"naishukuru serikali ya ccm na hasa mh rais katika hii miaka hamsini na ushehe ya uhuru,nimepata ajira.mimi ni dereva bodaboda"...nilimsikia kijana mwenzangu akiropoka,cjui alikuwa keshapewa buku 7 au ndo yuko brainwashed
Haki yako imeshakuwa hisani.
hana sababu ya kushukuru,ajira ni haki yake ya KIMSINGI,labda hajui tu,na serikali yeyote dunian ni lazima ihakikishe watu wake wanakua na ajira,aidha kwa kuwaajiri,au kuwatengenezea mazingira ya wao kujiajiri
Mkuu,
Yaani nisome miaka;
7;primary
4;secondary
2;high school
5;university
Total;18
Halafu nije niendeshe BODABODA?
EXCUSE ME!!!!!!!!!!!!!!!!
Kama ndio hivyo mbona hao wanenu tuliosoma nao wanaajiriwa kwenye makampuni makubwa na kuendesha ma-range wakati walikuwa vilaza tu?
Mie niendeshe BODABODA na yule alomaliza la saba afenyaje sasa?Tunawafundisha nini wale wanafunzi wanaosoma sasa?Kuwa elimu ni ufunguo wa BODABODA!?
MSHINDWE!
Bulldog nami ndo nimeshangaa,watu wanasema tunaishukuru serikali kwa kutujengea barabara,oooh
Ajira zinatangazwa kila kukicha bado mnalalamika hata hivyo serikali haiwezi kuajiri kila mwanafunzi anaemaliza chuo kikuu ndio maana tunasisitizWa kuangalia fursa nyingine katika sekta binafsi.
mbona ndo inavyowafanyia hivyo wengine?kwanini sisi?
sawa mkuu but graduate ukafanye kibarua kiwandani kwa muhindi buku 5 kwa siku,inatosha?
mbona ndo inavyowafanyia hivyo wengine?kwanini sisi?
kazi si lazima kufanya kwa muhindi tu vijana wasomi wanaweza kujiunga nchi hii ina rasilimali ardhi kubwa wakaitumia kupata mikopo kwenye mabenki. vijana ambao hawakwenda shule wamejikomboa sana wana bodaboda ,wamejiunga vikoba wanafanya biashara ndogondogo na maisha yanasonga mbele. tatizo vijana wasomi wanataka mafanikio ya haraka bila kuumiza kichwa mwisho wana baki kuichukia serikali na kuwa na imani upinzAni ukishika serikali ajirA Zitatolewa Kama njugu.
ulishawahi kujiuliza ni vijana wangapi wanahitimu kila mwaka kutoka vyuo vyote nchini? umeshawahi kujiuliza uwezo wa serikali na sekta binafsi ni vijana wangapi kwa mwaka?!! Enzi zile "wasomi" walikuwa wachache, watu walikuwa wakimaliza kidato cha nne na sita ajira zinawafuata waliko, sasa hivi "wasomi" ni wengi, ukingoja ajira utashangaa unazeeka na bahasha ya khaki mkononi!
CYBERTEQ, inaelekea kuna siku watu watataka elimu ishike kijiko ichote cha
ulishawahi kujiuliza ni vijana wangapi wanahitimu kila mwaka kutoka vyuo vyote nchini? Umeshawahi kujiuliza uwezo wa serikali na sekta binafsi ni vijana wangapi kwa mwaka?!! Enzi zile "wasomi" walikuwa wachache, watu walikuwa wakimaliza kidato cha nne na sita ajira zinawafuata waliko, sasa hivi "wasomi" ni wengi, ukingoja ajira utashangaa unazeeka na bahasha ya khaki mkononi!