Pole sana, unaweza kuwa unamuongoza ama kusema wote sala hii fupi nina imani atapona tu mkimtumainia yeye aliye juu, pamoja na kumpeleka kuombewa pia jitihada zenu ni muhimu:
Moto wa Roho Mtakatifu x7
Damu ya Yesu x7
Katika jina la Yesu x3
Baba wa Mbinguni ninakushukuru kwa kuwa ulisema katika Zaburi 50:15 kuwa nikikuita siku ya mateso utaniokoa na wewe utanitukuza.
Baba, ninakuita leo uje unikomboe nisiwaone watu hawa wageni tena, katika jina la Yesu.
Kila pepo lililojivisha sura ya ndugu aliyekufa, rafiki, dada au mke/mme (taja kile kinachohusika), ninakifunga na kutupa mbali na upeo wa macho yangu, katika jina la Yesu x3
Haijalishi ni jina gani unajiita, ninakukataa katika jina la Yesu.
NInakufunga ewe pepo ambaye hunijia mchana na usiku, ninakukataa na kukutupilia mbali na upeo wa macho yangu, katika jina la Yesu x3
Asanye Yesu kwa kunikomboa, katika jina la Yesu.
Amina