Mwana FA mgeni rasmi Simba Vs Vipers, mchezo wa CAF Champions League

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma (Mwana FA) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa klabu bingwa Afrika kati ya Simba Vs Vipers SC ya Uganda mchezo utakaochezwa Jumanne Machi 7, 2023 katika Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
 
Mimi ndiyo maana naamini kuwa mifumo yetu ya kisiasa ndiyo kikwazo cha maendeleo nchi hii.

Huyu MwanaFa ni msanii mkubwa muda mrefu na amekuwa mpenzi mkubwa wa Simba muda mrefu, lakini hawajawahi kufikiria kumpa ugeni rasmi hata katika mechi za kirafiki. Leo hana hata wiki tena kwa cheo cha Unaibu Waziri ndiyo wanaona anafaa kupewa heshma hiyo.

Lini wamewahi kumkumbuka hata mchezaji wa zamani na kumpa heshima hiyo?

Na hii nazungumzia kwa vilabu vyote na tasnia nzima ya sanaa na michezo.
 
Kwanza Mpe Heshima yake
Hao unao waheshimu wewe Ni Watanzania kama yeye
Hawana Vichwa 2 Wala Mikono 10
Kwenye Simba Nayanga Hakuna Utakaye Mchagua Asiwe katika Hizo Timu
Amealikwa kwakuwa ni Kiongozi kwa sasa
 
Haujaelewa mantiki ya hoja yangu. Kwa nini hiyo heshima ya ugeni rasmi hawakuweza kumpa kabla ya nyadhfa ya kisiasa? Na kwa nini mpaka mtu awe na cheo ndiyo tunamuona wa maana?
 
Ajabu nini mpaka kuanzisha mada kwa jambo lisilo na tija yoyote kwa Simba.
 
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma (Mwana FA) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa klabu bingwa Afrika kati ya Simba Vs Vipers SC ya Uganda mchezo utakaochezwa Jumanne Machi 7, 2023 katika Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Kazi kweli siku hiyo asijegeuka akajisahau akawa na midadi ya ushabiki yy sasa hivi ni mheshimiwa sana
 
Kaka utatupiga sasa.. next mechi mgeni rasmi utakuwa wewe..!
MwanaFa ni msanii wa muda wote ninayemkubali katika kizazi cha Bongo Flava. Eleweni mada zinazoletwa mezani, watu mna vichwa vigumu sana.
 
Ajabu nini mpaka kuanzisha mada kwa jambo lisilo na tija yoyote kwa Simba.
Mimi sijaanzisha mada. Nimewahi kuyatoa haya maoni mara nyingi tu, leo nimeona huu uzi ni sehemu sahihi ya kukumbushia.
 
Mimi ndiyo maana naamini kuwa mifumo yetu ya kisiasa ndiyo kikwazo cha maendeleo nchi hii.

Huyu MwanaFa ni msanii mkubwa muda mrefu na amekuwa mpenzi mkubwa wa Simba muda mrefu, lakini hawajawahi kufikiria kumpa ugeni rasmi hata katika mechi za kirafiki. Leo hana hata wiki tena kwa cheo cha Unaibu Waziri ndiyo wanaona anafaa kupewa heshma hiyo.

Lini wamewahi kumkumbuka hata mchezaji wa zamani na kumpa heshima hiyo?

Na hii nazungumzia kwa vilabu vyote na tasnia nzima ya sanaa na michezo.
Kwani wakati mama samia anakamatwa na trafiki barabarani kwa kosa la kuoverspeed ulitegemea leo hao trafiki wangemsafishia njia?

Bro dhamana na thamani ni kwenye vyeo ndugu.
 
Sijaelewa unachokisema kinaingiaje hapa. MwanaFa ni msanii ambaye amekuwa anaishi bila scandal zozote za kihuni au kiuhalifu kwa hiyo angealikwa wakati ni msanii tu wa muziki ila mdau wa Simba isingeleta minong'ono wala mshtuko wowote katika jamii.

Kwani wakati mama samia anakamatwa na trafiki barabarani kwa kosa la kuoverspeed ulitegemea leo hao trafiki wangemsafishia njia?

Bro dhamana na thamani ni kwenye vyeo ndugu.
 
Hamisiii nakuita mara 3.

Kazi yako ya kwanza ni kumuokoa kijana wa kizanzibari mwenye malalamiko mengi juu ya soka la ugali na sukari
 
MwanaFa ni msanii wa muda wote ninayemkubali katika kizazi cha Bongo Flava. Eleweni mada zinazoletwa mezani, watu mna vichwa vigumu sana.
Swali dogo tu ni kua ili uwe mgeni rasmi wa mpira inabidi uwe na sifa Gani? Maarufu? Mwanasiasa? Etc?
 
Nadhani yoyote anaweza kupewa heshima hiyo ingawa inaonekana wanaopewa ni wanasiasa. Ningependa kuona wengine ikiwemo wachezaji au watendaji wa zamani waliowahi kuitumikia club wakipewa heshima hiyo.

Ningefurahi zaidi kama MwanaFa angepewa heshima hii KABLA ya uteuzi wa juzi.
 
Back
Top Bottom