Naionya China, isijaribu

Ok mkuu ngoja tusubiri mwisho wa vita ya Ukraine ndo tutajua ni nani atakaekuwa katika maumivu zaidi.
 
Kwanini mkuu.
Kwa sababu alikuwa na uthubutu na maamuzi magumu.hawa wa sasa ni waoga sana tokea utawala wa Deng Xiaoping mpaka Sasa Xi Jinping sijaona mtu mwenye uthubutu Kama Chairman Mao Zedong labda mbeleni watabadilika . Taiwan kurudi China inahitajika maamuzi magumu na uthubutu wa hali ya juu.
 
Unauliza swali kisha unajijibu mwenyewe, vita inafilisi uchumi balaa tupu. Westerners wanapenda bata sana kwenye mataifa yao na kuwaingiza vitani watoto wawatu lazima uwe na sababu za kutosha.
 
Hiyo miaka 5 kuna maghala ya silaha za marekani yatakuwa yameisha maana hata javelin maghala yake ya hapo ulaya yameisha juzi
Marekani ina akiba ya silaha kubwa ambazo kamwe haiwezi kuzitumia katika vita isio yake. Hizo silaha unazoona anazituma kwa Ukraine ni used hazina mantiki yoyote kwa marekani sasa hivi.
 
Nakusoma sana inaonekana unapenda sana sera za ujamaa with Chinese characteristics. But we can't live with a single reality as long as we live in the world with full of diversities. Mao was a ruthless hero.
 

Kwa hyo Sasa hivi Russia analima na kuvuna ngano kwa amani Hilo alikoteka Ukraine bila kusahau anafyatua ma- nuclear weapons Kama mchwa hapo Ukraine πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ dah once ignorant always ignorant!
 
Kutoa maoni sio dhambi usipangie watu cha kuongea kama dampo unaushi wewe kunguni mkubwa. Unafikili Russia wana mili ya chuma, unafikili askari wa Russia wanavyofanya mauji ya watoto roho haziwaumi baada ya vita Kuna wengine watapata uchizi ( postpartum depression ). Awe beberu wala Russia hakuna anaeweza kushinda vita ya uonezi.
 
Nakusoma sana inaonekana unapenda sana sera za ujamaa with Chinese characteristics. But we can't live with a single reality as long as we live in the world with full of diversities. Mao was a ruthless hero.
Mkuu Mimi Kama Mimi napenda ujamaa tena Sana .Ila sihitaji wala sipendi kuona ardhi yetu ya Tanzania inaongozwa na mfumo wa chama kimoja hicho kitu Mimi mwenyewe nipo mstari wa mbele kukipinga kwa kuwa kimekwisha Leta matokeo hasi kwetu kwa zaidi ya miaka 60 CCM imetawala bila maendeleo yoyote kutuletea . Mimi ni muumini wa mfumo wa vyama vitatu vyenye nguvu na mgombea binafsi . Pia sipendi kuona serikali ikilazimisha nchi kuongozwa kwa ujamaa kwa 100% au ubepari kwa 100% Mimi napenda kuona serikali ikichukua Yale yaliyo mazuri kwenye ujamaa na kuyatumia na kuchukua Yale yaliyo mazuri kwenye ubepari na kuyatumia kwa faida ya maendeleo ya nchi. Ndio maana namejipachika mjamaa wa kisasa kwa sababu napenda ujamaa uwe kisasa wenye faida ukubali kukopa na kuungiza mambo yenye faida yaliyo nje ya ujamaa kwa sababu Mimi naamini ujamaa unapaswa kuwa mfumo ulio hai unapaswa kukua na kubadilika kutokana na wakati , mazingira na watu ili ulete faida role model wangu wa ujamaa wa kisasa ni mtaalamu Deng Xiaoping. Ni hayo tu machache mkuuπŸ˜„
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…