Nahitaji ushauri: Nimechoka kukaa ukweni

Nahitaji ushauri: Nimechoka kukaa ukweni

Aisee sasa unalia lia nini?? Hizi posti nyingine unaweza kudhani ni maigizo fulani hivi.
 
Umeshaondoka?

Kama bado nini kinakuzuia si umesema una nyumba yako au haijaisha?
 
Mkuu mambo haya yapo nayanatoke kila siku kwenye jamii zetu.
Sasa si usepe???!!! Umefungwa miguu huko ukweni??? Inawezekana haya mambo yanatokea lakini nashindwa kuona mantiki ya wewe kulia lia hapa wakati umeshasema una nyumba yako mwenyewe. Mimi kwa uzoefu wangu, wanaume wengi wanaokaa ukweni huwa wako katika hali ngumu kiuchumi, sio eti mtu ana nyumba yake kaoa halafu anaishi ukweni. Ndio maana watu wanakushangaa hapa.
 
Ili uitwe mwanaume ni lazima uwe na uwezo wa kutoa maamuzi magumu la sivyo hata huyo mtoto wako atakudharau. chapa mwendo kaka.
 
Kitouti Una lako jambo. Hapo kwa baba mkwe mambo ya msosi ni shwari. Mtu mwenye nyumba yake hawezi kukubali upuuzi huo! hiyo naona iko kwako tu mkuu! Baba mkwe anawapenda sana wakwe zake huyo ni nomaaaaaaa.
 
Mkuu unalalama nini, hii sio kitu ya kuleta jamvini. Hivi utaishije ukweni kisa nini? Mke!!!!! Mwambie mke aamue moja wakati huo haupo hapo! Yaani hata huyo mtoto wako anakuona kama ka house boy fulani
 
Kuishi au kujenga ukweni ni sawa na kujenga nyumba katikati ya barabara huku waziri wa miundombinu akiwa J. POMBE Magufuli.
 
Mkuu unalalama nini, hii sio kitu ya kuleta jamvini. Hivi utaishije ukweni kisa nini? Mke!!!!! Mwambie mke aamue moja wakati huo haupo hapo! Yaani hata huyo mtoto wako anakuona kama ka house boy fulani
Mkuu, mficha maradhi mauti humumbua. Nimeileta jamvini ili nipate maoni ya wanajamii kuhusiana na swala hili, wenda ikawa sipo pekeyangu.
 
Ondoka mwambie mkeo unaondoka siku ya pili akufuate na mtoto usibebe kitu mbali ya nguo chache. Ni aibu kukaa ukweni hata kama kitanda huna kalali kwenye godoro.
 
uzuri ni kwamba walikuambia toka mwanzo masharti na ukakubaliana nao but najiuliza hukujua au hukuomba ushauri kabla ya kukubali madhara ya kukaa ukweni. Mimi mwanamke mwanaume atake kunioa halafu anipeleke nikaishi na kwao ukweni sikubali najua sitakuwa na uhuru kila nitakachokuwa nafanya nitakuwa najistukia sasa kwa wewe mwanaume I can imagine how desperate you are.
 
Moja ya mitihani ninayo kumbana nayo kwenye ndoa yangu ni mazingira ninayo ishi.

Nimevumilia sana lakini sinabudi kusema basi, liwalo naliwe lakini siwezi kukubali kuendelea kuishi ktk nyumba ambayo ni mali ya familia ya mke wangu (Ukweni).

Siokwamba nyumba ni mbovu au maeneo ni yakishamba hapana, tatizo nashindwa kujitawala ndani ya ndoa yangu.

Nashindwa kufanya maamuzi ya kiume ndani ya ndoa yangu sina kauli kabisa kisa naishi kwenye nyumba yao, nyumba ambayo imejazana kaka na dada wa mke wangu.

Siwezi hata kumkata makofi mke wangu pindi aniudhipo kiufupi nipo ndani ya ndoa isiyo na furaha kwa upande wangu . Hiiyote ilitokana na mimi kukubali kumuoa binti yao.

Hii familia ni ya kibabe sana Huwezi amini.

Nilipo jitokeza na kutangaza nia yangu ya kumposa binti yao sharti kubwa nililopewa nikua binti yao hawezi kwenda kuishi mbali nao Kwa hoja bado ni mdogo kiumri hivyo anaitaji uangalizi kutoka kwao.

Hivyo ikaamuliwa kama nahitaji kumuoa binti yao basi nikubari tuishi wote hapo kwao hivyo nikakabidhiwa chumba ambacho naona kama ndio kinacho nitesa kwasasa.

Nimevumilia dharau kutoka kwa kaka na dada zake kwa muda wa miaka minne sasa ila imefikia hatua nasema nimechoka bora kama mke nikose kuliko kuendelea kuonekana ----.

Kama kuzaa tumesha zaa na tayari mtoto keshakua. Kama nyumba ninayo tena siyo ya urithi kama mtoto wao walisema bado hajakua sasa tayari ameshakua ushahidi ni huyu mtoto tulie nae.

Hapana bora nikose mke kuliko kuendelea kuonekana ----. Inafikia hatua mpaka mke wangu ambaye ndiye mtoto wao ananionea huruma jinsi ninavyo buruzwa na familia yake?

Hapa bora niende zangu nyumbani wazazi wangu wanashindwa kujitawala pindi wakija kunitembelea wanakosa uhuru Kabisa wa kupanga mambo mbalimbali na mimi mtoto wao kisa niko ukweni?

Uko wapi utamu wa ndoa ikiwa kila kitu anapanga baba mkwe? Chakula anunue mpaka nguo za mke wangu pia?
Kwa kifupi umeolewa.
 
makubwa yaani unapewa chumba ukweni unakubali? mi nilidhani ulipewa bonge la mjumba ...sasa unagegeda vipi? gemu naona mnalipiga kwenye silent mode tena usiku mzitooo...yaani sikupatii picha. ila una moyo aisee...
umejidhalilisha sana ujue..na hao wazazi wako wanaokuja hapo kukutembelea eti hawapo free nawashangaa sana mimi wala nisingerusha mguu hapo kamwe.
nenda kwenu haraka sana
Hahahaaaa game inapigwa kwenye silent mode... Miguno yote inamezewa... Jamaa ana uthubutu, kuishi ukweni kabisaaa!!! Afadhali hata ingekuwa mnaishi kwenu si kwa mwanamke, mkuu Kitoabu hebu amka acha izo mambo zako bhana.
 
Siafadhali angekua anamnunulia mwanae tu! Kunasiku alininunulia suti, mpaka leo ipo tu ndani sajawahi kuivaa.
Hahahaaaa, noma sanaa, wewe umuwezeshe yeye ndio anakuwezesha? Umeianzisha vema weekend yangu mkuu, huu ni Mzaha nini? Mnavishwa na kulishwa? Plus free acomodation. Si ajabu kama amewapa shamba ni yeye ndiye anaweka vibarua lol, waume wenzio w ameridhika tuu ehhh? Umemgeuzageuza na kumpindua pindua mtoto wa watu usiku alafu asubuhi mnakaa sitting room na wakwe zako na mashemeji mnakunywa chai, aisee hataareeee
 
Back
Top Bottom