Naibu spika NDUGAI apinga vikali spika kutokuwa mbunge

Alikuwa anategemea kuwa speaker kamili 2015 kwa hiyo anaona shingo yake imeshaliwa!!!!!!!!!
Basi ajiondoe kwenye chama chake ili 2015 asiwe mbunge agombee uspika. Lakini nadhani inatakiwa usiwe mwanachama wa chama cha siasa kwa miaka 5 kabla ya uchaguzi wa spika, kwa hiyo hata 2015 atakuwa bado hajakamilisha 5 years hata kama itatokea atajivua gamba leo
 
Uyu Ndugai anataka kutuaminisha kua Jaji anaweza kusimamia kesi ya mtoto wake bila kuadhiri haki kitu ambacho hata sheria hairuhusu (conflict of intetest)..
 
Akalime mashamba kongwa atuachie bunge letu. hana sera anataka vyeo vyote haoni speker kutoka nje unakuwa umeongeza ajira 1 kwa mtanzania? na pia kunapunguza ubaguzi ndani ya bunge.
 
Tatizo la Ndugai anafikiri bado tuko kwenye mfumo wa chama kimoja!

Kwa hali ya kibinadamu, Spika ambaye ni mbunge wa chama fulani, hata ajitahidi vipi kuna wakati lazima atkipendelea chama chake. Kuondoa hii hali Spika asichaguliwe kutokana na wabunge!
 
Ndugai si amezoea matusi na kejeli bungeni. Uwezo wake wa kuona mbali ni mdogo sana. Kuendelea kuongozwa na viongozi kama akina Ndugai ni kurudi nyuma. Hafai hata kuongoza taasisi zaidi ya familia yake
 
wale wote wenye urohpo wa madaraka hii katiba inawaumiza sana ndo maana hata ndugai hatulii maana alikuwa anacount 2015 amreplace makinda ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha sasa sie wanchi hiyo ndo hatutaki tunataka proffesionals katika hizi nafasi tulete watu wapya na kuwe na mabadiliko kabisa na naomba katika vetting ya nafasi za juu na bunge itumike kimombo kabisa kama ilivokuwa inatumika wakati wa kutafuta wabunge wa EALA ili kupunguza vilaza kabisa
 
Mbona mkuu wa shule anaongoza wanafunzi ili hali yeye si mwanafunzi?

mkuu argument yako si mchezo!! Lakini wanafunzi wanachagua kiranja mkuu wao ambaye ndiye huwa mwenyekiti wa baraza la shule! Lakini binafsi napendelea spika asiwe mbunge tofauti na maoni ya Mhe. Ndugai. Nakumbuka Mzee Msekwa katika kipindi chake cha mwisho cha uspika hakuwa mbunge!
 
Huyu jamaa na wasi wasi na ufahamu wake! Ubunge umekuwa na Proffessionalism kama udakitari kweli kuwa Mbulula sio lazma ufeli mtihani
 
Mzee wa wanyamapori analilia mpunga.duu kwa rasmu hii weng watatoa machoz hadharani.
 
Ndo maana mi nasema hii rasimu ukiiangalia kwa jicho la utaifa au uzalendo imekaa poa sana, ila ukiiangalia kichama chama au kimaslahi binafsi utaikosoa mpaka basi!! Big up Warioba et al :)
 
Mtu mmoja hawezi kubadili Katiba ya Nchi iliyoridhiwa na Watanzania wengi tena kwa kupenda kwake madaraka. Pole Ndugai unaibu kwa heri una miaka miwili tu kuvaa joho!! Katiba Hii Haina Rangi ya Chama Chochote, tumeipenda sana Shukrani Mh Joseph Sinde Warioba J.
 
Ndungai amesahau katiba ya sasa inaruhusu kabisa mtu ambaye sio mbunge kugombea uspika na akishinda anakuwa spika na ndo maana Mabere Marando alijaribu kugombea kwa tiketi ya chadema wakati hakuwa mbunge. Sema sasa kwa sababu imeboreshwa tu kuwa mbunge kwa sasa hataruhusiwa kugombea sasa anajiuliza aache kugombea ubunge halafu awanie uspika au akomae tu na ubunge ndoto za kuwa spika zifie hapo
 
lazima aseme hivyo mana anajua Makinda alishasema hagombei tena ubunge kwa ivo alijua 2015 atakuwa spika sasa wamemshitukia pole zake
 
Wanajamvi, mm nindugu yenu, naomba sana kuungwa mkono na ninyi, nataka kugombea jimbo la Kongwa, nibishane na Ndugai au na yeyote, mimi nitakuwa mgombea binafsi thou bado rasimu lkn nilipanga kugombea hata kwa chama chochote, huyu jamaa ameiharibu sn kongwa, wilaya ya mika nenda rudi lkn inashindwa na kibaigwa ya juzi, hata madhari yake kama siyo wilaya, tumebarikiwa maji tele, mafuriko miaka yote, lkn njaa, yeye yupo tu, njia ya vumbi, yeye yupo tu, jamani nisaidieni nataka kuikomboa Kongwa, mara nikichaguliwa, nitaandaa mabwawa makubwa sn kwenye nja ya maji ya mvua, nitahakikisha watu wanalima masika na kiangazi kando ya maji hayo, nitahakikisha mfuko wa jimbo unanunua chakula cha tahadhari badala yakusubiri chakula cha serikali, nitajenga ofisi ya jimbo ambapo kila mru atakuwa huru kuja kusema chochote, pia nitavuta maji kwenye milima yetu yakaribu kwenda sehemu kame, tafadharini niungeni mkono nikotayari kwa faida ya wote, niko serious, japo wapo watakao ni beza, elimu yangu nina MBA, na sasa nipo nje kikazi ya serikali natazamia kurudi haraka sana kukomba ndugu zangu, natokea Chamkoroma kwa wale wanao jua huko.
Asanteni vijana ndo nguzo ya Taifa la TZB .
 
Ana wasiwasi kuwa mwisho wa CCM utakuwa umefika,Watu wamechoka na upendeleo bungeni,ukanadamizaji wa vyama vya upinzani.ccm hoii
 
Back
Top Bottom