Nahitaji msaada wa maombi yenu.

Miwatamu

JF-Expert Member
Oct 2, 2012
1,450
487
Siku zote imekuwa ni kawaida yetu sisi wana jamvi kupeana ushauri na kutiana moyo katika mambo mbalimbali yanajitokeza katika maisha yetu ya kila siku. Nafahamu kuwa humu tupo watu wenye itikadi na imani tofauti, ila wote tunamtegemea mola pekee, kwa imani hiyo naomba wana jamvi mnisaidie kumuombea mke wangu ambaye kwa muda wa miezi kadhaa sasa anasumbuliwa na mapepo wachafu (Majini) kiasi kwamba hata kazini ameshindwa kuhudhuria vile ipasavyo. Hivyo kupitia uzi huu na imani zetu naomba tumuombee kwa dhati.
Natanguliza shukrani.
Amen.
 
CIELLO, daima huwa napenda sana mawazo yako na hicho ndicho kinachofanyika hadi sasa na kwa %kubwa mungu ameonesha uwezo wake ila tukiunganisha na nguvu yako, pamoja tutashinda kwa muda mfupi. UBARIKIWE.
 
Siku zote imekuwa ni kawaida yetu sisi wana jamvi kupeana ushauri na kutiana moyo katika mambo mbalimbali yanajitokeza katika maisha yetu ya kila siku. Nafahamu kuwa humu tupo watu wenye itikadi na imani tofauti, ila wote tunamtegemea mola pekee, kwa imani hiyo naomba wana jamvi mnisaidie kumuombea mke wangu ambaye kwa muda wa miezi kadhaa sasa anasumbuliwa na mapepo wachafu (Majini) kiasi kwamba hata kazini ameshindwa kuhudhuria vile ipasavyo. Hivyo kupitia uzi huu na imani zetu naomba tumuombee kwa dhati.
Natanguliza shukrani.
Amen.

Kwa uzoefu nilionao mapepo hayaombewi kwa remote control. Hivyo ni vema ukampeleka kwa mhubiri wa injili, mchungaji aliyeokoka au mtu yeyote aliyeokoka ili amwombee ana kwa ana. Mungu atamsaidia mapepo yatatoka na atapewa ushauri wa nini cha kufanya ili mapepo hayo yasije yakamrudia tena. Kila laheri
 
mpeleke kwenye maombi ndugu atapona kabisaaaa.pelekea mwakasege huyo nimeshuhudia dada mmja amefunga tu ndoa akawa kichaa sasa hivi ni mzima kabisa anafanya kazi yake ya ualimu .waishi mkoa gani?
 
mpeleke kwenye maombi ndugu atapona kabisaaaa.pelekea mwakasege huyo nimeshuhudia dada mmja amefunga tu ndoa akawa kichaa sasa hivi ni mzima kabisa anafanya kazi yake ya ualimu .waishi mkoa gani?

Asanteni kwa ushauri mwema na sasa hivi tupo chini ya maombezi makubwa na mungu anatenda maajabu yake kwa kweli, la msingi ni kutaka kuwashirikisha nanyi wana jamvi kwani tumeshakuwa ni wanandugu.
NIVEA mimi nipo hapa Dar.
 
Kwa uzoefu nilionao mapepo hayaombewi kwa remote control. Hivyo ni vema ukampeleka kwa mhubiri wa injili, mchungaji aliyeokoka au mtu yeyote aliyeokoka ili amwombee ana kwa ana. Mungu atamsaidia mapepo yatatoka na atapewa ushauri wa nini cha kufanya ili mapepo hayo yasije yakamrudia tena. Kila laheri

Acha kuwa na imani haba, hicho unachokisema ni tofauti kwa maana unamwamini Ana kuliko MUNGU.
Hebu tuungane kwa pamoja na kumuombea mke wa Miwatamu kwa yale tunayoyaita maombi ya pamoja,
Ka mimi nitaanza saa 4 usiku na ningependa tuungane pamoja kumuombea kwa muda huo kwa yeyote atakayepata muda.
 
Kwa jina la yesu mapepo yanayamsumbua mkeo yatoke, ila wakati mnakwenda kwa watumishi wa mungu kwa maombezi zaidi na nyie pia ombeni kwani mungu huyo huyo anaemwamini mchungaji ndio na nyie mnatakiwa mmwamini kwani kwa imani kila kitu kinawezekana
 
Pole sana, unaweza kuwa unamuongoza ama kusema wote sala hii fupi nina imani atapona tu mkimtumainia yeye aliye juu, pamoja na kumpeleka kuombewa pia jitihada zenu ni muhimu:

Moto wa Roho Mtakatifu x7
Damu ya Yesu x7
Katika jina la Yesu x3
Baba wa Mbinguni ninakushukuru kwa kuwa ulisema katika Zaburi 50:15 kuwa nikikuita siku ya mateso utaniokoa na wewe utanitukuza.
Baba, ninakuita leo uje unikomboe nisiwaone watu hawa wageni tena, katika jina la Yesu.
Kila pepo lililojivisha sura ya ndugu aliyekufa, rafiki, dada au mke/mme (taja kile kinachohusika), ninakifunga na kutupa mbali na upeo wa macho yangu, katika jina la Yesu x3
Haijalishi ni jina gani unajiita, ninakukataa katika jina la Yesu.
NInakufunga ewe pepo ambaye hunijia mchana na usiku, ninakukataa na kukutupilia mbali na upeo wa macho yangu, katika jina la Yesu x3
Asanye Yesu kwa kunikomboa, katika jina la Yesu.
Amina
 
Pole ndugu, tupo pamoja katika hilo.
Mungu asikie sala zetu.
 
mungu amponye mpendwa, pia usichoke kumpeleka kwa wahubiri, Mwakasege bila shaka anaweza kusaidia kumrudisha katika hali ya kawaid

pole sana mkuu kwa majaribu
 
sala zangu zinaambatana nawe,, katika jina la unaemwamini Mungu moja, na atapata kupona believe and t will be yaz just wait when the rit time comes, maombi yetu yatajibiwa baki ukiomba nasi tukiomba nawe
 
Hayo mapepo na yashindwe, kwa jina la aliye mbinguni...............:A S-omg::A S-omg:
 
POLENI SANA NDUGU!!
But usiogope x365 kwa maana neema ya MUNGU ipo nanyi daima!
Simama imara usitetereke, nasisitiza tena usitetereke simama imara,
Chukua hatua madhubuti tangu sasa, msalimishe kwa Mungu kupitia kwa Yesu Kristo (japo sijui we ni mkristo ama muislam), ila mimi naamini katika kristo na hivyo nakuhakikishia lazima atakuwa salama ukimsalimisha kwake!
Pls usiyumbe, simama imara ongea na Mungu washirikishe na viongozi wa dini kwa namna moja ama nyingine!!
Soon utarejea hapa jamvini kwa ushuhuda wa uponyaji, AMEN.
 
Kwa Jina la Yesu ewe pepo mchafu toka na urud kuzimu,Damu ya Yesu imtakase mke wa Miwatamu na awe mzima tangu sasa,ktk Jina la Yesu awe huru,Amen
Tuko pamoja naungana na Saudari maombi ya kuanzia saa 4.
 
Maombi tu ndo yatamfungua. Kila la kheri, MUNGU AKAJITUKUZE KWENU. Tunangojea ushuhuda hapa.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom