa unapopitia jambo fulani gumu, nakushauri fanya yafuatayo.

1. Mtumaini Mungu hata kama kuomba inakuwa ngumu ila kiri ushindi
2. Jipe moyo kuwa utayashinda.
3. Omba ushauri kwa mtu au watu unao waamini watatunza siri.
4. Jitahidi kusamehe au kuachilia jambo ambalo liliwahi kukuumiza moyo.
5. Changamana na marafiki ili u refresh.
6. Jitahidi kupunguza kufikiria sana " overthink"

Nakuombea Mungu akupe amani moyoni na furaha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimejikuta na hali hiyo kaka angu,hata watu huwa wananiuliza nawambia hakuna chanzo,basi wengine hudai huenda nimerogwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Doh, hapo kwenye kurogwa wala usipatilie maanani sana kwa sasa kwa sababu mambo ya mfumo wa afya ya akili una mambo mengi mno na linaweza kuwa ni tatizo ambalo linatatulika kwa kupata mtu akakushauri au hivi umetoa dukuduku lako humu ukajikuta baada ya muda unakaa sawa.

Binafsi naweza kusema kuwa kuna kitu hakiko sawa katika mzunguko wa maisha yako, unaweza ukawa unasema hukijui kwa sababu unakichukulia kama hali ya kawaida kumbe kinakula ndani kwa ndani na matokeo unayoyaona ndo kama hayo. Jaribu kuupitia mzunguko wako wote wa maisha yako kama, watu unaoambatana nao, sehemu unazopenda kutembelea, vitu gani unavifanya ukiwa peke yako nk nk.
 
We unafikiri nchi ikiongozwa na mwehu watu watakosa kusononeka?

Hata subconsciously tu uongozi wa nchi unachangia watu kusononeka.

Sent from my typewriter using Tapatalk
Hali ni mbaya kwa kweli, watu wangu wa karibu wengi wanalalmika na unaweza kuona kuwa wanaisha kwa ndani kdri siku zinavyokwenda. Sijui tutavuka hapa ama vipi.
 
Kila mtu huwa na stress kipindi fulani lkn jinsi ya kuondoa huwa tunatofautiana. Miye nikiona yamenijaa huwa naenda zangu beach,au club toka asbh mpk jioni, huko jioni huwa nafarijika Sana.

Ngoja nikupe kisa kimoja nilipomaliza shule wazazi wangu walisimamishwa kazi kwa kupisha mwezi mmoja loohh.

Taarifa ya bi mkubwa niliipata nikiwa Dar, Basi nikaenda beach maana niliona dunia imenielemea Sana, kufika kule asbh nimekaa kwenye kibanda nawaza hili na lile Mara pembeni yangu namuona mshikaji anafuta machozi. Nikamwita njoo mbona hivyo akasema wazazi wamefariki na baba yao mdogo ameuza anauza Mali za familia, na yeye anatakiwa aende chuo na ada hamna.

Duuuh niliona yangu madogo sbb wazazi wangu walikuwepo. Tulipiga stori na tukawa washikajiii.
 
Nimesoma nilipofika pale “hata kazini” nikajisemea kumbe anakazi sasahivi nipo YouTube naangalia JeJe JeJeJe JeJe oooh nononooo

Portfolio | 2020
😁😁😁😁 dah we jamaa umefanya siku yangu iishe vizuri, nimecheka kisenge tho ninamastress kinoma.
 
Back
Top Bottom