Ilushenisti
Senior Member
- Mar 11, 2013
- 118
- 46
Ni kitambo toka niibuke hapa jamvini, mara chache nimekuwa naingia kama guest hata id yangu imepotea nimelazimika kutengeneza mpya. Nimekuja vile nina jambo nataka kuitangazia dunia, "ninatembea na mke wa mtu na sijutii kabisa hili"
Si jambo la kujivunia hata kidogo na wala la kupigia mfano, vijana wadogo hapa wasilichukulie hivyo, usinihukumu kabla ya kufika mwisho wa thread hii.
Ni hivi ilikuwa enzi za ujana mchanga, nilikuwa na miaka kama ishirini hivi kipindi hicho. Nilimpenda sana huyu binti na alikuwa mpenzi wangu wa kwanza. Tulikubaliana hakuna kukutana kimwili hadi ndoa na mimi nilikuwa tayari kwa hilo nilimpenda sana huyu binti na hata sitaki kupenda tena kama vile. Shida ilikuja wakati tunakwenda vyuoni tukapangiwa vyuo tofauti mikoa tofauti.
Huyu binti alisaliti penzi letu na nilijua kwa namna ambayo ilinisababishia maumivu makubwa sana. Kilichoniumiza zaidi miezi kama sita baada ya kujua ukweli na kuachana binti alirudi akiomba msamaha, alidai hajui aliteleza vipi na bado ananipenda sana, japo bado nilikuwa na mapenzi naye sikuwa tayari kwa hilo, nikamwambia hapana mama nenda ukweli ni kwamba bado nakupenda sana ila kamwe hatuwezi tena kuwa wapenzi.
Jamaa aliyemchukua alionekana mstaarabu sana na pamoja na yote nilimheshimu jamaa nikaamua ntakaa mbali na huyu binti na kuheshimu uhusiano wao. Binti alipomaliza chuo akaoana na jamaa na hadi harusi nilialikwa na nikaenda, inaumiza moyo ila nilikwenda. Baada ya hapo nilijitahidi sana kukata mawasiliano yote na binti yule, japo alijaribu sana mwanzoni na maisha yakaendelea kwa upande wangu.
Mwaka jana mwanzoni nikakutana na rafiki yangu mmoja ambaye alinifahamu mimi na huyu binti na alijua uhusiano wetu, walisoma chuo kimoja na huyu binti. Jamaa akanipa habari ambayo sikuwahi kuwazia kabisa! Ni hivi huyu jamaa aliyenipora huyu binti alicheza mchezo mchafu. Kumbe binti alipofika tu chuoni jamaa akamwona alimzimia akaanza kufanya mkakati wa kumpata.
Binti aliamwambia ana jamaa yake na jamaa yake mwenyewe ni mimi, huyu ndugu akaanza kunifuatilia, hakuwa akunifahamu lakini alikuwa na marafiki chuo nilichokuwepo na alifanikiwa kupata habari za kutosha kuhusu mimi. Kwa ujuzi wa hali ya juu jamaa akachukua taarifa za ukweli na tutengeneza uongo ambao kwa kiasi kikubwa sana ulifanana na ukweli, aliutumia kuniponda kiaina kwa huyu binti ikionesha kuwa sikuwa mkweli, sikuwa serious na mapenzi yetu, kwa kifupi alitumia madhaifu madogo madogo akayakuza kwa uongo wa kitaalamu hadi akaushinda moyo wa binti huyu nikaonekana sifai, hili lilifanyika kwa dozi ndogo ndogo sana ambapo mwisho wa siku sumu ilitosha kuua.
Njia aliyotumia ilikuwa kujiweka rafiki wa karibu na huyu binti, wakati binti anashtuka alikuwa ameshachelewa. Mbaya zaidi aliwatumia watu niliodhani ni marafiki zangu wa karibu kunichimba!
Nilipojua ukweli japo miaka mingi imepita maumivu yalirudi upya, kilichoniuma zaidi ni kwamba jamaa nilimheshimu, nilidhani ni mtu mstaarabu, alinidanganya mimi kama alivyomdanganya huyu binti.
Ni ngumu kusema maumivu yapi ni makubwa zaidi, ya kunyang'anywa msichana niliyempenda ua ya kudanganywa na kutokujua. Nikufikiri jamaa alivyokuwa anajifanya mstaarabu na muungwana mbele yangu, huyu ni nyoka. Mimi najifahamu, mi ni mkora ila naweza kuwa mstaarabu nikikutana na watu wastaarabu na dawa ya mtu mshenzi ni ushenzi tu.
Baada ya kuufahamu ukweli nikaweka azimio moja, nitalipiza kisasi, na namna nzuri ya kufanya hivyo ni tutembea na mke wa jamaa (my ex girlfriend). Nilianza taratibu mwezi wa tano mwaka jana kurudisha mawasiliano na mke wake, haikuwa ngumu kwa vile pamoja na miaka kadhaa kupita bado kuna hisia kati yetu! Ikafika hatua tunawasiliana kila siku hata mara tano kwa siku, akanieleza mambo mengi sana sitaki kuyaweka hapa, sikuwahi kumtamkia namtaka kimapenzi wala sikuhitaji kufanya hilo, mambo yalikuwa yanatokea tu.
Bado nilikuwa nasita, labda kwa sababu pamoja na maovu mengi niliyofanya sijawahi tembea na mke wa mtu nikijua fika ni mke wa mtu, nina kanuni zangu maishani ambazo ni ngumu kuzivunja. Nilikuwa nakwepa kukutana naye, tupo miji tofauti. Mwezi wa kumi mwaka jana nilikuwa Zanzibar kwa kazi ya siku mbili, nikaamwambia nimwarifu naelekea Zanzibar ananiambia na yeye anakuja kikazi next day. Nilikuwa na maswali mengi, mbona hakuwa ameniambia angekwenda Zanzibar kikazi? Siku zote alikuwa ananiambia kila kitu ratiba zake ninazo kuliko hata mume wake! Naam alifika siku iliyofuatia jioni, tulikula chakula cha jioni pamoja, vinywa vyetu havikuongea sana tukiwa pale mezani, ila miili yetu, macho yetu yalisema kila kitu, nikabaini bado nampenda sana huyu binti.
Nikapendekeza tunyooshe miguu mchangani, tukatoka pale hotelini na kuanza kutembea mchangani, hatukwenda hata mita kumi tukajikuta tumeng'ang'aniana kama luba, miili yetu ilikuwa na kiu fulani na kulikuwa na namna moja tu ya kuikata. Siku hii tulilala pamoja hotelini kwangu hadi asubuhi, sijui kama tulilala au tulikesha! Asubuhi akanieleza ukweli hakuwa na kazi Zanzibar! alichofanya ni kuhamia hotelini kwangu, nikamaliza shughuli yangu Zanzibar nikaongeza siku nyingine mbili na huyu bibie.
Tumeendelea na mapenzi haya na jamaa kashaanza kushtuka, kibaya zaidi binti ananiambia anataka mtoto wangu, kwamba ni kitu anachokiota sana. Upande mmoja najisikia vibaya kumtumia kama chombo cha kulipiza kisasi japo nampenda kiukweli ila hakuna kitu kuzuri kinachonifurahisha kama jamaa anapopiga simu niko na mkewe.
Nampigaga loud speaker alafu naenjoy jinsi anavyolalamika kuwa hamwelewi mkewe hamwelewi mkewe eti amebadilika sana. Pamoja na kuwa mambo hayako shwari kati yao eti huko nyuma angalau alikuwa rafiki mzuri, analalamika siku huzi akisafiri mawasiliano anakata kabisa, simu akipiga ni shida kupokelewa (itapokelewa vipi wakati mkewe anapewa anafurahia mapenzi kwa mara ya kwanza katika maisha yake?) Nikifikiri jinsi alivyozunguka na kuwatumia hata watu niliodhani ni marafiki zangu kunipindua kifidhuli naona ni sawa yake kabisa. Nikifikiri jamaa lilivyokuwa linajifanya listaarabu kwangu na lina heshima kumbe lilikuwa linanichimba naona hii ndio adhabu sawa sawa.
Navyoandika nimetoka kumsindikiza uwanja wa ndege mwanza, anarudi Dar baada ya kuwa pamoja kwa siku tano, Ni siku za kukumbukwa, kati ya vitu ambavyo nimeshindwa kuelewa ni jambo aliloniambia, hajafanya mapenzi na mume wake toka nilipoanza kuwasiliana naye, anasema hajawahi kumpenda na imekuwa kama adhabu kuishi na jamaa.
Anasema jamaa anampenda sana na anajitahidi kuwa mume bora ila moyo umeshindwa kumpenda. Tulipiga mechi ya kufa mtu kabla hajaondoka, tulipomaliza akasema jambo ambalo bado linanifikirisha sana. Anataka kuachana na jamaa, anasema anaelewa itakuwa ngumu kwangu kumwamini na kuwa na uhusiano kama zamani, hategemei ndoa kutoka kwangu, anataka tu tuwe na uhusiano wa kimapenzi hata bila ndoa ila nimhakikishie hakutakuwa na mwanamke mwingine.
Materially hakuna anachotegeme toka kwangu maana she is doing much better than me! Amewekeza sana kwenye ardhi ila hajajenga, mumewe hajui ni kama amekuwa na mpango wa muda mrefu wa kutoka kwenye ndoa hii. Nikimtizama naona bado ni Yule inosenti geli, (labda penzi linanipofua) anadai hakuwahi kutembea nje ya ndoa kabla lakini ndani ya moyo wake aliamini angetokea siku tukarudiana, tukiwa wapenzi hautukuwahi kukutana kimwili lakini anadai hata baada ya kuolewa amekuwa anatamani hilo litokee.
Nina rafiki wa kike wa muda wa kama miaka miwili na nusu ila tumepishana kuhusiana na vipaumbele vyetu tukakubalia tupeane muda tukae mbali maana kila mtu anashikilia msimamo wake! Sifikirii kuoa, nina watoto wawili wa kike mapacha, (niliwapata nilipozibuka baada ya kuachana na huyu binti enzi hizo) wananitosha kabisa na ndio kitu cha kwanza kabisa maishani kwangu.
Nafikiria sana uhusiano huu unaelekea wapi ila kama kuna jambo moja ambalo halinisumbui akili ni dhamira yangu japo natembea na mke wa mtu na mumewe analalamika sana, anahisi anachukuliwa mali zake ila anastahili kabisa!
Soma lakini usinihukumu.