Naibu Spika kuwa na adabu kidogo

Naibu Spika kuwa na adabu kidogo

..mi naipenda tone yake....maana inakua kama ya demu wa ukwe...bila hiyo arrogance watu watakavua nguo mchana kweupe...kama yule demu wa kibongo huko India....
 
Wameshakuharibu kijana sio kosa lako.
Mkuu achana nae huyu hana analolijua ni kanjanja tu na mungo mkubwa Mzee wa Ufaransa ambapo pana nyumba za kizaramo yaani anafix huyu bwana ni hatari anatanabahi kuwa anategwa na mama mkwe wake Mbelgiji kwamba huwa anakatisha sebuleni akiwa anaenda kuoga na hvyo humuachia hali tete sana sasa bado najiuliza huka ufaransa kuna nyumba kama za kwetu uzaramoni ambapo ukienda kuoga mpaka upite sebuleni??? huyu mtu ni USELESS na maneno yake machafuu
 
Mkuu una mbwembwe sana mara Ufaransa mara Marekani sijui unaishi wapi hasa?Mara Rwanda mara Tanzania mara usalama wa Taifa aiseee wewe ni nomaaa.....anyway habari yako Mkuu?
Mie nilijua anaishi Congo Kishansha maaana kuna jukwaa letu la wapenda bolingo yeye huchambua hadi nyimbo na historia ya bendi za huko.
 
Bungeni sio nyumbani kwako, kama unataka upewe heshima ya babu basi kakae na wajukuu zako nyumbani. Ukileta uharo hakuna wa kutazama umri wako, unapewa kavukavu.
 
To be honest huyu naibu spika Mimi simpendi tu automatically wala sio manually hahaha.
Anajisikia sana, she is so arrogant and she thinks she knows every thing.
I bet IPO siku atakuja tibuana na akina mdee, lisu, sakaya, mnyika,nk watampa live bila chenga.

Swadakta Crucial Man;

Kwake yeye anateswa na intellectual arrogance akiamini being a phd holder wa sheria anajua kila kitu na yuko right always..so anakua too defensive!

Tatizo lingine ni kuwa kuna watu wame-mjaza profiles za prominent figures kichwani so its like kabla hujamaliza kuongea wewe..TL say..anakua amejiandaa reaction..so mostly ana ku pre judge!..

- Upande wa wabunge wengine wanajistukia mapema ..mfano juz kati kuna mmoja alisema"tena eti huyo ni phd holder wa sheria"..ni kauli za vijembe...na kuonyesha kuogopana!

Cha msingi: Elimu yake akiitumia vizuri itamsaidia kuongoza bunge na kuisaidia nchi ...asijistukie wala kujidefend too much.Na wabunge msijihami sana!

Pia akumbuke hata uwe na degree mia sisi ni wabantu na tunazo tamaduni za kuheshimiana BILA kuvunja sheria na kanuni..aki opt hili credibility yake itapanda zaidi..
 
Huyo mnae mzungumza si ndio huyu hapa

Nakiri wewe ni mwana CCM mwenzangu tena uliyetukuka tu na nakukubali kiutendaji kutokana na sifa zako za kiueledi ulizonazo ila nimekuwa nikikufuatilia kwa jicho langu la tatu la (tai) hasa siku ambazo umekuwa ukishikilia hicho kiti na nimegundua mambo kadhaa ambayo najiuliza je huwa unafanya makusudi tu au labda hujakaa sana na wazee ujifunze jinsi ya kuishi nao?

Sababu iliyonipelekea kuandika uzi huu ni kitendo chako ambacho kinajirudia kila kukicha cha kutowaheshimu wabunge hasa wazee kiumri na ambao nina uhakika kuwa wengi wao wana watoto manjemba (wakubwa) kuliko hata umri wako. Muda si mrefu tu umetoka kumfokea mama yetu mama magreth sitta wakati akiwa anachangia na binafsi nimejisikia vibaya mno.

Rai yangu kwako dada yangu naibu spika wa bunge hebu jaribu basi kuwapa kidogo upendeleo maalum hao wabunge wote wenye umri mkubwa wa CCM na wa UKAWA na tambua kuwa hata kwa umri walionao kidogo huchukua muda mrefu kueleza au kujenga hoja hivyo na wewe wachukulie tu hivyo hivyo.

Naogopa kuna siku atasimama mbunge mwenye uzee kama wa mama Sitta halafu unaweza hata ukamsonya kwa kupoteza muda wakati anajenga hoja zake. Jaribu kuwaonyesha kuwa unawajali na kuwaheshimu kwani nina amini hao wanaweza kuja kuwa msaada mkubwa mno kwako kiutendaji.

Mwisho naomba kukuuliza je hiyo sauti yako ni ndivyo ilivyo tu au una mafua au umeishi sana kwa wakoloni na mabepari?
tulia2.jpg
tulia.jpg
 
Huyu "Betina" ana "academic arrogance" sana..yaani yeye kuwa Dr wa sheria basi anaamini kuwa anajua kila kitu na wengine wote ni mazuzu,hana heshima wala adabu..nashukuru utovu huu wa nidhamu anaufanya hata kwa wabunge wa CCM.Kwanza ana kauli mbaya sana,hata "tone" yake ya kumwambia mtu muda umekwisha ni kana kwamba anaongea na mtoto wa darasa la kwanza,mtu mwenyewe cheo cha "kubebwa".
Nimemfuatilia sana,anawajibu wabunge hovyohovyo bila adabu,anawakaripia tu kama watoto,anaamini yeye ndio mjuwaji wa kila kitu..kweli nimeamini kuwa na elimu dunia sio kuwa na busara...Sijui wamemuokota wapi huyu dada.
umri mdogo+madaraka makubwa= dharau
 
Wana JF ninavyowafahamu wanawake wa Kinyanyusa wana adabu na heshima kweli kweli .Nashindwa kuelewa huyu ni Mnyakyusa wa aina gani mwenye dharau za kupitiliza kiasi hiki.
 
Nakiri wewe ni mwana CCM mwenzangu tena uliyetukuka tu na nakukubali kiutendaji kutokana na sifa zako za kiueledi ulizonazo ila nimekuwa nikikufuatilia kwa jicho langu la tatu la (tai) hasa siku ambazo umekuwa ukishikilia hicho kiti na nimegundua mambo kadhaa ambayo najiuliza je huwa unafanya makusudi tu au labda hujakaa sana na wazee ujifunze jinsi ya kuishi nao?

Sababu iliyonipelekea kuandika uzi huu ni kitendo chako ambacho kinajirudia kila kukicha cha kutowaheshimu wabunge hasa wazee kiumri na ambao nina uhakika kuwa wengi wao wana watoto manjemba (wakubwa) kuliko hata umri wako. Muda si mrefu tu umetoka kumfokea mama yetu mama magreth sitta wakati akiwa anachangia na binafsi nimejisikia vibaya mno.

Rai yangu kwako dada yangu naibu spika wa bunge hebu jaribu basi kuwapa kidogo upendeleo maalum hao wabunge wote wenye umri mkubwa wa CCM na wa UKAWA na tambua kuwa hata kwa umri walionao kidogo huchukua muda mrefu kueleza au kujenga hoja hivyo na wewe wachukulie tu hivyo hivyo.

Naogopa kuna siku atasimama mbunge mwenye uzee kama wa mama Sitta halafu unaweza hata ukamsonya kwa kupoteza muda wakati anajenga hoja zake. Jaribu kuwaonyesha kuwa unawajali na kuwaheshimu kwani nina amini hao wanaweza kuja kuwa msaada mkubwa mno kwako kiutendaji.

Mwisho naomba kukuuliza je hiyo sauti yako ni ndivyo ilivyo tu au una mafua au umeishi sana kwa wakoloni na mabepari?
Mkuu bado kuna wengine wa kuwakumbusha mambo kama haya,binafsi anaposimama mbunge wa Kawe(sikumbuki jina lake)huwa nasikia uoga hata kusikiliza-naona kama communication skills kidogo huwa zinampa shida ingawa ni mzuri wa kujenga hoja.Mfano mzuri ni siku alipokuwa akifanya dhihaka za wazi kwa waziri Dr Mwakyembe bila kujali ni mtu mwenye hadhi ya Baba kwake,na kama haitoshi pia ni mwalimu wake.Ni vyema viongozi wetu wakawa mfano kwetu kwa namna wanavyowasiliana,ilivyo ni kwamba ukiwa ni mtu usiyetambua hadhi ya wenye mamlaka kwako ni lazima nawe itakurudia tu, utadhalilishwa tu somewhere some how.
 
Hata Kama Ni Wa Chama Tawala Ila Naona Kama Vile HAWAHESHIMU Wabunge Saa 12 Jioni ( Wazee ) Mule Hasa Kwa Jinsi Anavyowajibu au Kuwaongelesha. Sidhani Kama MAADILI Ya Kitanzania Anayo Hasa UKIZINGATIA Tokea Chekechea, Shule Ya Msingi, Ya Upili Na Hadi Chuo Kikuu Kasomea MAMTONI Hivyo Hana Habari Na Akina Siye Tuliosomea Shule Zetu Hizi Za SIAMINI KICHEKO.
Gentamycine umekumbushwa dhihaka zako . Umeona sasa ? Hizo ndiyo tabia za wana ccm wote ukiwamo wewe na maneno yako juu ya Lowassa na Mdahalo
 
Mgeyaona wapi kama yasingerushwa live kwenye tv?
 
Mgeyaona wapi kama yasingerushwa live kwenye tv?
 
Huwezi fananisha vijana ccm wasio na midomo ya kuchambua maneno hata Membe mnamtukana ni malezi gani hayo usitake malumbano
 
Back
Top Bottom