Naiomba serikali kuwachunguza wakurugenzi wao namna wanavyowatumia watendaji wa kata na Kijiji kuwaumiza wanannchi

Frustration

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
3,095
4,059
Serikali inajitaihdi sana kutoa mafungu mbalimbali ya fedha kwa ajiri ya maendeleo vijijini. Bahati mbaya zile hela mara nyingi vijiji huingiziwa na serikali bila ya kutoa muongozo wa matumizi. Serikali inaamini vijiji vina matatizo mengi, nikweli vijiji wanahitaji fedha nyingi kukamilisha miradi mbalimbali.

Kuna ujenzi wa vyoo vya shule, ofisi, majengo ya serikali, ukarabati wa vyumba chakavu, hospitali n.k. Mara nyingi vijiji huingiziwa milioni 50 karibia kila mwaka ili kufanya ukamilifu na uboreshaji wa baadhi ya vyumba au yovyote vile kijiji kitaona inafaa ilimladi tu matumizi yosomeke ya muhimu.

MILIONI 50 ANAANZA KUIMEGA MKURUGENZI MTENDAJI WA WILAYA.

Sijajua hadi mda huu mshahara wa Mkurugenzi ni shilingi ngapi. Wakurugenzi wa wilaya Tanzania ndio chanzo cha uovu,ubovu au uzuri wote wa Watendaji wa Kata na vijiji kwote nchini. Mkurugenzi ndie Mungu mtu wa Watendaji kwa kuwa wao wanamwakilisha yeye hivyo anawatumia kwa masilai yake binafsi.

Na kubali kuna watendaji wanatabia ya kujiongeza wao kama wao,ila maeneo mengi wanatumiwa na Wakurugenzi.
Uuzwaji holela wa mashamba ya vijiji pia una baraka ya wakurugenzi. Tuwaonee huruma hawa watendaji kwa kweli wanapitia magumu mengi sana na kutokana na matendo yao hata jamii mda mwingi inawatenga.

Wakurugenzi wanawatumia watendaji kupata hela ya vocha na bia. Hii inapelekea watendaji kuwakamua wananchi bila huruma, na ofisi ya mtendaji imekuwa kama TRA.

Pesa ya serikali ikitoka tu kabla kijiji hakijaingiziwa Mkurugenzi atawaita mwenye kiti, watendaji wake wote kwa maana ya mtendaji wa kata na kijiji husika na diwani wake. Agenda 1 tu iliyojificha nyuma ya panzia namna ya kuila hela ya moto.

Wanambinu nyingi mfano watumie ushawishi wao kulazimisha hela ipelekwe kwenye matumizi fulani. Huko utakuta tu sasa ghafla simenti ya jengo la hospitali inatinduliwa na kuwekwa mpya tena yenye rangi nyekundu, na nje wamenunua tenk la maji. Hadi kufikia hapo hela imeisha.

Naiomba serikali kuwachunguza wakurugenzi wao namna wanavyowatumia watendaji wa kata na Kijiji kuwaumiza wanannchi, na kurudisha nyuma maendeleo ya vijiji na rushwa zilizopo.
 
Back
Top Bottom