Nina stress sana huenda nimeathirika

RoadLofa

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
1,344
2,948
Yapata miezi 3 sasa tangu nipate matibabu ya U.T.I sugu ambayo ilifikia kiasi cha kutoa usaha wa ute ute mweupe nikikojoa, matibabu ambayo ilikuwa ni sindano na dose mbili za Metradazolone, Ciprofloxacin nk ambazo zilinisaidia sana hadi kupona.

Sema tatizo naona limeisha sema bado kuna maumivu kwa mbali huwa nayasikia kwa mbali chini ya kitovu maeneo ya kibofu ila muda mwingine yanapotea kabisa, pia nisipokunywa maji kama maumivu yanarudi.

Kiukweli U.T.I sugu usiombe ikupate inatesa sana na kuisha kama kuna muda inapotea na kuna muda inarudi, sasa wasiwasi wangu ni kwamba kama niliweza kuambukizwa U.T.I sugu je sijaambukizwa kweli H.I.V maana natamani kweli nikapime ila nina wasiwasi kweli, na nina stress muda wote najiona kama tayari nimeathirika tayari maana nikijiangalia baadhi ya dalili kama naziona kama kuchoka bila sababu, kuumwa kichwa mara kwa mara, sasa sijui kama hizo ni dalili direct au ndo kama wanavyosema magonjwa mengine huanzia kwenye psychology.

NAOMBENI USHAURI ILI NIPUNGUZE IZI STRESS ZISIJE NIPELEKA KWENYE DEPRESSION
 
Jiwekee imani hata kama itatokea una ngoma basi jipe tumaini kuwa imeshatokea na maisha lazima yasonge mbele fanya zoezi hilo kwa siku kadhaa au miezi ukiwa tayari nenda kapime kwa sbb mwili wako utakuwa tayari kwa majibu yeyote yale

Hali kama yko iliwahi kunitokea kiukweli muda wote nilikuwa na mawazo yasiyoisha baadae nilijitengea muda wa kujitafakari kwa kina kisha nilikuja kuamua maamuzi hayo kuwa lolote na liwe hata kama litakuwa gumu kiasi gani maana sitaweza kubadilisha hali ambayo itakuwa imejili katika maisha yangu.

Yote hayo yalitokana na mwenzi wangu alikuwa kicheche wa kufa mtu rafiki zangu walikuwa wanajua shemeji yao ni malaya na licha ya kutembea na watu kibao lkn kati ya hao alikuwa anatembea nao alikuwa na ngoma na ametembea na mke wangu mara nyingi tu kwa hiyo moja kwa moja hata mimi nitakuwa muathirika kwa hiyo walikuwa wanashindwa hata kunieleza wanaanzaje

Mwisho wa siku na mimi tetesi zilianza kunifikia kutoka kwa watu wengine kabisa kuwa nina ngoma kwa kuwa mke wng anatembea na mtu mwenye vvu ,mwanzoni niliteseka sana kuwa nitakufa siku za karibuni tu lkn nilijikaza na kuenda kupima baada ya miezi kadhaa

Sikuamini majibu kuwa ni negative nilikwenda hospitali nyingi tofauti tofauti na kwa vipindi tofauti lkn bado majibu yalikuwa negative tukio hilo lilinitokea mwaka 2013 na hadi leo nadunda tu na huyo mwenzi wng hadi leo hii ni muathirika na walikuja kuoana kabisa na huyo jamaa

Hivyo ndugu nakutia moyo usijipe mawazo yasiyo na majibu kama jambo litakuwa hvo shukuru Mungu pia kama litakuwa kinyume chake pia Mshukuru Mungu kwani kuwa na H.I.V siyo mwisho wa maisha na hao niliowazungumzia hadi leo ni wazima na wanaendelea na maisha kama kawaida

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Dawa ni Azithromycin aseee!! Kanunue vile vidonge vitatu utakuja kushukuru hapa baadae
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom