Naibu spika NDUGAI apinga vikali spika kutokuwa mbunge

Kutapatapa kwingine kwa Ndugai kunachekesha sana! Kwani Katiba na sheria ya sasa zinamzuia mtu kuwa Spika bila kuwa Mbunge? Si Pius Msekwa si aliwahi kugombea bila kuwa mbunge na akabwagwa na Sitta?

Kwa mtu kama Ndugai , bila kutumia ubunge ili kuwa Spika atakosa kabisa uwezo wa kuongoza bunge lenyewe (atapoteza kabisa Confidence ) , maana ni mvunja sheria za bunge ! Sasa anaona afadhali ubunge maana utamfichia aibu kuliko asipokuwa mbunge ! Shame on him !
 
watumie uwezo wao kuifanya tume ifuate matakwa yao

hawaoni wenzao wa kenya.

......waanze na kuwanyima bajet kabla ya kutoipitisha

wakati wa bunge maalum la katiba.
 
Sishangazwi na hoja zake nyepesi.. sio kosa lake. Wenye akili zao wamejadili vya kutosha.. na kuona umuhimu wa spika kutoka nje ya vyama vya siasa, na kutoka nje ya Bunge ili kumaliza kasumba ya kubebana... sasa...
 
Naomba aelewe tunatumiaPESA nyingi za walipa kodi kuuandaa katiba yetu! Hii ni safari ya kututoa kwenye umasikini uliopindukia kwenda kwenye kipato cha kati! Sasa wasitake katiba iandaliwe ili kushibisha MATUMBO Yao kwa miaka mitano ujayo! Naomba waelewe tunaandaa mwongozo unaweza kutufaa hata kwa miaka 200 ijayo! Nakushukuru Warioba na team yako kwa kazi nzuri na ngumu.
 
Ndugai alisema kuwa suala zima ni mapendekezo, na litakuja hadi Bungeni kwa majadiliano na hii itapata changamoto nyingi.
Hii ngoma ikija bungeni lazima CCM wataipiga Tik Taka! ili hoja hii ipite na ukizingatia Ndugai ni naibu spika!
 
Imbecile ******! Hawezi hata kufikiri, yeye anawaza kusema Lissu out, Sugu out, Mnyika out, Lema out, Wenje out, Msigwa out!
 
Aache kugombea ubunge, ili achaguliwe uspika. Ila rasimu yangu ni kwamba ndugai anafaa kuwa mwenyekiti wa maboda boda.
 
Huyu jamaa ni mpuuzo sana, hajuai kuwa Hata bosi wake Anne Makinda alilipendekeza hili. Bado nina tatizo kubwa kama mambo haya ambayo tunayashangilia Bunge la katiba (la CCM) au Mabaraza ya Katiba (ya CCM) yataruhusu!

Lakini Watanzania tuwe tayari kupigania haya wakati wa kura ya maoni!
 
NDUGAI anaogopa kibarua kitaota ndio maana ana kipalilia. na hii ni tatizo kubwa kwa watu ambao ni waroho wa madaraka.
 
Mfano alioutoa hauendani na swala analolizungumzia. Daktari ni fani na watu wanasomea miaka 5 lakini ubunge sio fani ni leadership position ambayo mwenye fani yoyote anayeweza kuitumikia. Sema ndoto zake za kuwa na vyeo viwili zimeota mbawa.
 
Ndugai, ambaye ni Mbunge wa Kongwa aliiambia Mwananchi jana kuwa ni kitu kizuri kwa Spika kuwa miongoni mwa wabunge.

“Mimi nadhani kuna tatizo hapa. Pamoja na kwamba ni rasimu, lakini ni kosa kwa Spika kutokuwa na chama.

“Hivi kweli, kuna umoja wa madaktari, halafu kiongozi wao atoke nje ya fani ya udaktari, sidhani kama kutakuwa na ufanisi na kuelewana hapo,” aliongeza Ndugai.


Nadhani Job Ndugai hakutumia muda mwingi kufikiri alipoamua kutumia mfano huo wa madaktari na pendekezo katika rasimu.
Mfano wake haupo hai kwa mantiki moja tu, Udaktari ni taaluma inayosomewa, maudhui na ujuzi upatikanao ndio humfanya mtu kuwa daktari. Kwa mantiki hiyo kuna ukweli kwamba kiongozi wa jopo la madaktari ni busara kuwa naye awe na taaluma hiyo.
Hilo ni kinyume kwa Ubunge kwani ni uwakilishi tu na wala sio taaluma kwamba mtu anapaswa kuusomea. Hivyo Spika wa Bunge si lazima sana awe na kofia ya Ubunge kwani mwiko pekee wa kusimamia Bunge ni kufuata taratibu zilizowekwa sambamba na kuzisimamia.
 
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai amepinga mapendekezo ya rasimu yanayotaka Spika na msaidizi wake wasitokane na vyama.

Ndugai, ambaye ni Mbunge wa Kongwa aliiambia Mwananchi jana kuwa ni kitu kizuri kwa Spika kuwa miongoni mwa wabunge.

“Mimi nadhani kuna tatizo hapa. Pamoja na kwamba ni rasimu, lakini ni kosa kwa Spika kutokuwa na chama.

“Hivi kweli, kuna umoja wa madaktari, halafu kiongozi wao atoke nje ya fani ya udaktari, sidhani kama kutakuwa na ufanisi na kuelewana hapo,” aliongeza Ndugai.Hata hivyo, Ndugai alisema kuwa suala zima ni mapendekezo, na litakuja hadi Bungeni kwa majadiliano na hii itapata changamoto nyingi.

source gazeti la mwanainchi leo.

Maoni yangu, huyu bwana asijifagilie nakumbuka nchi hiihii bunge hilihili la ambalo nae NDUGAI amebahatika kuwa mbunge liliwahi kuwa na spika ambae hakuwa mbunge ambae nakumbuka alikuwa akiitwa Chifu Adam Sapi Mkwawa, bunge aliliendesha vizuri kabisa kwani tatizo lilikuwa nini

Mhe NDUGAI akubali matokeo, spika bila kuwa bunge inawezekana.

Asidanganye watu, wabunge nitofauti na madaktari. Daktari ni 'proffession' wabunge ni wawakilishi walioteuliwa na wananchi wanaokubaliana na itikadi za kisiasa za wawakilishi hao. lazima spika awe 'neutral' kwa kutokuwa mwanasiasa wa chama chochote
 
naibu spika wa bunge, job ndugai amepinga mapendekezo ya rasimu yanayotaka spika na msaidizi wake wasitokane na vyama.

Ndugai, ambaye ni mbunge wa kongwa aliiambia mwananchi jana kuwa ni kitu kizuri kwa spika kuwa miongoni mwa
wabunge.

“mimi nadhani kuna tatizo hapa. Pamoja na kwamba ni rasimu, lakini ni kosa kwa spika kutokuwa na chama.

“hivi kweli, kuna umoja wa madaktari, halafu kiongozi wao atoke nje ya fani ya udaktari, sidhani kama kutakuwa na ufanisi na kuelewana hapo,” aliongeza ndugai.hata hivyo, ndugai alisema kuwa suala zima ni mapendekezo, na litakuja hadi bungeni kwa majadiliano na hii itapata changamoto nyingi.

Source gazeti la mwanainchi leo.

Maoni yangu, huyu bwana asijifagilie nakumbuka nchi hiihii bunge hilihili la ambalo nae ndugai amebahatika kuwa mbunge liliwahi kuwa na spika ambae hakuwa mbunge ambae nakumbuka alikuwa akiitwa chifu adam sapi mkwawa, bunge aliliendesha vizuri kabisa kwani tatizo lilikuwa nini

mhe ndugai akubali matokeo, spika bila kuwa bunge inawezekana.


amesahau magamba wanavyofanya. Blandina nyoni kutoka uhasibu mpaka uadaktari wizara afya.
 
ubunge sio fani, ni tofauti kubwa sana na udaktari, DAKTARI ANAWEZA KUWA MBUNGE, LAKINI MBUNGE HAWEZI KUWA MBUNGE, NDUGAI ANAUWEZO MDOGO SANA WA KUFIKIRI
 
...Ndugai is an ignorant politician.....yeye ameshindwa hata kujua kuwa amechangia sana kwa watanzania kujua tatizo kubwa walilonalo wao kama ma spika (kutoka ccm)kwenye maamuzi yao mengi yaliyojaa utashi wa siasa za chama chao.....Inasikitisha sana kuona anafikiri watanzania bado wamelala kama yeye.....
 
Kumbe alikuwa anategemea kuwa atapewa tena nafasi ya kulivuruga bunge?!!!!
 
Back
Top Bottom