Naibu spika NDUGAI apinga vikali spika kutokuwa mbunge

Kiwa

JF-Expert Member
Oct 4, 2011
2,109
1,250
Na upumbavu kufananisha mwenyekiti wa chama cha madaktari na SPIKA wa bunge!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
kinyoba

JF-Expert Member
Jun 2, 2011
1,272
1,250
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai amepinga mapendekezo ya rasimu yanayotaka Spika na msaidizi wake wasitokane na vyama.

Ndugai, ambaye ni Mbunge wa Kongwa aliiambia Mwananchi jana kuwa ni kitu kizuri kwa Spika kuwa miongoni mwa wabunge.

“Mimi nadhani kuna tatizo hapa. Pamoja na kwamba ni rasimu, lakini ni kosa kwa Spika kutokuwa na chama.

“Hivi kweli, kuna umoja wa madaktari, halafu kiongozi wao atoke nje ya fani ya udaktari, sidhani kama kutakuwa na ufanisi na kuelewana hapo,” aliongeza Ndugai.Hata hivyo, Ndugai alisema kuwa suala zima ni mapendekezo, na litakuja hadi Bungeni kwa majadiliano na hii itapata changamoto nyingi.

source gazeti la mwanainchi leo.

Maoni yangu, huyu bwana asijifagilie nakumbuka nchi hiihii bunge hilihili la ambalo nae NDUGAI amebahatika kuwa mbunge liliwahi kuwa na spika ambae hakuwa mbunge ambae nakumbuka alikuwa akiitwa Chifu Adam Sapi Mkwawa, bunge aliliendesha vizuri kabisa kwani tatizo lilikuwa nini

Mhe NDUGAI akubali matokeo, spika bila kuwa bunge inawezekana.
huyu jamaa kweli kachanganyikiwa! siasa ya tanzania ni Fani? siasi ya Tanzania ni usanii tu na ujanja ujanja! tunamtaka spika ambaye hayumbishwi na usanii uliopo katika vyama. tunataka spika mwenye busara atakaeongoza bunge katika standars zake. wapo wasomi wengi tu TZ wasio na vyama ambao wanaweza kuliongoza bunge kuliko hao tulionao sasa hivi.
 
Piere. Fm

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,196
2,000
Jamaa katolea mfano madaktari inamaana ye hajui kuwa i le profesional? Tena me ningependa sio tu kwamba asiwe mbunge bali awe Mwanasheria.
 
Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,307
2,000
“Hivi kweli, kuna umoja wa madaktari, halafu kiongozi wao atoke nje ya fani ya udaktari, sidhani kama kutakuwa na ufanisi na kuelewana hapo,” aliongeza Ndugai.
Mama yangu!.....huyu ndio naibu spika?

Hata kule TFF pamoja na madudu yake hawachaguani moja kwa mojan kwa Usimba au Uyanga wao licha ya kuwa viongozi wa soka huwezi kuwatenganisha na ushabiki wao
 
FARC

Member
Dec 4, 2012
12
20
Ndugai ni goigoi wa uongozi!Angeanza kukataa kwanza mgombea binafsi kwasababu bungeni kunaweza kuwa na wabunge huru ambao hawafungamani na chama chochote ila hauwezi kuwa na daktari huru ambaye hana taaluma.Hivyo anajaribu kutuhadaa magreat thinkers! Bungeni kunaweza kutokea conflict of interest Rais ambaye ni mwenyekiti wako anaweza toa maagizo ya kulinda chama chake kwa spika wa chama chake bugeni. Apuuzwe anatapatapa.
 
LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
5,589
2,000
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai amepinga mapendekezo ya rasimu yanayotaka Spika na msaidizi wake wasitokane na vyama.

Ndugai, ambaye ni Mbunge wa Kongwa aliiambia Mwananchi jana kuwa ni kitu kizuri kwa Spika kuwa miongoni mwa wabunge.

“Mimi nadhani kuna tatizo hapa. Pamoja na kwamba ni rasimu, lakini ni kosa kwa Spika kutokuwa na chama.

“Hivi kweli, kuna umoja wa madaktari, halafu kiongozi wao atoke nje ya fani ya udaktari, sidhani kama kutakuwa na ufanisi na kuelewana hapo,” aliongeza Ndugai.Hata hivyo, Ndugai alisema kuwa suala zima ni mapendekezo, na litakuja hadi Bungeni kwa majadiliano na hii itapata changamoto nyingi.

source gazeti la mwanainchi leo.

Maoni yangu, huyu bwana asijifagilie nakumbuka nchi hiihii bunge hilihili la ambalo nae NDUGAI amebahatika kuwa mbunge liliwahi kuwa na spika ambae hakuwa mbunge ambae nakumbuka alikuwa akiitwa Chifu Adam Sapi Mkwawa, bunge aliliendesha vizuri kabisa kwani tatizo lilikuwa nini

Mhe NDUGAI akubali matokeo, spika bila kuwa bunge inawezekana.
Ndugai ni kiazi kilichokutana na jiwe, udhaufu wao wa kuliongoza bunge ndio uliofanya wananchi wakatae ujinga.
Mbona mawaziri wanaongoza wizara ambazo haziendani na fani zao walizosomea???
Pole Ndugai kama ulidhani kuna siku utakuwa spika futa na kifutio. By the way bunge la 2015 utalisikia kwenye bomba, Kongwa wameshaona huwafai.
 
A.R.M

Member
Oct 6, 2012
89
95
Bila shaka ndugai anataka kujaribu tena nafasi zote 2 mwaka 2015(ubunge na uspika) hivyo katiba mpya itamkosesha kimoja.
 
Chikwa

Senior Member
Jul 26, 2012
138
195
Naibu Spika asiyejua historia ya bunge...Msekwa, Adam Sapi, Karimjee waliwahi kuwa Maspika bila ya kuwa wabunge.

Ni miaka michache imepita wabunge walichagua Spika na yeye Ndugai aligombea, Mzee Marando aligombea lkn hakuwa mbunge au ameshasahau. Ahhh hawa wanasiasa wetu hawa......
 
Aggrey86

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
855
195
Ndungai keshaanza kuweweseka mapema hivi wakati yeye mwenyewe ni shahidi jinsi anavyoongoza bunge kwa upendeleo na kuvunja sheria za bunge ilimradi akibebe chama chake.
 
mtotowamjini

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
4,531
0
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai amepinga mapendekezo ya rasimu yanayotaka Spika na msaidizi wake wasitokane na vyama.

Ndugai, ambaye ni Mbunge wa Kongwa aliiambia Mwananchi jana kuwa ni kitu kizuri kwa Spika kuwa miongoni mwa wabunge.

"Mimi nadhani kuna tatizo hapa. Pamoja na kwamba ni rasimu, lakini ni kosa kwa Spika kutokuwa na chama.

"Hivi kweli, kuna umoja wa madaktari, halafu kiongozi wao atoke nje ya fani ya udaktari, sidhani kama kutakuwa na ufanisi na kuelewana hapo," aliongeza Ndugai.Hata hivyo, Ndugai alisema kuwa suala zima ni mapendekezo, na litakuja hadi Bungeni kwa majadiliano na hii itapata changamoto nyingi.

source gazeti la mwanainchi leo.

.
hivi huyu jamaa kaenda shule kweli? madaktari wote ni wa moja hawajali chama wanateteana wote kama madaktari hata walimu wanateteana wote kama group moja...wabunge kuna wa ccm cuf chadema hakuna umoja maana kila chama kina sera tofauti ndio maana kila siku kuna matusi huko bungeni....spika awe neutral thats it.
 
Mtumbatu

JF-Expert Member
Apr 27, 2012
328
225
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai amepinga mapendekezo ya rasimu yanayotaka Spika na msaidizi wake wasitokane na vyama.

Ndugai, ambaye ni Mbunge wa Kongwa aliiambia Mwananchi jana kuwa ni kitu kizuri kwa Spika kuwa miongoni mwa wabunge.

“Mimi nadhani kuna tatizo hapa. Pamoja na kwamba ni rasimu, lakini ni kosa kwa Spika kutokuwa na chama.

“Hivi kweli, kuna umoja wa madaktari, halafu kiongozi wao atoke nje ya fani ya udaktari, sidhani kama kutakuwa na ufanisi na kuelewana hapo,” aliongeza Ndugai.Hata hivyo, Ndugai alisema kuwa suala zima ni mapendekezo, na litakuja hadi Bungeni kwa majadiliano na hii itapata changamoto nyingi.

source gazeti la mwanainchi leo.

Maoni yangu, huyu bwana asijifagilie nakumbuka nchi hiihii bunge hilihili la ambalo nae NDUGAI amebahatika kuwa mbunge liliwahi kuwa na spika ambae hakuwa mbunge ambae nakumbuka alikuwa akiitwa Chifu Adam Sapi Mkwawa, bunge aliliendesha vizuri kabisa kwani tatizo lilikuwa nini

Mhe NDUGAI akubali matokeo, spika bila kuwa bunge inawezekana.
Mchumia tumbo tu huyo, yupo kwa ajili ya manufaa yake sio wananchi waliomchagua, asubiri kusulubiwa na wananchi ikipita katiba mpya
 
Mnyakatari

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,820
2,000
Huyu Ndugai nae!Mbona hakuwahi kuipinga katiba ya sasa ambayo inatoa mwanya wa uwezekano wa Spika kuwa sio mbunge!

Tofauti hapa ni rasimu imefutilia mbali uwezekano wa mbunge kuwa spika.Lakini uwezekano wa mtu asiye mbunge kuwa spika upo tangu kwenye katiba hii ya 1977.

Sijawahi msikia Ndugai akiipinga hii katiba hasa hiko kipengele!
 
Luno G

JF-Expert Member
Sep 22, 2012
2,368
2,000
huyu ndugai si mzima mbona hasemi ili kuwa refarii sio lazima uwe mchezaji
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom