Naisikia Singida United tu Lipuli na Njombe Mji mpo wapi?

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,671
Timu tatu zimefanikiwa kupanda ligi kuu msimu huu Singida united,Lipuli na Njimbe mji ila katika maandalizi naisikia Singida united tu hawa wengine wapo wapi sijui.

Singida United wanaonyesha wanataka kuwa kama Leicester city ya Bongo wako seriazi sana na maandalizi yao nawapa nafasi ya kushika nafasi 3 za juu ligi ijayo,Nimesoma wanataka kuweka kambi yao Oman kwa ajili ya maandalizi yao.

Wanakocha mzuri,wamesajili Wazimbabwe 3 naimani watakua njema na pia wameanza mazoezi mapema sana.

Angalizo Njombe Mji na Lipuli msije kurudi mlikotoka mkatuaibisha wanaKusini tena fanyeni usajili mzuri na pia muanze maandalizi yenu mapema msije kuwa wagawa pointi tuu.
1494001215378.jpg
 
Huwezi kuitenganisha Singida United na Mwigulu Nchemba! So na hizo timu nyingine zinahitaji products kama Mwigulu Nchemba!
 
Hizo zote ni tiamaji tiamaji mwisho wa ligi zitapigana kubaki ligi kuu
 
Singida united si timu ya wanachama. Sgd united ni kampuni,hivyo kuna watu kama Yusuph wameweka mzigo wa kutosha hapo kwenye timu. Lipuli juzi tu hapa walikuwa wanagombania uongozi,sasa unategemea wanaweza fanya kipya. Tatizo la timu za mikoani hujigeuza mawakala wa simba na Yanga. Hizi timu zingejisimamia na kupata udhamini tingeekuza mpira.Hivi timu kama toto inafaida gani hapa Nchini.
 
Kwanza hao sitegemei kuja kufanya maajabu kwani hata kupanda kwao ligi kuu hawajapanda kwa haki,karibia michezo yao mingi waliyocheza hapo Iringa timu nyingi ziliwakatia rufaa,na pia hii timu imepanda kisiasa sana kwani karibia michezo mingi karibia viongozi wa kiserikali walikuwa wanashiriki mfano mdogo Dc kasesela na n.k
 
Back
Top Bottom