Naichukia ndoa yangu..

Kupunguza ni kutafuta sehemu ya kuyaelekeza......

Unatafuta mtu mwenye extra kuzidi ya mumeo...game over....lol

Thanx The Boss sina maana ya kwamba natafuta nyumba ndogo..Ni je nipunge vip haya mapenzi kutoka 75 to 50% nateseka mie
Nahangaika ndani ya nyumba kama mama ,nampenda mme wangu,namuheshimu lakini yote anaona ni kazi bure..
nataka ibaki 50% ili hata kama akinifanyia visa nisiumie sana .
 
Thanx The Boss sina maana ya kwamba natafuta nyumba ndogo..Ni je nipunge vip haya mapenzi kutoka 75 to 50% nateseka mie
Nahangaika ndani ya nyumba kama mama ,nampenda mme wangu,namuheshimu lakini yote anaona ni kazi bure..
nataka ibaki 50% ili hata kama akinifanyia visa nisiumie sana .

Ndo maana nakwambia Plan A inakufanya uteseka sasa kwa mpango mzima tafuta plan B itakushusha mpaka kwenye 50%
 
Kesha sali sana na kufunga sana kesha ombewa sana mambo magumu.

Atafute plan B aweze kupooza mtima wake angalizo (mm mwenyewe nipo tayari kumpa faraja mama Clea)

Fidel80 acha kumsemea bana!,

hata ivyo Muumba hana mwanzo wala mwisho, usitegemee ukiomba leo akujibu leo
 
Pole sana. Omba Mungu atakusaidia. Na inabidi uombe sana. Mungu sio sukari inayokolea mara moja, lakini atasikiliza kilio chako na kumbadilisha.
Epuka na tamaa ya "kulipiza kisasi" au kitu cha namna hiyo
asante Kibukuasili ..naomba na kufunga kwa imani

siku moja kaa naye,mwangalie machoni mtamkie 'nakupenda sana darling' ......hakikisha naye anakuangalia machoni
Ni jana tu nimemwambia maneno haya akatazama pembeni bila kutoa neno lolote

Nitafute kwa ushauri zaidi - hii inahitaji faragha kuweza kuchukua 25% ya mapenzi kutoka kwa mtu!

nimeweka jamvini nisaidia hapa jambivi Obuntu ,asante

Kaka,nadhani ule uzi wa bishanga unahusika vile,lol!
Seriously mtoa mada, una miaka 29 ya umri na unasema mumeo hakui! Kwani ana umri gani?
Ana miaka 34

Unajua dada yangu tatizo ulilo nalo wewe ndilo nililo nalo na mimi kwa mke wangu, Nadhani nikutafute tubadilishane uzoefu na tuangalie the way forward plz ni-PM tu-arrange.

tubadirishane uzoefu gani?
 
Kweli wanawake mnadeka sana kama mtoto mchanga
Usipo bembelezwa ndo murder case ooh mm hubby hanipendi

We naye, mtoto mchanga hadeki, wanaodeka ni wale watoto wakubwa kubwa kidogo 2yrs na kuendelea. Ukiona mwanamke anadeka kwa mumewe, ujue anapendwa hapo upendo upo. Na shida yetu ni kupendwa ili tudeke...Hivi unaweza kumdekea mtu ambaye hakupendi si atakutoa baru jamani..Tudekezeni jamani
 
Kama ni kweli anayoyasema huyu mama naona yeye ndiye mwenye tatizo maana anatafuta jinsi ya kupunguza penzi na si jinsi ya kuokoa.Nashauri yeyote anayemshauri azingatie hilo.

Ni kweli Fige natafuta wataalam wa saikolojia wanisaidie hili ,linanisumbua sana..napenda niwe na mapenzi ambayo yamebalance hata akinifanyia vituko vyake nisiumie sana kama ninavyoumia sasa ,mpaka nahisi moyo unanipasuka
 
Yaonekana huyo mumeo anadeka na anajua unampenda.Wewe jifanye haujali vibweka vyake na kutokuonyesha anakuumiza na mambo yake.Jipende na usiache kula utapata vidonda vya tumbo bure na utakufa siku si zako na wanao watateseka.Wenzako wakiwa na maudhi ndio wananenepa kwa sababu wanajipendelea kila eneo hasa la chakula.
 
Fidel80 acha kumsemea bana!,

hata ivyo Muumba hana mwanzo wala mwisho, usitegemee ukiomba leo akujibu leo

Watu wanakufa wakiomba miaka nenda rudi na Mungu hawasikilizi kabisaaa hawa tusemeje?
 
We naye, mtoto mchanga hadeki, wanaodeka ni wale watoto wakubwa kubwa kidogo 2yrs na kuendelea. Ukiona mwanamke anadeka kwa mumewe, ujue anapendwa hapo upendo upo. Na shida yetu ni kupendwa ili tudeke...Hivi unaweza kumdekea mtu ambaye hakupendi si atakutoa baru jamani..Tudekezeni jamani

Mi namchukia sana mwanamke anae nidekea, maana najua ni wizi mtupu
 
JF nimeolewa miaka nane iliyopita nikiwa na 21 years old,nimekaa na mme wangu katika ups and down za ndoa ..
Ila mme wangu naona ana mambo mengi ya ujana,dharau na kutojari familia , hakui najaribu kumwelewesha misingi ya ndoa na kumwelewesha pale anapoenda kinyume
lakini inakuwa kazi bure.
Kinachoniuma nadhani nampenda sana mme wangu akinikosea ninaumia hata week nzima siwezi kula ,kulala Napata shida wakati yeye
Anakuwa normal na hana hata muda wa kuomba msamaha.
Nahisi haya mapenzi niliyonayo kwa mme wangu yananiua ama kunipeleka vibaya.
Mtaalam mmoja aliniambia Tatizo langu nina 75% ya penzi kwa mme ,nijaribu kuweka 50/50%
Najitahidi kufanya hivo na ku-ignore yote anayoyafanya ,,mwisho wa siku nashindwa najikuta naendelea kuumia zaidi na kunyong'onyea .
Ni mengi anayonikosea.
JF ninawezaje kupunguza haya mapenzi ili niishi kwa Amani?
Nisaidie nakufa siku si zangu..nifundisheni nilipunguze vip hili penzi kwa baba chanja nisiumie

Mama Clea


Pole Condeliza dia .................Mungu akusaidie. Jamani mi sikuombei mapenzi ya pungue kwa mumeo bali nakuombea mumeo abadilike na kuwa baba halisi nyumbani kwenu. Mi siamini kama kuna kupenda 50/50 ni either yapo au hayapo. Take heart dear one God is there for you.
 
1.Anaekwambia upunguze penzi anafanya kosa la kiufundi...ukipunguza matatizo yanazidi.
2.dawa ni kuzidisha penzi. Likifika 100% hutaona kosa au tatizo lolote toka kwa mumeo. Kila kitu utaona kizuri.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom