Naibu Meya Arusha Ajiuzulu

Huyu naibu Meya nampa BIG up kwani kasoma alama za Nyakati. Ila huyo meya asubiri moto wake uko jikoni.
 
Meya anatakiwa afuate nyayo za naibu wake ajiuzulu. Kama anajihamini warudie uchaguzi na agombee tena tuone kama atashinda.
 
Kutokana na mauaji yaliyotokea Arusha hivi karibuni Naibu Meya wa jiji la Arusha bwana Kivuyo amejiuzulu wadhifa huo. Source: radio one breaking news.

Ameshasababisha mauaji ndo anajiuzulu. Mungu atamlipizia yeye na CCM yake...
 
Kutokana na mauaji yaliyotokea Arusha hivi karibuni Naibu Meya wa jiji la Arusha bwana Kivuyo amejiuzulu wadhifa huo. Source: radio one breaking news.
wameanza hao mwingie atafuata sasa hv walikua wanategeana nani aanze!kwasababu rafu inaonekana wazi kabisa ilichezwa iweje diwani wa Tanga aje apige kura Arusha na bado viongozi wanabariki uchaguzi hata hivyo pamoja na kujihudhuru damu za waliokufa zitalipwa vipi bado dhambi ipo palepale ndio maana huwa tunasema kwamba unapotaka kua kiongozi bora nafsi yako itoke ndani mwako na sio kwa shinikizo la nje kivuyo inaelekea kawaza sana baada ya tukio la juzi akaona kikombe hiki kitamsuta siku moja kwa mwenyezi mungu ila hongera kwa kujihudhuru maana ni wachache sana wenye moyo kama huo na kwa tz inawezekana 0.1%
 
Kutokana na mauaji yaliyotokea Arusha hivi karibuni Naibu Meya wa jiji la Arusha bwana Kivuyo amejiuzulu wadhifa huo. Source: radio one breaking news.

Kama kweli amejiuzulu basi ni MUUNGWANA.
 
Uchaguzi ulimweka madarakani ulikuwa batili sasa hakua na haki ya kujiuzuru alitakiwa kuukana huo unaibu meya aliopewa na ccm, kusema anajiuzuru ni kuhalalisha uchaguzi batili, tuseme ameukana unaibu meya wake batili
 
Huyo naibu meya mnafiki tu baada ya kushiriki dhambi ya ubakaji wa demokrasia iliyopelekea kufa kwa ndugu zetu na kugundua nguvu ya umma ambayo hata askari hawakutosha ndio anazinduka,kachelewa.
Wanazidi kupungua tu ushindi unakaribia na hilo jinamizi litawatesa sana.
 
Safi kabisa aache kuwajibika kwa serikali ya wauwaji maana kila siku tunashuhudia duniani kote watu wana andamana lakini hawauliwi tena hata wale ambao wana andamana bila kibali nao pia sija wahi kuona wakiuliwa zaidi ya kutulizwa kwa ustarabu.SHAME ON YOU JK
 
Ndugu Maiko Kivuyo kutoka TLP Hongera sana na jiunge na madiwani wa Chadema, Hivi ndivyo inatakiwa ili nguvu ya polisi wabaki wanaangaliana,lazima sheria zifuatwe na uchaguzi ufanyike upya wa umeya
 
Laiti ccm wangekuwa wana masikio na wawe wanasikia kweli au kuwa na macho na waone kinachotokea nchini; wasingeendelea kudai kuwa wana ridhaa ya wananchi kutawala tena!!! jinsi siku zinavyokwenda wanaendelea kupoteza imani kwa wananchi hata kwa wanachama wao!! Nina hakika hata baadhi ya wajumbe wa baraza la mawaziri wa sasa wa Kikwete hawana imani naye achilia mbali wananchi wa kawaida.
 
Safiiiii safi sana Bado MKWERE mwaka huuu lazima achiie ngazi au adondoke:A S-confused1:
 
Huo ndio uwajibikaji KIVUYO usikubali kungangania cheo kinachonuka damu epuka laana ndugu kumbuka mbinguni huendi na cheo na utaenda kujibu mauaji uliyosababisha
 
Huyo Naibu Meya hakuna kitu. Kwa nini alikubali kuwa na CCM wakati anajua ucghchuzi haukuwa wa huru na haki. Huyo ni bendera fuata upepo na tena inaelekea ana njaa sana na pesa za mafisadi


Tunashukuru kwa kujiuzulu ila ujue we ni **** tu
 
Back
Top Bottom