Naionya China, isijaribu

China Hana mpango wa kuivamia Taiwan kama watu wanavyopenda itokee. Mpango wa China toka mwanzo kuhusu Taiwan ni "peaceful reunification" siyo military operation kama anachokifanya Urusi kule Ukraine. Na watu waache kufananisha mgogoro wa Taiwan na Chima na ule wa Urusi na Ukraine.
 
Iache iporomoke kiuchumi ili isiwe na hela za kuwajaza wachina africa. wamekuwa kero kila mahali africa hawa wachina. halafu lazima walipe hasara ya kuleta siasa za kupeleka vijana vijijini, kukamata wazururaji na kujenga vyuo vya propaganda.
Hahaha hawa jamaa wametapakaa kila mahali hapa Afrika. Na kazi zote wanafanya, iwe kuuza duka, kutembeza mahindi au kubeba mchanga wao wamo.
 
Ya ni kweli mkuu Tsh , pamoja na nguvu ilizonazo USA, lkn haiwezi kupuuza ukweli kwamba Russia sio nchi ya kuifanyia mzaha kwa namna USA inaweza kufanya kwa nchi zingine. Mmarekani anafahamu fika kwamb Russia nae ni miongoni mwa tatu bora za super power ulimwenguni, so lazima aende nae kiakili sana.
 
Sasa hao watu wengi ikawaje wakashindwa jua Pelosi anaenda Taiwan hadi waliposikia kwenye vyombo vya habari, ndo wakaanza mobilization ya vifaa?
Tena mobilization zenyew zimefanyika baada ya Pelosi kutoka tayari ndani ya Taiwan. Watu ambao wanaweza kufanya kile wanachomaanisha na hata marekani inajua kama haiwezi kuwafanyia mzaha kama huu ni Iran na pengine North Korea.
 
Nyie endeleeni kuwajaza upepo wenzenu, ila mwisho wa vita ndo utakuwa wakati mzuri wa Russia kuhesabu hasara zake.
 
Lengo kubwa la Marekani ni China iwe ya Kidemokrasia
China ikiwa ya kidemokrasia basi uongozi mzima wa nchi yao utang'olewa, maana wengi wameshachoshwa na aina ya uongozi wa nchi yao. Ni basi tu hawana mahali pa kuonesha hisia zao, labda wale wanaofanikiwa kutoroka nchi humo.
 
Ila mrusi Hadi Sasa anagharimia vita Kwa Mali za anayepigana nae.
Mkuu vita vya Ukraine na Russia ni kama vile mpira wa miguu. Mmoja anashambulia huku mungine anajifanya kurudi nyuma, wale wanaoshambulia wakianza kuchoka wale wanaoshambuliwa na wao wanaanzisha mashambulizi kuelekea kwa adui. Hivyo hivyo ndo jinsi vita vinaendeshwa.

Kwa mfano sasa hivi Ukraine umeshaanza kushambulia na kurudisha baadhi ya maeneo yaliotekwa na Urusi.

So that's how the way war it going.
 
Ya ni kweli mkuu, kuingia vitani na nchi yenye ushirikiano na marekani ni sawa sawa na kujaribu na ukuta wa nyumba yako mwenyewe. Maana likitokea la kutokea ni wewe mwenyew ndio utakaepata hasara.
Unachek putin anavyohaha na anaona aibu kujitoa alidhani anapambana na Ukraine.
China aliusoma mchezo akaona asimeze ndoano kama Putin.
 
Shukran sana mkuu kwa kumpa makavu huyo puppet wa warusi. Sisi tunaongelea uhalisia yeye analeta mahaba yake kwa nchi anayoipenda yeye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…