Nahitaji ushauri, mke wangu hana uzazi

Nahitaji ushauri, mke wangu hana uzazi

Habari zenu watu wa Mungu,
Mimi ni kijana nina umri wa miaka 30, naishi mkoa wa arusha wilaya (mabano). Ni mwalimu wa sekondary, nilioa miaka kadhaa iliyopita na bahati mbaya mpaka sasa mke wangu hajafanikiwa kupata mtoto. Nimetafuta namna nyingi za matibabu sijafanikiwa. Mbaya zaidi mke wangu nionavyo mimi kuna kitu anakijua ndani ya hili tatizo. Kuna watu walishawahi kuniambia kabla kuwa hana uzazi na haitatokea azae, ila niliona ni wivu tu. Pia waliniambia kuwa amenidanganya vitu vingi ambavyo siwezi kuweka wazi. Kutokana na hali hii saivi mke wangu hana amani na hata sura yake imeanza kuchoka. Ninachojiuliza kwa nini nilime na nisipate mazao miaka mingi? Nahisi kukata tamaa, na huyu mwanamke anajulikana kama nini kijijini kwetu. Amenifanya nisipate mwanamke mwingine, kila nikijaribu nahisi atajua.
Naombeni ushauri, mimi mkristo mshika maadili na naheshimika kanisani. Huyu mwanamke ameanza kunizeekea na saivi sina hata mtoto wa kusingiziwa kutokana na uaminifu wangu. Naona wenzangu waliooa juzi tu wanapata watoto, mimi naumia tu. Nifanyeje nipate watoto na heshima yangu iendelee kuwepo?
Poleni sana...take it as a couple problem... Usilifanye tatizo liwe lake pekee yake.
Ni kweli, kuna furaha kubwa sana kuwa na watoto,lakini ndoa ni zaidi ya watoto.
Watoto ni zawadi ambayo ni matokeo ya baadae.Mungu amependa muwe hivyo; ridhika na hiyo hali.

The Great Gatsby
 
mkuu kuwa serious kufuatilia issue ya mkeo na acha kusikiliza watu ... nenda hospitali uambiwe tatizo lipon wapi? labda kama alitoa mimba kizazi kikazengua kikatolewa hiyo ni issue nyingine
 
Yes...uje na maelezo ya pande zote mbili ili tushauriane vema.
Mheshimu mkeo; tunzianeni siri zenu.

The Great Gatsby
 
Lisemwalo lipo ndugu,sio wote wanaokuonya wanakuonea wivu,pengine watu walijua historia ya mkeo kabla ya kukutana na ww,walizijua njia zake ndo maana walikuonya.
Hukuwasikiliza,siku zote watu wasemapo mambo yahusuyo maisha yako au watu wa karibu na ww usiwapuuze moja kwa moja fanya uchunguzi kidg ujiridhishe.
Any way mshirikishe mkeo mawazo yako,atakuelewa pengine atakuruhusu upate mtoto kwa mwanamke mwingine,japo usimdharau mkeo bro.

Philips X2560
 
mkuu kuwa serious kufuatilia issue ya mkeo na acha kusikiliza watu ... nenda hospitali uambiwe tatizo lipon wapi? labda kama alitoa mimba kizazi kikazengua kikatolewa hiyo ni issue nyingine
hilo ndo niloambiwa kabla sijamwoa
 
Mpe redcard oa mwingine upate mtoto maana kuvunja amri ya 6 ni dhambi kisha utakwenda kumrudia tena. Utakosa mtu wa kurithi mali zako ndugu yangu Fanya hima umri unakuacha hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya mambo yahitaji akili ya ziada wala si ushauri,
Tafuta mwanamke pembeni azisha mausiano kama mchepuko wako na atakuzalia tu tena arusha mbona wapo wengi sana!
Ila angalizo mschana yoyote utakayekuwa naye nje ya mkeo usimweleze chochote kuhusu mambo yanayohusu ndoa yako wala akishika mimba yako muone kawaida wewe mpe matunzo ya kutosha.
Mkuu akienda uko nje akakosa au akawa yeye ndo ana tatzo?
Azungumze na mkewe vzur anaweza pata kamchepuko kumbe na kenyewe kana chepuka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu watu wa Mungu,
Mimi ni kijana nina umri wa miaka 30, naishi mkoa wa arusha wilaya (mabano). Ni mwalimu wa sekondary, nilioa miaka kadhaa iliyopita na bahati mbaya mpaka sasa mke wangu hajafanikiwa kupata mtoto. Nimetafuta namna nyingi za matibabu sijafanikiwa. Mbaya zaidi mke wangu nionavyo mimi kuna kitu anakijua ndani ya hili tatizo. Kuna watu walishawahi kuniambia kabla kuwa hana uzazi na haitatokea azae, ila niliona ni wivu tu. Pia waliniambia kuwa amenidanganya vitu vingi ambavyo siwezi kuweka wazi. Kutokana na hali hii saivi mke wangu hana amani na hata sura yake imeanza kuchoka. Ninachojiuliza kwa nini nilime na nisipate mazao miaka mingi? Nahisi kukata tamaa, na huyu mwanamke anajulikana kama nini kijijini kwetu. Amenifanya nisipate mwanamke mwingine, kila nikijaribu nahisi atajua.
Naombeni ushauri, mimi mkristo mshika maadili na naheshimika kanisani. Huyu mwanamke ameanza kunizeekea na saivi sina hata mtoto wa kusingiziwa kutokana na uaminifu wangu. Naona wenzangu waliooa juzi tu wanapata watoto, mimi naumia tu. Nifanyeje nipate watoto na heshima yangu iendelee kuwepo?
nenda kwa tb joshua
 
hilo ndo niloambiwa kabla sijamwoa
duh kaa na mkeo sasa mwambie akuambie ukweli kilichotokea halafu mfanye maamuzi pamoja kama uzae nje uchukue mtoto mleee au iweje? hata me mkinipa milioni kumi nawafanyia favor nakubebea damu yako nakupa mtoto wenu me naendelea na maisha yangu ..... ila kwa sharti la nikisikia mnamnyanyasa i will come back sababu kukupa kiumbe kwa milioni kumi ni ndogo sana hiyo ni matunzo mkuu na wala sijakuuzia
 
Lisemwalo lipo ndugu,sio wote wanaokuonya wanakuonea wivu,pengine watu walijua historia ya mkeo kabla ya kukutana na ww,walizijua njia zake ndo maana walikuonya.
Hukuwasikiliza,siku zote watu wasemapo mambo yahusuyo maisha yako au watu wa karibu na ww usiwapuuze moja kwa moja fanya uchunguzi kidg ujiridhishe.
Any way mshirikishe mkeo mawazo yako,atakuelewa pengine atakuruhusu upate mtoto kwa mwanamke mwingine,japo usimdharau mkeo bro.

Philips X2560
mwanzoni tulikuwa tunashirikishana sana, sasa kipindi hiki sina hamu ya kuongelea mambo hayo. Isitoshe nimeajiriwa kijijini, yeye ni mzawa wa huku. Kilichonifanya nifikirie ni wivu ni kwamba wakati wa kuanza mahusiano nilipata wapinzani wengi mkuu
 
yaan azae na beki 3!umenikwaza! we kama huna ushauri kaa kimya! utajskiaje ww huna uzaz mkeo akazaa na houseboy wako!....yap yap fisi mwekundu
Jamani....sasa azae na nani Binti?anyway nisamehe buuuure!?
Well...jee wewe Una kizazi?samahani lakini.
 
duh kaa na mkeo sasa mwambie akuambie ukweli kilichotokea halafu mfanye maamuzi pamoja kama uzae nje uchukue mtoto mleee au iweje? hata me mkinipa milioni kumi nawafanyia favor nakubebea damu yako nakupa mtoto wenu me naendelea na maisha yangu ..... ila kwa sharti la nikisikia mnamnyanyasa i will come back sababu kukupa kiumbe kwa milioni kumi ni ndogo sana hiyo ni matunzo mkuu na wala sijakuuzia
hahahaaa, sidhani kama kuzaa mtoto na kulelewa na mama tofauti ni sahihi. ambao tutakuwa na uchungu na huyu mtoto ni mimi na wewe, yeye atalazimisha tu kwa sababu ya tatizo lake. Nawaza kwa herufi kubwa NIZAE TU NA MKE MWINGINE NAYE AWE MAMA WATOTO WANGU.
 
Back
Top Bottom