Naishukuru serikali ya CCM imenipa ajira

Naishukuru serikali ya CCM imenipa ajira

kazi si lazima kufanya kwa muhindi tu vijana wasomi wanaweza kujiunga nchi hii ina rasilimali ardhi kubwa wakaitumia kupata mikopo kwenye mabenki. Vijana ambao hawakwenda shule wamejikomboa sana wana bodaboda ,wamejiunga vikoba wanafanya biashara ndogondogo na maisha yanasonga mbele. Tatizo vijana wasomi wanataka mafanikio ya haraka bila kuumiza kichwa mwisho wana baki kuichukia serikali na kuwa na imani upinzani ukishika serikali ajira zitatolewa kama njugu.

umesema vema mkuu,but lets think beyond evening.hicho ndicho wewe na hao wanasiasa wenzako mnataka kutuaminisha.mbona watoto wao hawajiungi na hivyo vikundi vya vikoba?walikuja na sera za kilimo kwanza,wakaleta matrekata,yanakopesheka?huo uwezo wa trekta upo?mbona mnataka tudanganyane?eti ardhi ipo etc etc mbona nyie hamlimi?hivi mnadhani mnaweza kutupumbaza eti kilimo,vijana wajiunge na vikundi etc etc,hivi unadhani maisha ni kupata hela ya kula tu?kwamba isitokee hata siku moja maishani mwangu na mimi niende kula bata kwenye beach za kopa kabana?mnataka mimi ndo nilime ili niendelee kuwa maskini?mbona watoto wenu wengine tumesoma nao,kichwani weupeeee,hata ufaulu wao ulikuwa shida lakini hawaendi kulima wala kujiunga kwenye vikoba?mnadhani sisi ni wa pumbav*kiasi hicho?
 
umesema vema mkuu,but serikali ina wajibu wa kuandaa mazingira ya ajira.ni miaka sasa hatuna ajira mpya,yaani zilizopo ni zile zile,wakati nchi ina rasilimali za kutosha.kwanini zisitumike kupanua wigo wa ajira.tunajua kuwa serikali na secta binafsi haviwezi kuajiri kila mtu but kuna mazingira ambayo yanafanywa ili kutengeneza ajira.imagine,kuna bilions ngapi uswizi?zisingeweza kufufua viwanda hata vitatu?vingetoa ajira kiasi gani kwa vijana?kila kinacholipa kinabinafsishwa kiujanja ujanja

Unajua hatukatai mkuu kwamba nchi ina rasilimali nyingi na mambo mazuri mengi, ila kwa kuwa hela zinapelekwa uswis na serikali haijaonyesha kuandaa mazingira ya ajira kwa kiwango unachokitarajia, je,tukae tu bila kufanya chochote kwa sabau serikali haijafanya kile tunachofikiri sisi inatakiwa kufanya ili kuongeza wigo wa ajira? Amini amini nakwambia kama huwezi kufanya chochote katika haya mazingira, hutaweza kufanya chochote hata kama serikali ingetimiza hayo unayofikiri inapaswa kutafanya ili kuongeza ajira.
 
umenena vema na ukishaelewa kwamba kuna "wengine" na "wewe" chukua hatua. Inamaana inawafanyia hivyo wengine ila wewe ukikaa bila kufanya chochote haitakufanyia hivyo mkuu. Na chunguza vizuri hao unaowaita wengine na madai ya kufanyiwa hivyo na elimu.

tatizo sio hao wengine kuwa hivyo,bali wanafanya hivyo kupitia jasho letu.mfano,leo hii wanapiga serekasi na elimu ya nchi hii ili hali watoto wao hawako kwenye elimu hii,mbaya zaidi baada ya kuiba kodi zetu ndo zinawapeleka watoto wao huko nje.
 
hahaha tena ukikuta wanajisifu utashangaa,eti wametoa ajira kibao kwa vijana

Ajira zaidi ya 3000 zimetolewa kwa vijana kwa kazi ya kuokota chupa za plastiki zilizo tupwa baada ya ktumia vimiminika vilivyo kuwema kama maji juisi na sada serikali yenu sikivu bado inaendelea kutoa ajira kwa vijana KIDUMU CHUKUA CHAKO MAPEMA !
 
unajua hatukatai mkuu kwamba nchi ina rasilimali nyingi na mambo mazuri mengi, ila kwa kuwa hela zinapelekwa uswis na serikali haijaonyesha kuandaa mazingira ya ajira kwa kiwango unachokitarajia, je,tukae tu bila kufanya chochote kwa sabau serikali haijafanya kile tunachofikiri sisi inatakiwa kufanya ili kuongeza wigo wa ajira? Amini amini nakwambia kama huwezi kufanya chochote katika haya mazingira, hutaweza kufanya chochote hata kama serikali ingetimiza hayo unayofikiri inapaswa kutafanya ili kuongeza ajira.

mkuu kwanza hapa naona kama unanikosea mkuu,sio kile tunachofikiri sisi,ila ni wajibu wa serikali.sio kwamba tumekaa tu,hapana tunajitahidi sana but we have limits.mazingira wanayotuwekea yana limits.we can't go beyond where we are.tunabaki kupata vihela vya kujenga kajumba kamoja,tena hadi ukakamilishe ni miaka sita,kununua ka vitz,basi na vijichenji vya kusomesha watoto private zetu hizi.mengine hamna.
 
ajira zaidi ya 3000 zimetolewa kwa vijana kwa kazi ya kuokota chupa za plastiki zilizo tupwa baada ya ktumia vimiminika vilivyo kuwema kama maji juisi na sada serikali yenu sikivu bado inaendelea kutoa ajira kwa vijana kidumu chukua chako mapema !

si unaona mkuu,leo hii graduate nikaokote chupa?what will a layman do?sasa elimu itakuwa ina maana gani?
 
mkuu kwanza hapa naona kama unanikosea mkuu,sio kile tunachofikiri sisi,ila ni wajibu wa serikali.sio kwamba tumekaa tu,hapana tunajitahidi sana but we have limits.mazingira wanayotuwekea yana limits.we can't go beyond where we are.tunabaki kupata vihela vya kujenga kajumba kamoja,tena hadi ukakamilishe ni miaka sita,kununua ka vitz,basi na vijichenji vya kusomesha watoto private zetu hizi.mengine hamna.

Nakubaliana na wewe kabisa , ni wajibu wa serikali. Sasa kama serikali haijafanya utaacha kuchangamkia fursa zinazojitokeza kisa unasubiri serikali itengeneze mazingira? Hata hivyo serikali nyingi duniani zinajaribu kukabiliana na hii changamoto ya ajira na ni tatizo kubwa duniani sasa hivi.

Nakuelewa kabisa mantiki yako ila nnachotaka kusema ni kwamba inabidi tubadilike tunavyolichukulia suala la elimu na ajira, zama zimebadilika! Niwie radhi kama umeona nimekukosea mkuu ila haikua maana yangu na sio dhamira yangu.
 
mkuu,mi ni muajiriwa serikalini but naumia sana kwa hali iliyopo sasa,after 5yrs ndo tunapata waajiriwa wapya 20,imagine
 
"naishukuru serikali ya ccm na hasa mh rais katika hii miaka hamsini na ushehe ya uhuru,nimepata ajira.mimi ni dereva bodaboda"...nilimsikia kijana mwenzangu akiropoka,cjui alikuwa keshapewa buku 7 au ndo yuko brainwashed
Hahahaaaaa mkuu you made my day.. ashapagawa na maisha huyo.
 
"naishukuru serikali ya ccm na hasa mh rais katika hii miaka hamsini na ushehe ya uhuru,nimepata ajira.mimi ni dereva bodaboda"...nilimsikia kijana mwenzangu akiropoka,cjui alikuwa keshapewa buku 7 au ndo yuko brainwashed
Nilijua tu ni dongo
 
Mkuu,

Yaani nisome miaka;
7;primary
4;secondary
2;high school
5;university
Total;18

Halafu nije niendeshe BODABODA?

EXCUSE ME!!!!!!!!!!!!!!!!
Kama ndio hivyo mbona hao wanenu tuliosoma nao wanaajiriwa kwenye makampuni makubwa na kuendesha ma-range wakati walikuwa vilaza tu?

Mie niendeshe BODABODA na yule alomaliza la saba afenyaje sasa?Tunawafundisha nini wale wanafunzi wanaosoma sasa?Kuwa elimu ni ufunguo wa BODABODA!?

MSHINDWE!

mkuu nafikiri utakuwa umesomea law hapo udsm( kutokana na miaka hiyo uliyotaja). ila ki ukweli elimu yako uliyoipata haijakusaidia!
 
Sijui kwa nini hatutaki kukubadiliana na mabadiliko ya mfumo wa maisha, enzi hizo kijijini baba yangu na baba mdogo ndio walikua wamemaliza darasa laba kijiji kizima na zikaja nafasi za ualimu baba akaenda kusoma na kuajiriwa ualimu ikafuatiwa na nafasi za mafunzo ya uaskari baba mdogo nae akaenda chuo cha polisi Moshi, wakiwa huko kwenye mafunzo vita ya Uganda ikaanza wakapelekwa huko na aliporudi nafikiri hapakua na haja ya kuendelea tena na mafunzo kwa sababu alikua amefuzu zaidi ya mafunzo aliyostahili kujifunza chuoni, akaenda moja kwa moja kwenye ajira.

mazingira yetu sasa hivi yako tofauti sana, hata pale unapotaka kusomea fani au ujuzi wa aina flani unajiuliza mara mbilimbili, nje ya ajira hichi nnachotaka kujifunza ntakitumiaje kunisaidia kuingiza kipato na kuendesha mambo yangu? zile enzi za kusoma kisha unakaa unatulia ukisubiri ajira zilikwisha kitambo! Thanks mkuu

thumb up,ukwel ndo huo
 
Ajira ni ngumu sana kwa sasa. LAkini kinachonisikitisha ni kuona ajira ngumu kwa watoto wa maskini tu. Watoto wao hawa walio madarakani hukuti hata siku moja wakisema ajira ni ngumu. KWanini? Wanapewa vyeo na kazi nono huko.Pia wanapewa mitaji kujiendeshea vibiashara vyao.
 
kwani unafikiri nimekwambia uendeshe bodaboda?!!...thubutuu, wewe kaa ukisubiri ajira utaajiriwa tu, watu ni wengi kuliko uwezo wa serikali na mashirika kuajiri kwa hiyo subiri "bahati yako" na usikae unaililia serikali kwa sababu haina nafasi za kutosha. Ukiamua unaweza kuamka, ukajitambua ukajua kwamba wewe ni wewe na maisha ni yako, na mwenye wajibu wa kuyarekebisha ni wewe mwenyewe. Elimu unapewa ili UITUMIE, siyo UITUMIKIE! Mwisho wa siku mimi ni mbwabwajaji tu, maisha yanabaki kuwa yako, yafanyie chochote unachopenda, ukichagua kukaa na cheti cha degree chumbani huku unatupia ugali wa mjomba na kusubiri ajira ni heri na haki! Wapo wenye kujiongeza, waliokaa wakaona ajirangumu wakaazima milioni moja kwa dada wakaanzisha bar chini ya mti, wakawa bar maid na sasa wanahesabu faida laki tano kila siku....wanasubiri ajira bana, watauzaje bar na wao wanamiliki bachelors degree?! Wapo walioamua kufuga nguruwe na sasa wanapiga mruzi,..wanasubiri ajira tu, utafugaje bata kama wa darasa la saba?...wapo walioamua kulima matikiti maji, kubrush viatu vya watu ofisi kwa ofisi, kupika mama ntilie....uwe na ajira usiwe na ajira, uwe na phd uwe na cheti cha darasa la saba mwisho wa siku unatakiwa kusurvive. Ukiamua kupiga siasa kijiweni, fine, ukiamua kuwa wewe na kupigana na maisha, safi pia!
KARIBU DUNIANI.

true braza
 
Mkuu, kiyecno changu hakina kitufe cha "LIKE" la ipokee juu kwa ju walahi!!!!
 
Back
Top Bottom