GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Nakiri wewe ni mwana CCM mwenzangu tena uliyetukuka tu na nakukubali kiutendaji kutokana na sifa zako za kiueledi ulizonazo ila nimekuwa nikikufuatilia kwa jicho langu la tatu la (tai) hasa siku ambazo umekuwa ukishikilia hicho kiti na nimegundua mambo kadhaa ambayo najiuliza je huwa unafanya makusudi tu au labda hujakaa sana na wazee ujifunze jinsi ya kuishi nao?
Sababu iliyonipelekea kuandika uzi huu ni kitendo chako ambacho kinajirudia kila kukicha cha kutowaheshimu wabunge hasa wazee kiumri na ambao nina uhakika kuwa wengi wao wana watoto manjemba (wakubwa) kuliko hata umri wako. Muda si mrefu tu umetoka kumfokea mama yetu mama magreth sitta wakati akiwa anachangia na binafsi nimejisikia vibaya mno.
Rai yangu kwako dada yangu naibu spika wa bunge hebu jaribu basi kuwapa kidogo upendeleo maalum hao wabunge wote wenye umri mkubwa wa CCM na wa UKAWA na tambua kuwa hata kwa umri walionao kidogo huchukua muda mrefu kueleza au kujenga hoja hivyo na wewe wachukulie tu hivyo hivyo.
Naogopa kuna siku atasimama mbunge mwenye uzee kama wa mama Sitta halafu unaweza hata ukamsonya kwa kupoteza muda wakati anajenga hoja zake. Jaribu kuwaonyesha kuwa unawajali na kuwaheshimu kwani nina amini hao wanaweza kuja kuwa msaada mkubwa mno kwako kiutendaji.
Mwisho naomba kukuuliza je hiyo sauti yako ni ndivyo ilivyo tu au una mafua au umeishi sana kwa wakoloni na mabepari?