Watanzania tumuombee Dkt. Tulia Ackson Mwansasu ashinde Urais wa IPU

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,305
9,734
Ndugu zangu watanzania,

Kwa unyenyekevu na heshima kubwa Sana nawaombeni watanzania kila mmoja kwa Imani Yake Tumuombee Mh Dr Tulia Ackson mwansasu Ashinde Urais wa IPU yaani umoja wa mabunge Duniani. Dr Tulia Ni spika wa bunge letu ,mpaka Sasa anaendelea kupata uungwaji mkono kutoka maeneo mbalimbali ndani ya Bara la Afrika.

Dr Tulia Ackson mwansasu Ni Dada msomi wa Kiwango Cha juu na nguli wa Sheria ambaye amekuwa Naibu mwanasheria mkuu wa serikali nafasi aliyoitumikia kwa uaminifu na weledi wa Hali ya juu Sana.Nyota yake kisiasa ilianza kung'ara Mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa 2015 ,Ambapo alipata bahati ya kuteuliwa ubunge na aliyekuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania awamu ya Tano Hayati Dr John Pombe Joseph Magufuli,Ambapo baada ya kuingia Bungeni kupitia mlango huo akapata bahati ya kuaminiwa na chama Cha mapinduzi kusimama Kama mgombea pekee ndani ya Bunge kuwania nafasi ya unaibu spika wa bunge letu na kufanikiwa kushinda kwa kishindo.

Aliongoza kwa mafanikio makubwa Sana, Ambapo ilipofika mwaka 2020 alitupa karata yake ndani ya CCM na kufanikiwa kushinda kwa kishindo katika kura za maoni ,na kupitishwa na kamati kuu ya CCM Taifa kupeperusha Bendera ya CCM Jimbo la Mbeya mjini,Ambapo alipita kwa kishindo kikuu na kurejea Bungeni Kama mbunge wa kuchaguliwa na wananchi na kupita Tena katika nafasi ya unaibu spika, na baadaye kuja kuwa spika wa bunge baada ya kujiuzulu kwa mh Job yuston Ndugai.

Dr Tulia Ni kiongozi mnyenyekevu Sana na mwenye moyo wa huruma na upendo Sana,ndio maana ukienda katika mkoa wa Mbeya hakuna mahali ambako hutakuta Alama za Dr Tulia,kila eneo utakutana na mikono ya Dr Tulia,kila sehemu utaona na kuonyeshwa juhudi na alama zake, Ni kiongozi aliyegusa maisha ya watu wengi Sana kuanzia yatima,watu wenye ulemavu ,wajane na wazee ame wasaidia Sana bila mipaka Wala kikomo,.vijana wengi Sana Mkoani Mbeya wamenufaika na kupata matumaini kupitia Dr Tulia,Ni yeye aliye wawezesha mamia kwa maelfu ya vijana mitaji ya kufungua biashara,ni yeye amewezesha mamia ya vijana kujipatia pikipiki mpya pamoja na bajaji bure kabisa kwa ajili ya kufanyia biashara na kusaidia familia zao na kuondokana na utegemezi wa kipato, Ni kupitia Dr Tulia vikundi vingi vya akina mama,vijana na watu wenye ulemavu walipatiwa mitaji ya kutosha,Dr Tulia ameleta nuru na Tabasamu kwa maelfu ya Wana Mbeya.

Dr Tulia ni Dada na kiongozi mwenye huruma Sana na msikivu wa Kiwango Cha juu Sana ,husaidia bila kujali eneo ,au Jimbo au mkoa .Ni kwa moyo wake huo wa upendo na huruma amewahi kusaidia mamia ya mabati katika shule ya msingi Mabatini inayopatikana katika mkoa wa songwe ,wilaya ya mbozi,mji mdogo wa mlowo,kitongoji Cha mabatini B.Alitoa msaada huo mkubwa kabisa bila kujali kuwa shule hiyo IPO katika mkoa na Jimbo jingine,akiwa na mh mbunge wa viti maalumu CCM mkoa wa songwe mh Juliana Daniel shonza walisaidia katika ukamilishaji wa vyumba vya madarasa yaliyo kuwa yanahitajika Sana kwa wakati huo.

Uongozi wa Dr Tulia umekuwa Ni kwa ajili ya kuwatumikia watu bila kujali itikadi za kisiasa,Wala eneo anakotokea mtu,maisha ya Dr Tulia yameleta furaha katika mioyo ya watu wengi Sana,amegusa maisha ya wengi Sana waliokuwa wamekata Tamaa na kuona Giza mbele Yao,siku zote amekuwa karibu Sana na watu,awapo jimboni au Mkoani Mbeya muda wote utamuona akiwa na wananchi wanyonge mitaani akitoa misaada ,utamuona muda wote akisaidia watu wenye Mahitaji maalumu,utamuona muda wote akisaidiana na viongozi wengine kutatua kero za wananchi,utamuona muda wote akiwatetea na kuwasemea Wananchi.

Ni kiongozi anayejuwa Nini maana ya maisha hasa kwa kuzingatia kuwa amekulia katika maisha magumu lakini akiwa na Imani IPO siku yatapita na Mungu atamgusa na kumuinua na siku moja atamfuta machozi mama yake na kugusa maisha ya watu wengine wenye kuhitaji msaada.Ni kiongozi asiye na kiburi Wala dharau wala ubaguzi na ndio maana husaidia Wote na kujumuika na wote ,Ni kiongozi mwenye kujishusha na kujinyenyekeza kwa watu,Ni mwenye hofu ya Mungu na mcha MUNGU Sana. Ni mwenye maadili mema na mwenye staha na heshima kubwa,anao uwezo mkubwa Sana wa kiuongozi na kiutendaji, anao uwezo wa kuwaunganisha watu na kujenga umoja na mshikamano,ndio maana kwa Sasa Mbeya haina mavurugu na badala yake inavuma na kusikika kwa maendeleo tu na miradi mbalimbali ya maendeleo inaendelea kuchipua na kufanyika .

Tufunge na kumuombea mtoto wetu, Dada yetu na kiongozi wetu Dr Tulia ili akashinde kwa kishindo na kutuletea heshima Kama Taifa kimataifa, Tuendelee kusimama Naye na kumpa faraja na nguvu za kusonga mbele. Itakuwa ni fahari kwetu watanzania akishinda uchaguzi huo unaofanyika mwezi October.Tumbebe katika mikono yetu na mioyo yetu kimaombi, Tumuombee kwa nguvu zetu zote na tuwashawishi wengine kutoka Mataifa mengine ili watuunge mkono kwa mtoto wetu wa kitanzania,Dada yetu imara ,msomi wa Kiwango Cha juu,mwenye msimamo usiyo yumba aweze kupita na kutuletea heshima.

Rai yangu Namuomba Dr Tulia dada yangu aendelee kumuomba mungu amtangulie katika safari hii ambayo sisi mamilioni ya watanzania tupo nyuma yake na tumembeba kimaombi, Aendelee kumtumainia na kumtegemea Mwenyezi MUNGU katika kila Hatua apigayo.viongozi wetu mbalimbali ngazi ya Taifa watumie ushawishi wetu kidiplomasia kumsaidia spika wetu kwa kila namna ikiwezekana hata viongozi wastaafu katika siasa katika ngazi mbalimbali wafanye ushawishi wa kidiplomasia kuhakikisha kuwa tunapata uungwaji mkono kwa Tulia wetu na kuzoa Kura za kutosha siku ya uchaguzi.mimi binafsi nitaendelea kumuombea Dada yangu kwa Imani yangu mbele za Mwenyezi MUNGU.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Tutamuombea

Hata Massele tulimuombea akashinda!
Hakika tuungane kumuombea Spika wetu aweze kushinda na kutuletea heshima Kama Taifa kimataifa.Tusimuache peke yake akiwa mpweke, watanzania siku zote yanapokuja masuala Kama haya kimataifa huwa Ni wenye umoja Sana na wenye ushawishi mkubwa Sana kimataifa ,.Hata katika hili naamini tunakwenda kushinda kwa kuwa Mungu yupo pamoja nasi
 
Itakuwa mkosi mkubwa sana !
Najuwa wewe siku zote una Vita na chuki yako binafsi kwa mh Dr Tulia,Hata hivyo maombi ya mamillioni ya watanzania yanayoendelea kutolewa na kumpatia baraka zote yatamuwezesha kushinda kwa kishindo.Taifa lipo na Dr Tulia, watanzania wapo Bega kwa Bega na Dr Tulia na Bara la Afrika linasimama na Dr Tulia na ndio chaguo Lao.
 
Ndugu zangu watanzania,

Kwa unyenyekevu na heshima kubwa Sana nawaombeni watanzania kila mmoja kwa Imani Yake Tumuombee Mh Dr Tulia Ackson mwansasu Ashinde Urais wa IPU yaani umoja wa mabunge Duniani. Dr Tulia Ni spika wa bunge letu ,mpaka Sasa anaendelea kupata uungwaji mkono kutoka maeneo mbalimbali ndani ya Bara la Afrika.
Tulia huyu huyu aliyeshiriki kupisha mkataba wa hovyo
 
Najuwa wewe siku zote una Vita na chuki yako binafsi kwa mh Dr Tulia,Hata hivyo maombi ya mamillioni ya watanzania yanayoendelea kutolewa na kumpatia baraka zote yatamuwezesha kushinda kwa kishindo.Taifa lipo na Dr Tulia, watanzania wapo Bega kwa Bega na Dr Tulia na Bara la Afrika linasimama na Dr Tulia na ndio chaguo Lao.
Thubutu ! labda kama Mungu kasinzia
 
Back
Top Bottom