Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,036
Aliyekuwa Waziri wa Ujenzi na ambaye aliwahi kukabiliwa na kesi ya rushwa Bw. Nalaila Kiula ameibuka leo na kumshangaa Waziri Mstaafu Bw. Joseph Warioba kwa kitendo cha ukosoaji wake wa kamati Teule ya Dr. Harrison Mwakyembe.
mambo mbalimbali yanayohusiana na matukio ya kisiasa nchini. Bw. Kiula amemshangaa aliyekuwa Waziri Mkuu Bw. Joseph Sinde Warioba kwa kitendo chake cha kushangaa kwanini kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Dr. Harrison Mwakyembe hakumuita Waziri Mkuu aliyejiuzulu Bw. Lowassa kufuatia suala la Richmond.
Bw. Kiula amesema kuwa Warioba siyo mtu wa kuzungumzia suala la "natural justice" kwani ni yeye katika wakati wake aliyeongoza tuhuma za rushwa dhidi ya Kiula na hakuna wakati wowote ambapo yeye Warioba alimuita Kiula kumuuliza juu ya tuhuma mbalimbali (zilizotajwa kwenye ripoti ya Warioba) na hatimaye kumuacha apoteze nafasi yake na hatimaye kukabiliana na mashtaka ya kihalifu ambayo baadaye alikutwa na hatia. Hata hivyo Bw. Kiula hatimaye aliweza kushinda rufaa yake.
Bw. Kiula alizungumzia pia juu ya utawala wa Rais Mkapa na katika hilo anakubaliana na baadhi ya viongozi wengine wa zamani wanaotaka Rais Mkapa achunguzwe kutokana na matumizi ya nafasi yake kujitajirisha.
stay tuned...