Nahodha: Sijui DCI Manumba alikoitoa ripoti ya Mwakyembe !!

Nahodha: Sijui DCI Manumba alikoitoa ripoti ya Mwakyembe !!

Nahodha: Sijui DCI Manumba alikoitoa ripoti ya Mwakyembe



WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha amesema uchunguzi kuhusiana afya ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe bado unaendelea na ni yeye atakayetangaza matokeo ya kama alipewa sumu au la baada ya kukamilika huku akiikana ripoti iliyotolewa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Kamishna, Robert Manumba.

Hii ni mara ya kwanza kwa Nahodha kutoa tamko hilo tangu kuibuka kwa mjadala kuhusu afya ya Dk Mwakyembe hasa baada ya DCI Manumba kuutangazia umma kwamba ripoti kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inaonyesha kuwa Naibu Waziri huyo hakulishwa sumu, kauli ambayo ilipingwa na Waziri mwenye dhamana ya Afya, Dk Haji Mponda na Dk Mwakyembe mwenyewe.

Akizungumza katika mahojiano maalumu ofisini kwake Dar es Salaam jana, Nahodha alisema uchunguzi kuhusu afya ya Dk Mwakyembe ni wa kisayansi na hauwezi kufanyika ndani ya wiki mbili au mwezi.

“Ninachosema ni kwamba uchunguzi nilioutangaza bado unaendelea,” alisema na kuongeza: Sasa mimi nimetangaza matokeo ya uchunguzi? Mimi ndiyo Waziri nasema uchunguzi bado unaendelea na mimi ndiyo nitatangaza hitimisho la jambo hilo.”

Alisema suala la Dk Mwakyembe ni zito na siyo la mtu kukurupuka kwani linagusa hisia za watu na kutahadharisha baadhi ya watu wanaojaribu kulifanya jepesi wanachezea kitu hatari.

“Ndiyo maana nasema ni jambo linalohitaji weledi wa hali ya juu katika kulichunguza. Ni jambo zito la kisayansi, naomba nipewe muda ili uchunguzi nilioagiza ufanyike kwa kina. Nasisitiza ni jambo linalohitaji weledi wa kisayansi.”


Waziri Nahodha alisema uchunguzi huo unafanyika kwa kuhusisha jopo la wataalamu wa sayansi hivyo kuwataka Watanzania kutambua kwamba uchunguzi huo unaendelea na ni vigumu kutamka utakamilika lini.

Kuhusu ripoti ya DCI

Alipoulizwa ni kwa nini asimchukulie DCI Manumba hatua kwa kutoa tamko wakati uchunguzi alioagiza haujakamilika alisema: “Ndiyo maana nasema, uchunguzi wa suala hili unaendelea. Sasa hatima yote hayo unayozungumza nasema nipeni muda.”

Alipoulizwa ni wapi DCI Manumba alipata ripoti ya Dk Mwakyembe wakati mgonjwa mwenyewe na Waziri wa Afya wameikana, alijibu: “Sasa, hilo ni vyema ukamtafuta yeye mwenyewe DCI aseme. Mtafute aseme yeye na Waziri wa Afya, hao watu wawili wanaweza kuzungumzia ripoti hiyo, lakini mimi nasema uchunguzi wa jambo hili la Dk Mwakyembe ni wa kisayansi na bado unaendelea.”

Alisema alichokisema DCI Manumba kinaweza kuwa na msingi ambao anaujua mwenyewe hivyo, ni vyema akaulizwa yeye kuhusu undani wa ripoti yake huku akisisitiza: "Mimi ninavyoliangalia jambo hili la Dk Mwakyembe linahitaji umakini wa hali ya juu katika kulishughulikia. Hilo la DCI mtafute mwenyewe akueleze.”

Nahodha pia hakutaka kuzungumzia suala hilo kwa undani hata pale alipoulizwa ikiwa haoni kwamba kukanwa kwa kiwango hicho kikubwa kwa ripoti ya DCI Manumba kunawafanya wananchi waanze kutilia shaka utendaji kazi wa jeshi la polisi.

Hata hivyo, alipoulizwa jana kuhusu kukanwa kwa ripoti yake na mawaziri, akiwemo wa Mambo ya Ndani ambayo ndiyo wizara mama inayosimamia Jeshi la Polisi, DCI Manumba alisema kimsingi hawezi kujibizana na waziri yeyote kwani kufanya hivyo itakuwa ni utovu wa nidhamu katika utumishi wa umma.

Alisema alichokifanya ni kuandaa jalada ambalo tayari liko kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ambaye kwa mamlaka na utaalamu wake wa kisheria, ataamua cha kufanya baada ya kulipitia.

“Siwezi kujibizana na waziri wangu au waziri yeyote. Kama amesema uniulize mimi, ninachoweza kusema ni kwamba tayari nimeandaa jalada liko kwa DPP. Sasa nikianza kuzungumza hili au lile itakua haina maana watu watasema nimeanza kujitetea,” alisema.

DCI, Dk Mwakyembe na Dk Mponda

Akizungumza na waandishi wiki mbili zilizopita, DCI Manumba alisema: “Ukweli kuhusu kauli hiyo inayodai kuwekewa sumu, tumeupata baada ya kuwasiliana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ambayo nayo imewasiliana na hospitali aliyokuwa amelazwa Dk Mwakyembe nchini India. Taarifa zinaonyesha kuwa hakuna sumu.”

“Hatua zaidi zinachukuliwa dhidi ya jambo hilo, kwa sasa litashughulikiwa kwa kufuata misingi ya kisheria,” alisema Manumba.

Hata hivyo, siku moja baada ya kauli hiyo ya DCI Manumba, Dk Mwakyembe alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akisema: "Napata tabu kuamini kama DCI Manumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matibabu yangu au walisoma taarifa ‘nyingine’ na kama waliisoma taarifa hiyo wenyewe au ‘walisomewa!’

“Nasema hivyo kwa kuwa alichokisema DCI Manumba kwa waandishi wa habari, hakifanani kabisa na picha iliyoko kwenye taarifa halisi ya Hospitali ya Apollo inayotamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow (uboho) kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukijua, kukidhibiti au kukiondoa huku vyombo vyetu vya dola vikipelekeshwa na mafisadi kusema bila msingi wa kisayansi wala aibu: “Hakulishwa sumu”, “hakulishwa sumu.”

Dk Mwakyembe pia alitoa sababu kuu tatu za kupinga ripoti ya DCI Manumba: “Kwanza kwa kuingilia mchakato wa matibabu yangu na uchunguzi wa kina kuhusu kiini chake, unaoendelea katika Hospitali ya Apollo, India ambako bado sijahitimisha matibabu yangu, pili kwa ufinyu wa uelewa unaojitokeza bayana kwenye tamko la Jeshi la Polisi unaosisitiza kuwa ‘sikunyweshwa sumu’ wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru, inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa tu.

Tatu ni kitendo cha Polisi kujiingiza kwenye suala ambalo kwa takriban mwaka mzima sasa, halijawahi kuwa na dhamira ya dhati ya kulielewa au kulichunguza mbali na kulifanyia mzaha kupitia magazetini.

Januari 19, mwaka huu gazeti hili pia lilifanya mahojiano maalumu na Waziri Mponda ambaye naye alisema kwa utaratibu, ripoti ya daktari ni ya mgonjwa... “Sisi hatujaandika ripoti, muulizeni DCI Manumba awape ufafanuzi.”

Alisema wanaoweza kuzungumzia maradhi ya Dk Mwakyembe ni familia yake au yeye mwenyewe kwani ndiye mwenye ripoti. Lakini wizara haiwezi kufanya hivyo.

Chanzo: Mwananchi
 
Jamani mbona sasa hizi sarakasi zinatuchanganya sisi watawaliwa? Hii ina maana gani kwa jamii ya watawaliwa?

Kwangu mimi ina maana kwamba Polisi huwa hawafanyi upelelezi na badala yake hukurupuka na kutoa taaraifa tu. Hali hii si nzuri hata kidogo yaani waziri mwenye dhamana ya Jeshi la Polisi anaikana hadharani Report ya Mpelelezi mkuu wa Serikali!! Hata sijui cha kusema ila tu bottom line ni kwamba Waziri Nahodha angeyasema hayo wakati DCI Manumba tayari akiwa anajipumzisha nyumbani kwake akiwa tayari ni DCI aliyejiuzulu; vinginevyo hii itakuwa ni sarakasi tu.
 
Hatuna serikali makini, tuna genge la wanaojiita viongozi wa serikali wasiojua uwajibikaji ni nini. Chama legelege huzaa serikali legelege.

Rais legelege huongoza serikali legelege.
Mtoto wa Mbale ulitakiwa kukamilisha kuwa Chama legelege huzaa serikali legelege, serikali legelege huzaa taifa legelege, na taifa legelege wananchi wake wote huishia kuwa legelege!.

Sisi Watanzania ni legelege, kule kwa watu wasio legelege si tumeona!, watu kama Misri, Tunisia etc sio tumewaona!. Sisi kazi yetu ni kuwaimbia tuu hawa watawala wetu nyimbo za shangwe na mapanbio tuu huku tukijidai kulalamika!.
 
Jamani mbona sasa hizi sarakasi zinatuchanganya sisi watawaliwa? Hii ina maana gani kwa jamii ya watawaliwa?

Kwangu mimi ina maana kwamba Polisi huwa hawafanyi upelelezi na badala yake hukurupuka na kutoa taaraifa tu. Hali hii si nzuri hata kidogo yaani waziri mwenye dhamana ya Jeshi la Polisi anaikana hadharani Report ya Mpelelezi mkuu wa Serikali!! Hata sijui cha kusema ila tu bottom line ni kwamba Waziri Nahodha angeyasema hayo wakati DCI Manumba tayari akiwa anajipumzisha nyumbani kwake akiwa tayari ni DCI aliyejiuzulu; vinginevyo hii itakuwa ni sarakasi tu.
Mkuu Kimbunga hii ndiyo Tanzania yetu, Waziri hajui report ya DCI wake!?. Kabla DCI hajaisoma hiyo ripoti ilitinga kwanza mezani kwa IGP na waziri anayo copy yake!. Halafu anamtuma mwandishi ndio akamuulize DCI alikoipata report!. Hiki ni kichekesho!. Kama ni uwajibikaji kesho yake tuu baada ya taarifa ile ya Manumba, angeamkia memo kali mezani kwake atoe maelezo alikoipata report ile!. Sasa unamtuma mwandishi kwa Manumba, kwani Manumba anawajibika kwa waandishi?!. Japo Nahodha ni mstaarabu wa hali ya juu, lakini na yeye ni nale nale tuu, laini laini kama maini au chapati maji!. Na kama ni mgumu kidogo basi ni mgumu kama nyanya!.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Haya DCI Manumba

huyo ni waziri wako ametoa tamko kuwa umeipata wapi hiyo ripoti yako? na ameweka wazi kwa yeye ndiye atakae zungumzia swala hilo baada ya uchunguzi kukamilika

Manumba waziri wako amekukana
 
Jambo la muhimu hapa tukumbuke ya kwamba Jeshi letu la Polisili na watu makini na wazoefu katika mambo ya uchunguzi au upelelezi, lakini ingekuwa busara zaidi kulisaidia jeshi letu lipate vitendea kazi vinavyoendana na wakati. Polisi wa Tanzania wanafanyakazi katika mazingira magumu sana, ukianzia kwa traffic, CID, FFU , watu wa IT, forensic experts wapo lakini ugumu huo wa vitendea kazi . Kweli kabisa tuahitaji kuboresha jeshi letu liwe la karne ya sasa na liwekaribu na raia wake kwa kuwalinda wao pamoja na mali zao. Police yetu mfano Patrol wa mijini, hii miji yetu midogo wako kwenye mazingira magumu sana, hakuna magari ya kutosha kufanya Patrol yao iwe ya kufurahia ingalau kiasi kidogo. Kwa DCI kutoa taarifa kama hiyo is part of Human contact intelligence,ni njia ya kutafuta ukweli kwa kuzungumza kam hivyo alivyofanya. Is part of investigation procedure ambayo ni kazi yake. Laumu kisiasa , lakini kiupelezi hasa ukilinganisha na nchi yangu yenye upungufu na uhaba wa vitendea kazi na techniciens Manumba is wright for his JOB. Leave Manumba do his JOb.
 
These guys are all clowns. Viongozi wetu wengi wamesoma lakini wanaogopana kwa sababu hawajui kuwa yupi ametumwa na nani, and that's why they all sound so idiotic. Kila mmoja anatafuta ni vipi atajaza tumbo lake leo badala ya kufikiria namna ya kupeleka maendeleo vijijini kwetu. Viongozi wetu wangekuwa wanafanya kazi kwa lengo la kuendeleza nchi, hakuna taifa Afrika nzima lingetufikia kwa sababu tuna resources na tuna wasomi wa kutosha. Muhimu ni kuwa tukumbuke haya wanayofanya hawa majuha ifikapo 2015. We need a major change.
 
Hii tamthilia itakuwa ya kichina manake mambo valu valu
 
TUFANYE KAZI SANA NA TUSALI SANA.... [TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Nahodha: Sijui DCI Manumba alikoitoa ripoti ya Mwakyembe Nahodha hajui kwa sababu yeye fan yake siyo upelelezi, Manumba ni mpelelezi and he is right kwa sababu ametumia kama mbinu za MM jeshini kupata info nyingi za tatizo hili, he is intelligent. Tanzania Jeshi la Polisi halina vitendea kazi vinavyoendana na karne hii. Kwa namna hiyo traffic, FFU, CID, wanafanya kazi katika mazingira magumu sana, traffic Dar utakuta yuko juani kuongoza magari kwa shida sana, sasa kwa suala la Manumba ametoa wapi Taarifa anjua kwa sababu kufanya hivyo ni njia moja ya kupata ukweli zaidi wa jambo. Hiyo ni human contact intelligence ambayo itamsaidia kupata info wizara ya Afya, Foreign, na kutoka kwa watu wengine wa karibu wa Mwakyembe. Tanzania ingekuwa na laboratory za uchunguzi wa kina kwa swala hilo, polisi wenyewe wangeweza kumchukua damu na kuweza kufanyia uchunguzi, wangeweza kutumia vifaa vinavyoendana na karne hii kama radiation detectors, radiowaves n.k. Haya yote Manumba anayafahamu kwa sababu ni kazi yake. Sioni sababu ya kumwandama hivi wakati yeye anakusanya data za uhakika kwa njia ambao naiona kabisa mimi ni sahihi kufuatana na hali halisi ya vitendea kazi vya polisi havikidhi kufanyia uchunguzi wa haraka na sahihi. Sielewi kwa nini waziri amesimama na kutamka hayo. Pengine hawana mawasiliano katika kutatua tatizo hili. Umakini wa kutatua au kubaini waliomdhuru(Kama kweli ni hivyo) Dr. Mwakyembe Manumba alikuwa anaenda vizuri sana. Congratulations Manumba. Inabidi ushinikize serikali wawapatie polisi vitendea kazi vinavyoendana na karne hii. Nimeandika hii siyo ninamlaaum waziri. Nawatakia kazi njema na ninaimani mtafanya kazi kwa ushirikiano mzuri kwa manufaa ya umma. God bless Tanzania, God bless Tanzania Police force and God bless Tanzanians. Thank God almighty for directing Tanzanians in the right path of development. Tuamke tusaidiane kuelimishana katika nyanja mbalimbali na siyo kutupiana maneno ya kukandamizana. Umoja ni nguvu, maneno ya kukandamizana yanaleta utengano.....Poleni Polisi kwa majukumu makubwa mliyonayo, fanyeni kazi kwa moyo mmoja mkijua mnawalinda ndugu zenu Watanzania.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
movie nzuri, atapatikana tu mchawi waacheni waruke ruke tu
 
Janga...ni dalili ya serikali ya JK kuparaganyika,kila mtu anatoa kauli ya kulinda maslahi yake.
 
Mkuu Nguruvi3, kusema ukweli hawa jamaa wanatuzeveza tuu na kujibaraguza!.

1.Nikianzia na taarifa ya DCI Manumba, japo sasa wote wanamruka, yeye alitoa taarifa ya kilichopo, " a bird in the hand worth two in the bush". Amini nawaambieni, Dr. aliporejea kutoka Apollo amekuja na complete medical report ya kilichopo!. Report hiyo iko serikalini, Dr. Mponda anajua, Nahodha anajua na JK aliisoma kwenye kikao cha Cabinet!. Hivyo DCI hakuzusha kitu and infact kazi yake ya awali alishamaliza, report yake iko kwa DPP kusubiri uamuzi zaidi.
2. Waziri wa Afya Dr. Haji Mponda ni muongo mkubwa na mnafiki kujifanya serikali haina report hiyo bali aliyenayo ni mgonjwa mwenyewe tuu!. Huu ni uongo mtakatifu unaofaa kuwadanganya watoto na humu jf tuna watoto kibao wa kifikra wakindanganywa tuu hata kwa issie ndogo, wanadanyanyika!.
3. Alichotakiwa kusema ni ukweli kuwa ripoti hiyo ipo ila ni personal report mgonjwa ndio mwenye full rights za disclosure na sio DCI Manumba!. DCI Manumba alitakiwa aseme uchunguzi wa awali wa kipolisi umebaini hakutiliwa sumu bila kui site report ile!.
4. Waziri Nahodha sasa ndio amekwenda deep, hapa sasa ndio tumepewa kitu kipya, kumbe ameagiza uchunguzi mpya wa forensic ya kubaini jinai ya sumu!. Tangu ameanza kuumwa hadi kupelekwa Apollo hakukufanyika forensic investigation yoyote sasa ndio Nahodha kaagiza ifanyike na ripoti hiyo ataitoa yeye Nahodha. This is something new and something else!. DCI Manumba alishatimiza wajibu wake na jalada liko kwa DPP, lakini kwa sababu waziri sasa ndio kaagiza uchunguzi mpya, jalada litarudi kwa DCI lipelekwa kwa watu wa forensic na hata Apollo sasa ndio wataarifiwa kuwa uchunguzi kwa mgonjwa huyo sio just the ordinary medical report bali ni forensic investigation ambayo ni kazi ya kipolisi na sio ya kidakitari, hata hao Apollo hivyo vipimo sasa watavipeleka kwa watu wao wa forensic for certification just in case kesi itatinga mahakamani!.
5. Kunapotokea ubishani kama huu unaohusisha hard facts, kama unaamini kwenye ukweli, unasimama na ukweli huo unaouamini hata kama utabaki peke yako kwenye ukweli huo kama Yesu alivyosulubiwa kwa kusimama kwenye kweli. DCI Manumba pia ataishia kusulubiwa ili serikali ijikoshe kuwa atleast sasa it is doing something kwenye tuhuma za Mwakyembe ambaye alizifikisha kwa IGP Mwema na wakuu wote wakiwemo Tiss, Waziri hadi Ikulu na alipeleka copy kwa baadhi ya wanabalozi just incase something inge imtokea kabla uchunguzi haujafanyika!. Tiss walimpuuza, IGP alimpuuza na kila mhusika walimpuuza only wanabalozi walikuwa concerned ila hawakuweza kuingilia kati kwa sababu haya ni mambo ya ndani!.Wajameni Mnyonge tumnyongeni ila haki yake, mpeni!.Pasco.
Mkuu Pasco, nikuhakikishie serikali imelikwepa hili suala si kwasababu ya uchunguzi, ni kwa unyeti wake na jinsi linavyogusa watu wasiogusika.

Waziri mkuu alikwepa, nahodha akakwepa, haji Mponda akaijitoa. Manumba amekubali kubeba mzigo asioujua au anaoujua ndani kuna nini. Leo likitokea lisilotarajiwa na mwenyezi aepushe, Manumba si mhusika tu ni mshiriki mkubwa. Hilo lipo katika kumbu kumbu za wanadamu na ataishi nalo.

Kama taarifa zilikuwa katika Cabinet, ni wazi yeye anajua hilo akiwa DCI. Kwa mtu mwenye akili asingekubali kutupiwa kamba na kuidaka. Ni wazi nahodha sasa anajua na amesoma watu wanasema nini naye anajivua mzigo wa misumari aliojitwika Manumba.

Kama Manumba angetumia fikra kidogo, angewauliza viongozi wenzake juu ya kushindwa kujibu tuhuma au kuzifanyia uchunguzi tuhuma za tishio la mauaji ya Dr Mwakyembe ambayo amekalia ofisini mwake miaka nenda rudi.

Baada ya viongozi wenzake kumkana iwe kwa ukweli uliopo au uongo, Manumba angejiuzulu mara moja. Sasa hivi heshima yake ndani ya vyombo vya dola imekwisha na amebaki kuogopwa tu kama tunavyomuogopa kiumbe yoyote anayeweza kutudhuru.

Pasco, fuatilia upandaji ngazi wa Manumba, angalia alifanya kazi na nani hutakawia kujua kuwa Manumba yupo njia panda akitafakari amtumikie nani kati ya 'mabwana wawili'. Serikali au waliomtuma awasafishe.
Unakumbuka msemo maarufu JF wa mapacha watatu?

Leo mkuu Pasco umegeuka serikali ile ile uliyosema uwezo wake wa uchunguzi umefika mwisho, na taarifa yake ni ya mwisho! Ukasema Sitta ashtakiwe kwa uzushi. Sisi tulijua wanatuchezea akili hawa akina serikali mapema kabisa.
Kwa jinsi wanavyojikanyaga na kujichanganya ndivyo shaka yetu inavyozidi.

Mshauri Manumba, kama anaona anaonewa ajiuzulu. Akiendelea kuwepo tutamuuliza kuhusu majaribio ya mauaji aliyoyaminya ofisini kwake na sasa anakurupuka na hili asilojua au analolijua Kwa kutoa taarifa za kiwango cha darasa la VI B.

Msimamo wa hoja zangu upo pale pale, tunataka ukweli na wala ukweli usifichwe kwa mwamvuli wowote.
Kama ni uharamia, maharamia watajwe na kama ni uzushi, basi wazushi watajwe.
 
huyu Nahodha kidogo ana make sense kulingana na maelezo yake..

Mkuu Ngumijiwe unajua hawa watu wamepima upepo na wameona sio kama walivyotarajia,kama unakumbuka awali kulikua kuna majibizano kati ya Sitta na Naodha juu ya ilo,inawezekana hata Manumba kuja na kauli ile alikuja nayo toka kwa ma boss wake,lakini baada ya kuona hali si kama walivyotarajia wote wanamruka DCI,unajua ili jambo la Mwakyembe liko tense sana,limebeba hatari/bomu kubwa kuliko watu wanavyofikiria kua ni rahisi,ndio maana hata Naodha mwenyewe ameamua kukiri kua ili jambo limebeba hatari kubwa,nafikiri wamepata taarifa za "kiintelejensia" na Mwakyembe nae kua kimya si kua ni mpuuzi,anaelewa nini cha kufanya,unajua always msomi aliyeiva kisomi uwa hakurupuki,ila hii yote inaonyesha jinsi serikali yetu isivyo organised,kila kiongozi anakuja na kauli yake
 
Tatizo ni vitendea kazi vinavyoendana na karne hii polisi hainavyo. Techniens hakuna hata hiyo ripoti ya doctor Mhindi akiwa nayo yeyote yule tukifuata utaratibu wa serikali kutoa proof ya kina kwa ripoti hiyo bila na kuwa na maabara ya uchunguzi ya polisi kutokuwepo ni ngumu sana. Ni vizuri polisi wawe na hospitali yao na doctors wao, maabara yao na techniciens wao, wapewe training kulingana na wakati unavyokwenda(karne hii ya leo).
 
Nangoja kauli ya mwisho ya mh rice, yeye atahutubia na kutuambia..."Hata mimi nawashangaa wote waliotangulia ktk hili suala!"
 
Hiki ni kipindi kigumu cha uongozi kutokea hapa nchini. Siamini kama itawahi kutokea tena. Sioni kiongozi hata mmoja. yaani ni ghalasa limeteua maghalasa kuongoza nchi. Mungu atusaidie.
 
Back
Top Bottom