Nahodha: Sijui DCI Manumba alikoitoa ripoti ya Mwakyembe !! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nahodha: Sijui DCI Manumba alikoitoa ripoti ya Mwakyembe !!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Matola, Feb 28, 2012.

 1. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Waziri wa Mambo ya Ndani,Shamsi Vuai Nahodha  • ASEMA UCHUNGUZI BADO UNAENDELEA NA MATOKEO ATATANGAZA YEYE, ATAKA MANUMBA AULIZWE MWENYEWE CHANZO CHA TAARIFA YAKE

  Ramadhan Semtawa

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha amesema uchunguzi kuhusiana afya ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe bado unaendelea na ni yeye atakayetangaza matokeo ya kama alipewa sumu au la baada ya kukamilika huku akiikana ripoti iliyotolewa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Kamishna, Robert Manumba.

  Hii ni mara ya kwanza kwa Nahodha kutoa tamko hilo tangu kuibuka kwa mjadala kuhusu afya ya Dk Mwakyembe hasa baada ya DCI Manumba kuutangazia umma kwamba ripoti kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inaonyesha kuwa Naibu Waziri huyo hakulishwa sumu, kauli ambayo ilipingwa na Waziri mwenye dhamana ya Afya, Dk Haji Mponda na Dk Mwakyembe mwenyewe.

  Akizungumza katika mahojiano maalumu ofisini kwake Dar es Salaam jana, Nahodha alisema uchunguzi kuhusu afya ya Dk Mwakyembe ni wa kisayansi na hauwezi kufanyika ndani ya wiki mbili au mwezi.

  "Ninachosema ni kwamba uchunguzi nilioutangaza bado unaendelea," alisema na kuongeza: Sasa mimi nimetangaza matokeo ya uchunguzi? Mimi ndiyo Waziri nasema uchunguzi bado unaendelea na mimi ndiyo nitatangaza hitimisho la jambo hilo."

  Alisema suala la Dk Mwakyembe ni zito na siyo la mtu kukurupuka kwani linagusa hisia za watu na kutahadharisha baadhi ya watu wanaojaribu kulifanya jepesi wanachezea kitu hatari.

  "Ndiyo maana nasema ni jambo linalohitaji weledi wa hali ya juu katika kulichunguza. Ni jambo zito la kisayansi, naomba nipewe muda ili uchunguzi nilioagiza ufanyike kwa kina. Nasisitiza ni jambo linalohitaji weledi wa kisayansi."

  Waziri Nahodha alisema uchunguzi huo unafanyika kwa kuhusisha jopo la wataalamu wa sayansi hivyo kuwataka Watanzania kutambua kwamba uchunguzi huo unaendelea na ni vigumu kutamka utakamilika lini.

  Kuhusu ripoti ya DCI

  Alipoulizwa ni kwa nini asimchukulie DCI Manumba hatua kwa kutoa tamko wakati uchunguzi alioagiza haujakamilika alisema: "Ndiyo maana nasema, uchunguzi wa suala hili unaendelea. Sasa hatima yote hayo unayozungumza nasema nipeni muda."

  Alipoulizwa ni wapi DCI Manumba alipata ripoti ya Dk Mwakyembe wakati mgonjwa mwenyewe na Waziri wa Afya wameikana, alijibu: "Sasa, hilo ni vyema ukamtafuta yeye mwenyewe DCI aseme. Mtafute aseme yeye na Waziri wa Afya, hao watu wawili wanaweza kuzungumzia ripoti hiyo, lakini mimi nasema uchunguzi wa jambo hili la Dk Mwakyembe ni wa kisayansi na bado unaendelea."

  Alisema alichokisema DCI Manumba kinaweza kuwa na msingi ambao anaujua mwenyewe hivyo, ni vyema akaulizwa yeye kuhusu undani wa ripoti yake huku akisisitiza: "Mimi ninavyoliangalia jambo hili la Dk Mwakyembe linahitaji umakini wa hali ya juu katika kulishughulikia. Hilo la DCI mtafute mwenyewe akueleze."

  Nahodha pia hakutaka kuzungumzia suala hilo kwa undani hata pale alipoulizwa ikiwa haoni kwamba kukanwa kwa kiwango hicho kikubwa kwa ripoti ya DCI Manumba kunawafanya wananchi waanze kutilia shaka utendaji kazi wa jeshi la polisi.

  Hata hivyo, alipoulizwa jana kuhusu kukanwa kwa ripoti yake na mawaziri, akiwemo wa Mambo ya Ndani ambayo ndiyo wizara mama inayosimamia Jeshi la Polisi, DCI Manumba alisema kimsingi hawezi kujibizana na waziri yeyote kwani kufanya hivyo itakuwa ni utovu wa nidhamu katika utumishi wa umma.

  Alisema alichokifanya ni kuandaa jalada ambalo tayari liko kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ambaye kwa mamlaka na utaalamu wake wa kisheria, ataamua cha kufanya baada ya kulipitia.

  "Siwezi kujibizana na waziri wangu au waziri yeyote. Kama amesema uniulize mimi, ninachoweza kusema ni kwamba tayari nimeandaa jalada liko kwa DPP. Sasa nikianza kuzungumza hili au lile itakua haina maana watu watasema nimeanza kujitetea," alisema.

  DCI, Dk Mwakyembe na Dk Mponda

  Akizungumza na waandishi wiki mbili zilizopita, DCI Manumba alisema: "Ukweli kuhusu kauli hiyo inayodai kuwekewa sumu, tumeupata baada ya kuwasiliana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ambayo nayo imewasiliana na hospitali aliyokuwa amelazwa Dk Mwakyembe nchini India. Taarifa zinaonyesha kuwa hakuna sumu."

  "Hatua zaidi zinachukuliwa dhidi ya jambo hilo, kwa sasa litashughulikiwa kwa kufuata misingi ya kisheria," alisema Manumba.

  Hata hivyo, siku moja baada ya kauli hiyo ya DCI Manumba, Dk Mwakyembe alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akisema: "Napata tabu kuamini kama DCI Manumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matibabu yangu au walisoma taarifa ‘nyingine' na kama waliisoma taarifa hiyo wenyewe au ‘walisomewa!'

  "Nasema hivyo kwa kuwa alichokisema DCI Manumba kwa waandishi wa habari, hakifanani kabisa na picha iliyoko kwenye taarifa halisi ya Hospitali ya Apollo inayotamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow (uboho) kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukijua, kukidhibiti au kukiondoa huku vyombo vyetu vya dola vikipelekeshwa na mafisadi kusema bila msingi wa kisayansi wala aibu: "Hakulishwa sumu", "hakulishwa sumu."

  Dk Mwakyembe pia alitoa sababu kuu tatu za kupinga ripoti ya DCI Manumba: "Kwanza kwa kuingilia mchakato wa matibabu yangu na uchunguzi wa kina kuhusu kiini chake, unaoendelea katika Hospitali ya Apollo, India ambako bado sijahitimisha matibabu yangu, pili kwa ufinyu wa uelewa unaojitokeza bayana kwenye tamko la Jeshi la Polisi unaosisitiza kuwa ‘sikunyweshwa sumu' wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru, inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa tu.

  Tatu ni kitendo cha Polisi kujiingiza kwenye suala ambalo kwa takriban mwaka mzima sasa, halijawahi kuwa na dhamira ya dhati ya kulielewa au kulichunguza mbali na kulifanyia mzaha kupitia magazetini.

  Januari 19, mwaka huu gazeti hili pia lilifanya mahojiano maalumu na Waziri Mponda ambaye naye alisema kwa utaratibu, ripoti ya daktari ni ya mgonjwa... "Sisi hatujaandika ripoti, muulizeni DCI Manumba awape ufafanuzi."

  Alisema wanaoweza kuzungumzia maradhi ya Dk Mwakyembe ni familia yake au yeye mwenyewe kwani ndiye mwenye ripoti. Lakini wizara haiwezi kufanya hivyo.

  CHANZO: Mwananchi
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Feb 28, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  'Em clowns!
  They love clowning
  We gonna make a move
  "A Clown who Clowned US"!
   
 3. Bwa'Nchuchu

  Bwa'Nchuchu JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,178
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Teh teh teh...

  Washaanza kutupiana mpira :lol::lol:
   
 4. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2012
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  This guy (Manumba) is so paranoid. Sijui hata u DCI aliupataje!
   
 5. Freeland

  Freeland JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 14,468
  Likes Received: 6,761
  Trophy Points: 280
  Te teh teh,hi hi hi hi,kwi kwi kwi.Patamu hapaaaa.Episode No........
   
 6. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280
  Hizo ndio teuzi za Jakaya Kikwete. hiyo ofisi Adadi Rajabu ndio alifit na sio huyu jamaa.
   
 7. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #7
  Feb 28, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  :A S embarassed::shock::eyebrows::lol::lying::eyeroll1::A S-confused1::behindsofa:


  I better go :fish2:
   
 8. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #8
  Feb 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280
  ........to fish!!!
   
 9. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Serikali ya JK na mfumo wake wa chama cha magamba ni zaidi ya "Ze Komedi"! Mara ikulu iseme hivi, Mtoto wa mkulima aibuke na lake, Waziri agutuke usingizini kivyake, Spika naye alete za kariakoo kivyake vyake, naibu wake naye kiaina. Mmmmh! Hivi wanatuona hamnazo sana eeh!
   
 10. Mpiga Nyoka

  Mpiga Nyoka JF-Expert Member

  #10
  Feb 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  kurukaruka ndio kuiva kwa maharage! Ok bye..
   
 11. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #11
  Feb 28, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Huyu mzee anakurupukaga huyu!!!Kwa kweli serikali ya JK imejaa mibabaishaji mweh! Sijui kwanini JK kaamua kuteua watu kuja kufanya mazoezi ya kuongoza kwenye serikali yake.

  Badala ya kufanya maamuzi naye anatoa mlio. Ila katika hili sekeseke la Mwakyembe naye amepoteza sifa ya kuongea na Wananchi mana naye ripoti ya Manumba inamhusu na alishagaongea hovyo huko nyuma kuhusu ishu Hii.

  Aidha, kwa kuwa Manumba yupo kwenye ofisi yake tunaamini kabla ya manumba kuutangazia umma upuuuuzi aliotutangazia, aliwasiliana na mabosi zake IGP na Waziri mwenye dhamana. So asijikoshe, atulie tu kama ananyolewa, si tushamuelewa anachotaka kusema!!
   
 12. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #12
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Nilishasahau, hivi hiki "Kichekesho" kimeingia sehemu ya ngapi sasa?
  PAZIA LIMEFUNGWA....UTAENDELEA WIKI IJAYO
   
 13. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #13
  Feb 28, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Hili jambo limefika mahali kila ndege mjanja anaepusha ubawa wake. Walijaribu kupima kina cha maji, ni wazi sasa wanafahamu kuwa wakati wa kudanganyana umepita kitambo sana na kila mtu atabeba mzigo wake bila kuoneana haya.

  JF walisema yapo mengi kuanzia ofisini. Ukisoma maneno ya Mwakyembe kuna sehemu amesema ' uchunguzi huo ulifanyikaje bila kuanzia katika ofisi.....'. Hapo ninakumbuka yale yaliyoandikwa JF na wengine kuyaita uzushi.

  Tumeambiwa kuwa ile ni taarifa ya serikali na inabidi tuikubali na hakuna haja ya kufikiri au kupembua!!!!
  Wizara ya Afya imekana, Wizara ya mambo ya ndani imekana, Ofisi ya waziri mkuu ikasema haina taarifa.

  DCI wa Tanzania R.Manumba amebaki peke yake akiwakilisha kundi lingine na si serikali.
  Taarifa yake ni ya uchunguzi alioufanya yeye na 'wenzake' na hakuna mkono wa serikali.

  Utata unaojitokeza unashadidia hofu aliyo nayo Dr Mwakyembe na umma wa Tanzania kuhusu hujuma.
  Kinachoshangaza zaidi ni kusikia eti faili amepeleka kwa DPP. Swali ni kuwa ikiwa anajua ni ugonjwa 'wa ngozi' na hakulishwa sumu faili ni la nini? Hivi wagonjwa wa malaria wanafunguliwa mafaili kwa DPP!!

  Tutaendelea kutumia fikra zetu kutafuta jibu hata kama ni miaka dahari. Tuunganishe dot na dash kidogo.
  DCI anatumiwa! Mwanasheria mkuu mstaafu, kiongozi aliyejiuzulu na mfanyabiashara!
  Hadi tutakaposikia taarifa ya wataalamu wa India anakotibiwa Dr, watuhumiwa watabaki na tuhuma.
   
 14. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #14
  Feb 28, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Ndio viongozi hawa wanaomuongoza Jk yaani kila mtu na kauli yake,na huyu Nahodha anashangaza kweli kwani huyu DCI alitakiwa ampige chini mara moja kwa sababu kuna waTz waliumizwa/wanaendelea kuumizwa na kauli za hovyo za viongozi wenye dhamana ya Usalama wa Raia,serikali ya ajabu kweli hii sijapata iona
   
 15. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #15
  Feb 28, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha"Wamekwishaanza"
   
 16. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #16
  Feb 28, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  huyu Nahodha kidogo ana make sense kulingana na maelezo yake..
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Feb 28, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,619
  Trophy Points: 280
  Mkuu Nguruvi3, kusema ukweli hawa jamaa wanatuzeveza tuu na kujibaraguza!.

  1.Nikianzia na taarifa ya DCI Manumba, japo sasa wote wanamruka, yeye alitoa taarifa ya kilichopo, " a bird in the hand worth two in the bush". Amini nawaambieni, Dr. aliporejea kutoka Apollo amekuja na complete medical report ya kilichopo!. Report hiyo iko serikalini, Dr. Mponda anajua, Nahodha anajua na JK aliisoma kwenye kikao cha Cabinet!. Hivyo DCI hakuzusha kitu and infact kazi yake ya awali alishamaliza, report yake iko kwa DPP kusubiri uamuzi zaidi.

  2. Waziri wa Afya Dr. Haji Mponda ni muongo mkubwa na mnafiki kujifanya serikali haina report hiyo bali aliyenayo ni mgonjwa mwenyewe tuu!. Huu ni uongo mtakatifu unaofaa kuwadanganya watoto na humu jf tuna watoto kibao wa kifikra wakindanganywa tuu hata kwa issie ndogo, wanadanyanyika!.

  3. Alichotakiwa kusema ni ukweli kuwa ripoti hiyo ipo ila ni personal report mgonjwa ndio mwenye full rights za disclosure na sio DCI Manumba!. DCI Manumba alitakiwa aseme uchunguzi wa awali wa kipolisi umebaini hakutiliwa sumu bila kui site report ile!.

  4. Waziri Nahodha sasa ndio amekwenda deep, hapa sasa ndio tumepewa kitu kipya, kumbe ameagiza uchunguzi mpya wa forensic ya kubaini jinai ya sumu!. Tangu ameanza kuumwa hadi kupelekwa Apollo hakukufanyika forensic investigation yoyote sasa ndio Nahodha kaagiza ifanyike na ripoti hiyo ataitoa yeye Nahodha.

  This is something new and something else!. DCI Manumba alishatimiza wajibu wake na jalada liko kwa DPP, lakini kwa sababu waziri sasa ndio kaagiza uchunguzi mpya, jalada litarudi kwa DCI lipelekwa kwa watu wa forensic na hata Apollo sasa ndio wataarifiwa kuwa uchunguzi kwa mgonjwa huyo sio just the ordinary medical report bali ni forensic investigation ambayo ni kazi ya kipolisi na sio ya kidakitari, hata hao Apollo hivyo vipimo sasa watavipeleka kwa watu wao wa forensic for certification just in case kesi itatinga mahakamani!.

  5. Kunapotokea ubishani kama huu unaohusisha hard facts, kama unaamini kwenye ukweli, unasimama na ukweli huo unaouamini hata kama utabaki peke yako kwenye ukweli huo kama Yesu alivyosulubiwa kwa kusimama kwenye kweli. DCI Manumba pia ataishia kusulubiwa ili serikali ijikoshe kuwa atleast sasa it is doing something kwenye tuhuma za Mwakyembe ambaye alizifikisha kwa IGP Mwema na wakuu wote wakiwemo Tiss, Waziri hadi Ikulu na alipeleka copy kwa baadhi ya wanabalozi just incase something inge imtokea kabla uchunguzi haujafanyika!. Tiss walimpuuza, IGP alimpuuza na kila mhusika walimpuuza only wanabalozi walikuwa concerned ila hawakuweza kuingilia kati kwa sababu haya ni mambo ya ndani!.

  Wajameni Mnyonge tumnyongeni ila haki yake, mpeni!.

  Pasco.
   
 18. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #18
  Feb 28, 2012
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hatuna serikali makini, tuna genge la wanaojiita viongozi wa serikali wasiojua uwajibikaji ni nini. Chama legelege huzaa serikali legelege.

  Rais legelege huongoza serikali legelege.
   
 19. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #19
  Feb 28, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  sinema ya starring kuzaliwa na kufa kwny bustan.
  Wao cheun hu.
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Feb 28, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,619
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ngumijiwe, sio kidogo ana make sense, he is making all the senses kwa sababu hii ndio mara ya kwanza serikali imekiri inafanya uchunguzi wa kipolisi na uchunguzi huu sio tuu utahusu uwezekano wa kupewa sumu bali madai yote ya Mwakyembe ambayo huko nyuma waliyapuuza!.
   
Loading...