Naibu spika NDUGAI apinga vikali spika kutokuwa mbunge

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,205
2,690
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai amepinga mapendekezo ya rasimu yanayotaka Spika na msaidizi wake wasitokane na vyama.

Ndugai, ambaye ni Mbunge wa Kongwa aliiambia Mwananchi jana kuwa ni kitu kizuri kwa Spika kuwa miongoni mwa wabunge.

"Mimi nadhani kuna tatizo hapa. Pamoja na kwamba ni rasimu, lakini ni kosa kwa Spika kutokuwa na chama.

"Hivi kweli, kuna umoja wa madaktari, halafu kiongozi wao atoke nje ya fani ya udaktari, sidhani kama kutakuwa na ufanisi na kuelewana hapo," aliongeza Ndugai.Hata hivyo, Ndugai alisema kuwa suala zima ni mapendekezo, na litakuja hadi Bungeni kwa majadiliano na hii itapata changamoto nyingi.

source gazeti la mwanainchi leo.

Maoni yangu, huyu bwana asijifagilie nakumbuka nchi hiihii bunge hilihili la ambalo nae NDUGAI amebahatika kuwa mbunge liliwahi kuwa na spika ambae hakuwa mbunge ambae nakumbuka alikuwa akiitwa Chifu Adam Sapi Mkwawa, bunge aliliendesha vizuri kabisa kwani tatizo lilikuwa nini

Mhe NDUGAI akubali matokeo, spika bila kuwa bunge inawezekana.
 
Anajua ugali wake unaanza kufikia mwisho mwisho. Kwa ratiba ya Tume ya katiba kufikia April 2014 ni lazima kuwe na katiba mpya, hivyo vyeo walivyo navyo kina Ndugai na Makinda vitakoma!!!

Alikuwa ana mipango ya kiujanja ujanja ya kumrithi mama makinda, kumbe mama Makinda akawa mjanja akawahi kutangaza kuwa agombei tena Ubunge lakini Kugombea Uspika hakusema kitu, vivyo hivyo kwa Sitta kashasema hagombei tena Ubunge lakini kugombea Uspika hakusema kitu.
 
ye alitegemea aje agombee ubunge ili awe spika ndugai acha tamaa kwani spika kutokua mbunge au mfuasi kutoka chama chochote cha siasa hakitaleta upendeleo wowote ndani bunge.


"the difference between the stupidity and genius is that genius has its limits" Albert Einstein.
 
Duh! Hii rasimu ya katiba imetibua mipango ya wengi. Jamaa alikuwa napigia mahesabu ya Uspika baada ya Anna Makinda. Wapo wengine hawatagombea tena ubunge kwa kuwa walikuwa wanajikomba kwenye kambi Fulani ili wapate pande la uwaziri.
 
Ngoja tusubiri bunge maalumu la katiba kama watapendekeza kama atakavyo Ndugai!
 
Maskini jamaa alikuwa bado ana mawazo ya uspika tena kwa kupigiwa kura za Ndioooooo na chama chake,
imekula kwako Ndugai'
 
Kwa mtazamo wangu Sifa na vigezo vya kupata na uwepo wa Spika ni moja ya sehemu ya Rasimu ya Katiba mpya zilizo ainishwa vema. Matatizo tuliyo nayo Bungeni sasa hivi kwa kiasi kikubwa yanachangiwa sana na the Fact kua Spika na Naibu Spika wote ni Viongozi wa Siasa na inajulikana wazi kua wapo upande wa Chama fulani (tawala). That in itself ni disadvantage sababu ni vigumu sana kuangalia maslahi ambayo yanaumiza upande wao kwa namna yoyote ile.

Spika inatakiwa awe neutral na kutoa maamuzi bila kuangalia Sura ya Wabunge ama interest ya yale yanayowakilishwa kwa Chama chochote kile. Kwanza ilistahili hata sifa moja wapo ni kuwa asiwe amefungamana na Chama chochote... In the sense kuwa asiwe mwanachama wa Chama chochote. Or hata kama aliwahi kuwa mwanachama huko nyuma anapochaguliwa kuwa Spika uanachama unajifuta by default.
 
Rasimu tu mapovu kibao,ikija katiba halisi sasa? job hawezi kuwa spika kamili,hana nidhamu,sio mvumilivu,ana hasira,jeuri,kujiona yeye ndiyo yeye,and i blv anatamani hata maadamu asiamke ili akaimu hicho kiti na kumalizana na wabunge wa cdm mara moja.

Rasimu hii ina mapungufu kiasi,acha ije kwetu tuijadili tena na tena then tuone kama itakidhi haja zetu sisi kama jamii,pamoja na yote hili swala la rais kuteua majaji kisha wakahakikiwe na bunge?
 
  • Thanks
Reactions: ram
Mbona mkuu wa shule anaongoza wanafunzi ili hali yeye si mwanafunzi?
i

You're too smart and sharp!! Ndugai ni tabularasa huyo, kwanini asitoe madhara ya kuwa na Spika/Deputy ambae sio mwanachama wa politiko pati.
 
Madaraka matamu sana hata ningekuwa mimi ningepinga vikali sana

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Huyu jamaa ni kilaza kweli! Kwani ubunge ni profession? Kigezo kikubwa cha kuwa spika ni kuwa jingajinga ili ufanye upuuzi.
 
Back
Top Bottom