Nahitaji mwanaume alietaliki au kufiwa na mkewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nahitaji mwanaume alietaliki au kufiwa na mkewe

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Maty, Aug 25, 2010.

 1. Maty

  Maty JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 2,170
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Wadau mimi sijui nijiite mdada au mmama, nina miaka 30 na nina mtoto mmoja ana miaka tisa. Nina kazi yangu nzuri kiasi inakidhi my basic needs including food, clothes and shelter.
  Nimekaa najisikia mpweke nahitaji mwanaume ambaye ameshataliki au mkewe bahati mbaya amefariki lakini sio na ukimwi na ikiwezekana awe na mtoto mmoja tuishi pamoja na kulea watoto wetu kwa upendo na amani tele. Kama uko interested na uko serious kwani sihitaji uhusiano wa kupita nahitaji strong relationship nimezunguka zunguka sasa nahitaji kutulia. waweza wasiliana na mimi kwa kupitia matyshirima@gmali.com
   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Bi Maty mbona hajaeleza Baba wa huyo mtoto anafanyanini,kwanini hutaki kukaa nae mlee mtoto wenu na ikiwezekana muongeze mtoto mwingine ?
   
 3. g

  gnasha Member

  #3
  Aug 25, 2010
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na je unatafuta mwanaume umri gani? dini gani?
   
 4. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,455
  Likes Received: 2,040
  Trophy Points: 280
  ningekuwa sijaoa ningetupa karata lakini mbona umri wako sio mkubwa kwa nn hutaki ambaye hajaoa kabisa maana mtoto mmoja wala si kikwazo cha kutafuta waliotaliki au waliofiwa
   
 5. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  okay,vizuri kama umeamua kutulia baada ya kuzunguka zunguka kidogo,najitolea kukuombea ufanikiwe kwani nia yako ni nzuri.
  haya mabinamu mnafit hapo?
   
 6. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #6
  Aug 25, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Naomba niulize ifuatavyo;

  1. Baba wa huyo mtoto mmoja yuko wapi na anajishughulika na nini? Kama amefariki, lini na kwa nini?
  2. Iwapo sina sifa ulizotaja; yaani sijataliki wala sijafiwa na mke, na nipo interested, itakuwaje?
  3. Unadai umezungukazunguka na sasa unataka kutulia...! Umezunguka hadi wapi? Umekutana na wangapi? Na je, unamaanisha bado hujatulia, lakini sasa unataka kutulia?
  4. Kazi unayofanya ni ipi? Bar maid, clerk, biashara ya ...., ufundi wa ...., n.k
  5. Kwa sasa unaishi wapi? Dar, Arusha, Mombasa .....
  6. What is your current health status?
   
 7. faithful

  faithful JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2010
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Maty hongera kwa kuvunja ukimya!wengi wana tatizo kama lako wanaona aibu kujitokeza hadharani....

  wewe konakali kama una interest m PM au kama vipi omba e mail au phone number atakujibu maswali yako...asimwage mchele kwenye kuku wengi.....
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Aug 25, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ngoja na mimi nizungukezunguke kwanza halaf n'tafikiria..
   
 9. Maty

  Maty JF-Expert Member

  #9
  Aug 25, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 2,170
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Baba wa mtoto yupo ana kazi nzuri tu na mtoto anamhudumia kama kawaida mtoto wetu anasoma boarding na yeye ndio analipa ada na mahitaji mengine muhimu ya mtoto ila sometimes akikwama huwa na mimi inabidi nimsaidie. Na kwa alieniuliza kwa nini baba wa mtoto hatukai nae ni kwa sababu ilitoke bahati mbaya katika ugirlfriend na uboyfriend miaka ile ndio ujauzito ukatokea na mtoto kuzaliwa hatukuwa tumepanga ilitokea tu accidentaly i think we were not ment to be together hakuwa ubavu wangu ila mtoto wetu kama nilivyosema 2namtunza wote vizuri tu na yeye alishaoa mke mwingine na anamaisha yake.

  Nimezunguka kidogo kwani mi ni bidamu nisingeweza kukaa hivi hivi ila na wangapi siwezi kukutaji my dia kwani hata wewe ningekuuliza umetoka na wangapi usingeniambia au ungenidanganya.

  Kuhusu kazi mimi ni administrative asistant kwenye international organisation moja mkoa sitotaja kwa sasa nitazungumza baadae.

  Nilihitaji ambaye ameshaoa au amefiwa na mke kwani hao wana experience ya kuishi katika maisha ya ndoa na kingine naona kama kaumri kameenda kidogo na sina uhakika kama naweza kupata bacherlor mwenye miaka 30 na kuendelea wengi wao wameshaoa. Ila kama uko interested inabidi uwe above 30 chini ya hapo haiwezekani na usiwe mwanaume suruali kama nilivyosema awali.


  Kuhusu afya niko kupima magonjwa yote yanayoogopesha mbele ya mtarajiwa akipatikana.
   
 10. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #10
  Aug 25, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145

  Binti si wazo baya pia kujihusisha na vyama mbalimbali vya Kitaaluma hasa katika Networking Events na Seminars. Utawakuta akina kaka singles wengi na wa kila namna wenye shida ya kupata mke pia. Nawafahamu several lakini hapa si mahali pake na wala mimi si msemaji wao.

  Otherwise Goodluck!
   
 11. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #11
  Aug 25, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  hapo kwenye blue bora second option.
  kwenye red, mhh mama uwe na majibu, hiyo baadaye inaweza kuwa fimbo ya kukuchapia.
   
 12. Beauty

  Beauty JF-Expert Member

  #12
  Aug 25, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 540
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Duh una hatari, ukimaliza kuzunguka, Maty kashajipatia wake wa maisha.
  Gud lucky Maty
   
 13. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #13
  Aug 25, 2010
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hamwagi mchele anataka kujibiwa hayo madukuduku yake,kwa vile nae kajieleza humu ili asaidiwe,akijiridhisha basi mambo yaanze maana kutakuwepo competition kali tu.
   
 14. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #14
  Aug 25, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  All the BEST Maty! Utampata unaefanana nae! Piga GOTI!
   
 15. D

  Dick JF-Expert Member

  #15
  Aug 25, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hongera Maty kwa ujasiri wa kusema. Usisahau kumuomba Mungu pamoja na mizunguko yako!
   
 16. Maty

  Maty JF-Expert Member

  #16
  Aug 25, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 2,170
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Kuzunguka nimeshastop siku nyingi sasa hivi niko alone tu mpaka nitakapopata wa uhakika. Na sina sababu ya kuzunguka kwani nina uwezo wa kujitimizia mahitaji yangu muhimu mana wengine wanazunguka kwa wana matatizo. Na sijazunguka sana kihivyo nilikuwa natafuta exposure tu lakini sijaona jipya
   
 17. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #17
  Aug 25, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Dada,
  Hongera kwa kuwa muwazi n amkweli.Katika vigezo, umezungumzia kutaka mwanaume mwenye uzoefu wa maisha ya ndoa post ya 9 hapo juu
  ( nadhani wewe huna uzoefu huu kwani hukuwahi kuolewa kufuatana na maelezo yako ).

  Mpendwa, unaelewa madhara ya kumpata mwenye uzoefu ukiacha faida zake ambazo bila shaka zipo.
  KIDOKEZO: Mwenye uzoefu ujue ana kigezo tayari cha kukupima na kukulinganisha. Utaweza kusikia ukiambiwa " mke wangu alikuwa ananipikia hivi, alikuwa hodari kwenye lile, hakuwahi kunifanyia hivi au vile" Uko tayari kuwa na mshindani asiyeonekana?

  Ni angalizo tu inaweza isitokee pia.

  Good luck!!
   
 18. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #18
  Aug 25, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nadhani hii email account
  PHP:
  matyshirima@gmali.com
  imeisha kuwa overloaded, Kila nikijaribu kutuma maombi kwa niaba ya rafiki yangu Fidel naona zanirudia.
   
 19. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #19
  Aug 25, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nakupongeza kwa uamuzi wako wa pekee wa kuamua kutulia.
  Je afya yako kwa sasa ikoje? Umesha check na kujiridhisha?
   
 20. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #20
  Aug 25, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hahahaha mpwa bana ngoja nijaribu na mm kuMP asije Nyani Ngabu akaniwahi bure.
   
Loading...