Nahitaji supplier wa vifaa vya Ujenzi na Hardware

Nahitaji supplier wa vifaa vya Ujenzi na Hardware

Godwin Arnold

Member
Joined
Feb 22, 2018
Posts
20
Reaction score
13
Habari wadau wa jukwaa hili.
Mimi ni kijana na mfanyabiashara wa vifaa vya ujenzi niko Dar wilaya ya Kigamboni.

Biashara hii nimeianza miezi miwili iliyopita, changamoto niliyonayo ni mtaji mdogo (nimeweka Tsh 9mil ukiachana na gharama za kodi, shelves na matengenezo mengine madogo madogo)

Nahitaji kupata supplier ambae atanipa mzigo kwa mali kauli nikiuza nampa pesa yake.
Mwenye connection anisaidie

Nina documents zote za biashara, kutoka BRELA, TRA na Halmashauri.
 
Sema upewe vifaa kwa mkopo, sio mali kauli.
 
Kwanza Jenga uteja na uaminifu uliotukuka Apo Apo ulikonunua huo mzgo wako WA mil 9 Kwa cash

Kisha Supplier wako akikuamini ataanza kukupa mzgo Kidogo kidogo.

Mfano:
Yaani kanunue mzgo kwake WA mil 5 afu mkope mzigo WA laki 5, na urejeshe pesa yake Kwa MDA mfupi.

Next time utapanda kdg kdg Kwa hatua Hadi kufikia kukopa mzgo WA milion Hadi billion kadhaa
 
Kwa mfanyabiashara mpya WA hardware,

sikushaur kabisa biashara yako changa ukaanza kuiingizia mizigo ya kuuza inayotokana na Mali kauli.

Wanaoendesha biashara zao Kwa mizigo ya Mali kauli, uwa ni ngumu Sana kutoboa.

Bidhaa Bei ya jumla inayouzwa elfu 15
Ili ukauze kwa elfu 20 rejareja,

Wewe unaechukua kwa Mali kauli utapewa Kwa elfu 18 ili ukaambulie elfu mbili.

Sasa Kama mzgukuko wako Bado mchanga, au kijana wako adokoe, au dharula yoyote itokee.

Aisee kurudisha pesa za watu itakuwia ngumu Sana.

Na hapo kufilisika ni CHAP KWA SANA
 
namimi nimetoka na kitu apa, asante mkuu DeepPond
 
Huyo ni beginner mkuu, anaweza pata japo sio rahisi kihivyo,,,, ! Umemjibu dry sana, mtie moyo
Kumtia Moyo ni kumlaghai na kumdumaza kiakili.

Cha muhimu Kama wateja anao,

Abane matumizi yake na afanye Mzunguko mkali Sana, Kila baada ya siku mbili ahakikishe anapakia mzgo.

Yaani account yake iwe njia ya kupitishia TU pesa, Kama ana assets au Liability kadhaa, aziuze zote TU aingize pesa dukani ili afanye mzunguko.

Baada ya MDA mfupi atajikuta amekua haraka sana na atajikuta hatohitaji hizo bidhaa za Mali kauli
 
Kuuza assets kwa ajili ya kukuza biashara kwangu ni big No, labda kuchukulia mkopo bank ! Biashara ni gambling mkuu ! Ukingatia anadai ni biashara mpya, mzunguko wake sijajua,,,, ndo anaanza kutengeneza wateja n.k ! Bado wampige/wamkope n.k !
 
Kwa kawaida,
Bidhaa nyingi za hardware zinazotoka sana individually zina faida ndogo sana.

Pesa ya faida kwenye hardware utaipata Kwa kua na mauzo makubwa.

Bidhaa Kama cement, Nondo,tiles, BATI na rangi ukizichukua kwa Mali kauli unajitengenezea mazingira ya kufilisika chap kwa haraka Sana.

Maana
1. Zina risk Sana,
Mfano,
- mfuko wa Cement unakuta faida yake ni buku, apo UJAWEKA zitakazoganda au kuchanika zikiwa stoo.

-box la Tiles unakuta faida yake ni buku 2, UJAWEKA zitakazovunjika ukisafirisha, na mteja akija kununua kwako anachambua na zilizovunjika hazitaki.

-ndoo za rangi faida unakuta ni buku 2 Hadi 3, apo Kuna ndoo kupasuka zikiwa stoo, rangi kuexpai kabla hazinunuliwa n.k

-kwenye bati ndo pasua kichwa kabisa

2. Unaweka mtaji mkubwa afu Zina faida kiduchu sn, unapaswa kubargain sana unaponunua ili zikulipe. Unapozichukua Kwa Mali kauli, Huna fursa ya kubargain sana.

3. Zina gharama kubwa sn za uendeshaji, YAANI gharama za usafirishaji , gharama za ushushaji, gharama za upakiaji, gharama za utunzaji. (Utapaswa kua na stoo za kutosha). Hivi vyote vinataka pesa.

4. Wateja wanapenda kuzikopa kopa Sana, na hardware ya rejareja bila kukopesha utapoteza sana wateja. Na kikawaida wateja wengi WA rejareja hawalipi Kwa wakati. MDA huo boss Aliekupa mzgo WAke kwa malikauli anaitaka pesa yake Kwa wakati.

4. Zinashawishi Sana vijana kuzidokoa, maana zinauzika mtaani chap kwa Sana. Na biashara ya hardware huwezi kuuza peke Yako,lazima uwe na vijana.
 
Kuuza assets kwa ajili ya kukuza biashara kwangu ni big No, labda kuchukulia mkopo bank ! Biashara ni gambling mkuu ! Ukingatia anadai ni biashara mpya, mzunguko wake sijajua,,,, ndo anaanza kutengeneza wateja n.k ! Bado wampige/wamkope n.k !
Sasa mkuu,
biashara mpya mzunguko wake ujaujua bado, ndo unataka ujilipue ukazamishe bidhaa za watu Kwa mgongo WA mali kauli?

Yaani mtu ukafanye gambling Kwa pesa za watu, huoni unajitaFtia stress za mapema Sana na kujichafulia cv ya kutokopesheka mapema sana?
 
Sishauri sana biashara ndogo ,,kuwa na Mali kauli , mara nyingi unapo omba Mali kauli una mpa nafasi pia mwenye Mali kukushindilia vitu vilivyomshikilia na yeye pia ,,

Mfano ukiwa unaomba mali kauli za tv ,mara nyingi boss anataka akupe na mshine za kufulia nguo ,Sasa hizi Huwa hazina mzunguko ,,mashine za kufulia viatu ,, vifriji vidogo vya chumbani Huwa haviuziki ,,ila ukiomba Mali kauli boss atakuambia chukua na hivi na unakuwa huna ujanja wa kuvikata kwasababu huna cash mkononi.. namwishowe anataka pesa yake ,, utauza vitu vyako vyenye mzunguko kulipa deni.
 
Back
Top Bottom